Maalum kwa watoto wa wakulima tu!

umenikumbusha miaka ya 1977 asubuhi wakati mnakamua maziwa viazi vinakuwa tayari kwenye moto aina kikome ukimaliza kukamua unachukua maziwa yako na viazi maziwa ni mabichi hakuna kuchemsha wala nini ukitoka hapo tumbo limejaa ukienda kuchunga usingizi wake maziwa yameganda tumboni ni full kusinzia ukijisahau mifugo iparamie mazao ya watu utapewa bakora za kutosha jioni unakutana nazo tena nyumbani
Duh mwaka 77! long time
 
View attachment 515775Hiyo ndio kabungila unakoka moto hilo tanuru hayo mawunguluma aka mabonge ya mchanga yanapata moto kiasi cha kuwa mekundu then unaweka mbatata humo ndani zikitoka hapo ndo lunch ya kijana mchungaji wa ng'ombe. ..Aina hii ya msosi vijana tuliokulia machungani hususani kule Mbeya Mbozi na kwingineko tumeinjoi sana enzi hizo
Oven ya kiafrika.
 
Siku hizi watoto wanadeka hawataki kula soseji full kubembelezana ha ha ha ha ha ha ha
 
nooo moom I don't like riicee, enzi zetu hujamaliza kusema ushalamba kofi moja amezing na kujibamiza ukutani na ndio utalala njaa hivo!
 
Wakati mwingine ilikuwa ni mchana na usiku kama dozi vile ilhali wengine huko mjini wanavitumia kama vitafunwa vya asubuhi pekee.
Msimu wa Kiangazi nafaka zikipungua hii huwa ndo menu kuu, unagonga vitu unashushia na Maji bariiidii ya kisima ukitoka hapo unaenda mtaa wa kati kutafuta wanzuki
 
Hivyo vitafunwa vimeniharibu saana mkuu.. leo siwezi kula kitafunio chochote nikajihisi nipo poa
mkuu mimi sijavila udogoni kutokana na mazingira niliyokulia, ila huku ukubwani sasa katika siku saba za wiki labda mkate nitakula siku mbili tu, lakini kinywea chai kikuu kwangu ni hayo mandoo ( viazi vitamu)
 
Back
Top Bottom