Kwenu mnaoficha idadi ya watoto wenu

mawardat

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
23,950
131,282
Assalaam,


Ni hivi kuna mmama wa mwendo kasi hapa jirani,

Huyu mama kahamia hapa kasema ana watoto watatu na kiila mtoto na baba yake,

Akapata ka kijana akamuoa kwa ndoa na kazaa mtoto mmoja,

Eeeeh usiku si tunasikia mtu analia,na kutaja jina mwanangu mwanangu farida umeniacha

Watu kwenda kumuuliza kulikoni?? Akasema kafiwa na mwanae wa kwanza huko mwanza,na binti kaacha na watoto wawili,

Sasa na mume wake nae akabaki kushangaa maana kuhusu huyo mtoto hajawahi kuambiwa kama mke ana mtoto mkubwa na wajukuu,

Maana anashindwa kwenda msibani kumzika mwanae kwa ujinga wake,

Mmama kaumbuka vibaya ni aibu, maana raia wamejazana kwake si kwaajili ya kumfariji bali ni kumsanifu tu,


kweli Mungu fundi,


Mnafichaga idadi ya watoto wenu hili iweje??


Hapo tena mume atamuamini mke wake kweli??
 
Back
Top Bottom