Maamuzi ya Bunge kuwafungia wabunge kuhudhuria vikao ni ukiukwaji wa KATIBA

Ni lazima wahanga wa suala hili wawaburuze mahakama kuu Spika na AG wakajibu kwanini wanawapora wapigakura kwenye majimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa.
Hili neno umelitoa kwenye hazina bora ya ubongo wako.
Asante mtanzania.
Huko mahakamani waombe sasa waruhusiwe kuingia bungeni kuzikabili hoja zinazowahusu jimboni kwao moja kwa moja.
 
Una hoja but you have a missed a point kwa kutoa conclusion.

Hoja yako umeinyima haki ya kudadavuliwa na wajuvi wa sheria na katiba kwa hoja yoyote inayokinzana na conclusion yako inaweza kuzua malumbano yasiyokuwa na tija.

BTW una nafasi ya kuirekebisha kwa kufanya editing ambayo itaifanya iwe hoja chokonozi badala ya hoja inayohukumu.
Hukumu ni sehemu ya common sense, Rutashubanyuma yupo sahihi
 
Haki ya wabunge kuhudhuria vikao na kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao ni ya kikatiba na kanuni feki za Bunge zinazolipa Bunge mamlaka ya kuwasimamisha wabunge kutekeleza majukumu yao ya kikatiba zinakiuka katiba ambayo wabunge hawa waliapa kuilinda na kuitetea Katiba husika!

Bunge halipo juu ya katiba na ndiyo maana wabunge wote huapa kabla ya kuanza shughuli za Bunge ya kuwa wataitii katiba ambayo hakuna mahali ndani ya katiba hiyo wamepewa mamlaka ya kuwasimamisha wabunge na kuwapora wananchi wanaowawakilisha haki yao ya kikatiba ya uwakilishi.

Tusipokuwa waangalifu itafikia wakati Bunge linamsimamisha Mbunge kwa miaka mitano na kuwapora wananchi wa jimbo husika haki yao ya kikatiba ya kuwakilishwa kwa kipindi chote cha uwakilishi.

Adhabu za kikanuni za Bunge hazina mamlaka ya kupora wananchi haki zao za kikatiba kama kuwakilishwa.

Kama Mbunge kavunja kanuni Bunge linaweza kumpa faini ili aathirike Mbunge mwenyewe bila kuathiri haki ya kuwakilishwa ya wananchi wa jimbo lake.

Spika Job Ndugai kuwaadhibu askari walioheshimu haki za binadamu pia linatia aibu si kwake tu bali kwa Bunge zima na taifa kwa ujumla.

Acha porojo nyingi elezea kipengele cha katiba
 
View attachment 520010View attachment 520011View attachment 520012

Watanzania sisi ni watu wa ajabu kabisa na ni watu wa kuhurumiwa sana.

Ni majuzi juzi tu kuna watu kwa maelfu yao walikuwa wanatamani Mh Spika Ndugai apone na aje kuliongoza (??) Bunge, wengi wakimwona Naibu Mh Tulia kama nuksi.

Niliwaonya na kuwaeleza (hapa na pale) bayana kuwa Ndugai na Tulia ni sawa sawa na rangi ya tui la nazi na maziwa. Je sasa hivi niwaulize tena wale waliokuwa wanatamani Ndugai akalie kiti maoni yao ni yepi? Je ameliboresha Bunge au limebaki mfu, kibogoyo na ukumbi wa michapo na vijembe?

Tunahitaji katiba MPYA inayotokana na Wananchi wa Tanzania. Huo ndio muarobaini pekee sahihi kwa matatizo lukuki tuliyonayo kila kona.

Leo kila kiongozi ni mungu-mtu kila mahali. DC leo ni zaidi ya chief wa kabila, RC ni zaidi ya untouchables "walioshika hatamu", Spika na Naibu ni zaidi ya makerubi na Rais ndo usipime.....jamani tunaelekea wapi???? Leo eti wao wanaamua kila kitu (kibaya au kizuri) kwa vile tu wana madaraka lakini sio kwa vile wamebeba maslahi yetu au ya Taifa letu. Wanaamua tu, wanaamrisha tu, hawajali kitu wala hawana hoja wala uwezo wa kufikiri vema bali kutimiza matakwa yao. Je kwani matakwa yao ni yetu? Ni wapi tunapokutana na kauchana kifikra na kimaslahi?

