Wajibu wa kujenga nidhamu bungeni ni wa wote; Kiti na wabunge. Kama uko huru kifikra ni rahisi kuona kwamba siku ya tukio Kiti chenyewe kiliandaa mazingira ya kutokea kwa kilichotokea. Kwa kadri ya mambo yalivyokuwa Kiti ambacho kinajua wajibu wake kisingeenda kujificha kwenye Kanuni bali kingemsikiliza Mnyika na kuahidi kufuatilia ili kujua ni nani aliyemtolea tusi la kwamba yeye ni "mwizi", basi. Na mambo yangeendelea kama kawaida! Nadhani Prof. Shivji aliposema Bunge halipaswi kuendeshwa kama darasa la wanafunzi alikuwa sahihi. Kiti kinataka kuliendesha Bunge kama vile darasa, tena nadhani la chekechea!
Mnyika alipewa nafasi na Ndugai kuomba mwongozo kuhusiana na mchango wa Lusinde,ipitie upya hoja ya Mnyika ujiridhishe kuwa alichokuwa anazungumza ndicho alichoomba,akakumbushwa.Akapuuza,akaambiuwa umeeleweka keti Lusinde aendelee na hoja yake akagoma ungekuwa spika ungeruhusu mgomo wa Mnyika uendelee?
Tukubaliane kwa manufaa ya kuhitimisha hoja Ndugai tuseme alikosea akaamrisha Mnyika atolewe nje,je ilikuwa busara wah. Wabunge wawili wanawake kutaka kupigana na askari ili Mnyika asitolewe nje.
Askari wa bunge wangekuwa wavuta bangi wakaamua kuwaonyesha kuwa wana nguvu kuliko wah.wawili wale nini kingetokea?
Je ni busara kwa mh.Mbunge anapohisi kuonewa au nduguye kuonea kujitetea kwa kutumia nguvu zake na siyo akili zake? ndicho tunachotak kufundisha watotot wetu?