Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 308
- 424
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mpango wa kuandika barua kwa mashirika ya kimataifa Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Ulaya (EU), Marekani (US), Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kikilalamikia mifumo ya uchaguzi.
Kulingana na Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, chama hicho kinadai mifumo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeunganishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa manufaa ya CCM.
Lakini historia yenye inaonesha kwamba barua na lundo la Malalamiko inaonesha wazi kwamba hayabadilisha chochote.
Tanzania ni taifa huru lenye katiba na mamlaka ya kujiamulia mambo yake. Jumuiya za kimataifa, hata zenye ushawishi mkubwa kama UN, haziwezi kufanya kazi ndani ya nchi bila ridhaa ya serikali husika. Hii ni kanuni ya msingi ya kidiplomasia uhuru wa mataifa (sovereignty),na Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuilinda.
Historia ya Malalamiko ya CHADEMA nje ya nchi
CHADEMA imekuwa na rekodi ndefu ya kutumia njia ya barua na malalamiko kwa mashirika ya kimataifa. Mifano kadhaa inathibitisha namna juhudi hizo zimekuwa zikikosa matokeo tarajiwa.
Sheria za Uchaguzi: Mwaka 2019, CHADEMA iliandika barua Umoja wa Mataifa kupinga marekebisho ya Sheria ya Uchaguzi, wakidai yalilenga kubana upinzani. Hata hivyo, hakuna hatua iliyochukuliwa, na mabadiliko hayo yalitekelezwa kwa mujibu wa bunge na mamlaka ya kitaifa.
Kuhamishwa kwa wamasai Ngorongoro: KKatika hatua na mkakati wa serikali kulinda hifadhi ya Ngorongor, CHADEMA na mashirika ya kimataifa na washirika wengine walipeleka malalamiko UN wakipinga mpango wa serikali kuhamisha baadhi ya wamasai hao kutoka kwenye hifadhi. Licha ya mijadala mikali, serikali iliendelea na mpango wake, na chadema haikuambia kitu.
Mikopo ya nje: CHADEMA pia iliwahi kuandika barua kwa taasisi za kifedha za kimataifa kama IMF na Benki ya Dunia (WB) kuomba mikopo ya maendeleo isimamishwe. Lakini mwaka 2021 na 2022 pekee, Tanzania ilipokea zaidi ya USD 1.3 bilioni kutoka IMF kwa ajili ya kufufua uchumi baada ya janga la COVID-19. Hii ilionyesha kwamba taasisi za kifedha huangalia uhalali wa miradi na uwezo wa taifa kurejesha fedha, si shinikizo la vyama vya siasa.
FIFA na CAF dhidi ya Yanga: Hivi karibuni, baada ya klabu ya Yanga kuchangia shilingi milioni 100 kwenye harambe ya CCM ya kuchangia za uchaguzi wa mwaka huu, CHADEMA walilalamika FIFA na CAF wakidai ni ukiukwaji wa misingi ya michezo kwa klabu kushiriki siasa. Lakini FIFA haikuchukua hatua yoyote, kwa sababu haina mamlaka kuingilia masuala ya kisiasa ya ndani pasipo ushahidi wa uvunjifu wa kanuni zake.
Kwanini nasema ni sawa kupaka rangi upepo?
Sababu kuu za Chadema kuangukia pua mara kwa mara ukweli kwamba hakuna taasisi ya kimataifa itakayohatarisha uhusiano wake na Tanzania kwa ajili ya malalamiko ya chama kimoja cha siasa.
Tanzania ni nchi yenye uchumi unaokua kwa wastani wa zaidi ya 5% kwa mwaka, na ni kitovu cha biashara katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
Diplomasia ya Tanzania inajengwa juu ya misingi ya kutoshirikiana na mashirika yanayoweza kuhatarisha uthabiti wake wa ndani. Ndiyo maana, mara zote, barua za CHADEMA zimeishia kuwa maandiko yasiyo na impact yeyote. Kwa wa kihistoria na takwimu, barua ya CHADEMA kwa UN, US, EU, AU na EAC hazitazaa matunda yoyote, wanafanya kazi ya bure isiyo na matokeo kama vile kupaka rangi upepo.