Leo hii eti Serikali inaahirisha mitihani bila hoja za msingi, mara eti wamepiga marufuku tuisheni ya wanafunzi (hawataki wanafunzi wasome zaidi ya lecture ya darasani eti kana kwamba elimu inayotolewa darasani (??) ina ubora na virutubisho vyote muhimu kwa afya ya elimu ya wananfunzi, na eti hawaihitaji kusoma zaidi) Taifa gani hili? Mnatengeneza watu duni, malimbukeni kwa elimu mbovu ili mje mshindane na nani sasa? Mnatengeneza mambumbu kwa kuifanya hovyo elimu yetu iwe tu ni kwa ajili ya mitihani basi i.e. (STD 4 & STD 7), wakati ukweli ni kuwa elimu ni zaidi ya mitihani.

Hawa creamers ni shida, kweli kuwa na viongozi wasio na maono ni laana kwa wananchi na Taifa letu. We gotta chase 'dem away, chase 'dem out of town........ send 'dem to the pit!
 
Adhabu waliyopewa ni kubwa mno ukilinganisha na kinachosemwa utovu wa nidhamu. Tujenge utamadamuni wa kuvumiliana na kupunguza jaziba kwenye mambo yasiyo ya msingi kwenye mambo ya msingi.
 
kanye urudi kitandani ulale mambo ya sheria na katiba yaache hujui kitu.
Mwenzetu ambaye hunyi kitandani na kulalia kinyesi chako hebu nielemishe nipate shule ya nguvu hivi ni maeneo yapi ys sheria na kikatiba siyajui.

Ukiondoa mapovu yako hujachangia lolote lile la maana
 
Kwa hili Raisi wa TLS Mhe. Lissu chama chenu kisipoonyesha njia basi acheni zile mbembwe zingine baada ya hapa.
Hatutetei maovu lakini haki kwa wote ionekane imetendeka. Yaliyowakuwa Mnyika,Mdee na Bulaya ni defense yao ndiyo imegeuzwa kuwa Kosa.
Pili haki ya wapiga kura kuporwa haiko sawa Kikatiba. Kanuni ya Bunge iko kinyume na Katiba ya Nchi .

Adhabu kama kuwanyima Posho na marupurupu mengine ndiyo sahihi na si kuwakilisha waliowapeleka Bungeni.
Ninaafiki hoja. TLS kama kweli wako makini kama tambo zao zinavyotujuza basi waanze na hili
 
Issue kubwa hapo ni kwamba CCM inajaribu kumficha KAlemani kwenye MAOVU ya mikataba na miswada mibovu kwa maana ndiyo sababu ya kuwepo kwake.

Kama kweli CCM wangekuwa wazalendo wasingepigia makelele makombo wakati wageni wanachukua chakula chote,halafu tunakuwa kama mazuzu kupigia makofi RAIS anayetaka tujadili makombo ya madini.Aibu kwa TAIFA masikini kama letu kupigia makofi ati RAIS ana uchungu sana kuona tunanyimwa asilimia kubw akwenye makombo ya chakula.Upumbavu wa hali ya juu kabisa wa hili bunge letu
Unapokuwa na wabunge kama Lusinde ambao kazi yao ni mipasho na vijembe unatarajia nini?
 
Nenda ukapigie makofi Makombo kule bungeni.Badala ya kuhoji haki za msingi za madini yetu MINARA/MICHE ya dhahabu uanpiga kelele kwenye makombo aibu jingalao,toka huko hatuhitaji makombo watanzania,madini mali yetu tunatakiwa tupigie kelele MICHE ya dhahabu.
Wako humu ndani ccm mercenaries ambao kazi yao ni kubeza ukweli
 
Kuwafungia wabunge watumiaji madawa ya kulevya si kosa, sema tu aliwaonea huruma maana ilibidi awahukumu wanyongwe ili kuwa fundisho kwa wabunge wengine. Madawa ya kulevya si peremende.
Kwa kuongozwa na katiba na sheria zipi? Kuhoji mikataba na sheria fedhuli siyo ulevi wa bangi bali ni uzalendo
 
Bahati nzuri katiba inatambua kwamba kuna kanuni na sheria nyingine ndio maana huwa inasema "BILA KUATHIRI KANUNI NA SHERIA ZINGINE ZA NCHI" Kwa maana hiyo hakuna katiba iliyokiukwa.
Hakuna mahali katiba imetaja neno KANUNI, pili sheria au kanuni yoyote inayopingana na Katiba ni batili.

Huwezi ukatetea Bunge kuwazuia wabunge wa upinzani kushiriki vikao vya Bunge.

Huo ni ubaguzi, uonevu na mbaya zaidi ni dhuluma dhidi ya majimbo ambayo wabunge hao wanayawakilisha.
 
Hili neno umelitoa kwenye hazina bora ya ubongo wako.
Asante mtanzania.
Huko mahakamani waombe sasa waruhusiwe kuingia bungeni kuzikabili hoja zinazowahusu jimboni kwao moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom