Maalum kwa wababa

bukerebe alex

Member
May 5, 2016
62
80
Habari Wana JF
Nilidhani ubaba ni kitu cha kawaida asee nilivyokuwa namuona mzee wangu akipambania familia yake pindi nakua nilidhani anatuhujumu. Ila nimegundua alikuwa nasi kuanza anaamka mpaka analala. I am proud to have him..

One day miaka fulani hivi baada ya mama kututoka mzee alinunua dagaa kisado na akasaga debe mwanzoni mwa mwezi hapo tupo wawili mie na dogo langu. Basi bana baada ya kununua vile vyakula nikamaindi kinoma hadi nikamfata personally kumblame, kwanini anatupa constant food mwezi mzima. Akaniambia ujue we pia utakuwa baba one day utajua namaanisha nini.

After 5 years today naona he was very very correctly. Baada ya mie pia kuwa na familia na kuipambania ili wale kila siku. Nilimkumbusha one day alinicheka Sana akasema hayo ndio maisha ya mwanaume aliye na familia..

Uzi huu nauanzisha ili tulio wababa woote tupeane experience namna ya kuhandle familia.

Karibuni Sana wadau so that we can share our beloved father's experience
 
Mara nyingi mwanzoni huwa hatueleweki Ila mwisho wa Mambo Aidha ukiwa hai au umekufa ndo utasikia Bora father angekuwapo.
 
Daaa! Umenikumbusha kitu ambacho baba alikfanya nikiwa mdogo nilishangaa sana kwa kipindi hicho, kwa nn anafanya hii kazi !!

Leo hii kile kitu kimenijenga ktk fikra. Wakati ninafanya hiyo kazi nilimweleza mke wangu hii kazi baba aliwahi fanya kumbe ni kwa masilahi ya ustawi wa afya ya watoto wake na leo hii nimefanya watoto wangu wameona na wamenishangaa sana tu nikiwa na mama yao!
 
Habari Wana JF
Nilidhani ubaba ni kitu Cha kawaida asee nilivyokuwa namuona mzee wangu akipambania familia yake pindi nakua nilidhani anatuhujumu.. Ila nimegundua alikuwa nasi kuanza anaamka mpaka analala. I am proud to have him..

One day miaka fulani hivi baada ya mama kututoka mzee alinunua dagaa kisado na akasaga debe mwanzoni mwa mwezi hapo tupo wawili mie na dogo langu. Basi bana baada ya kununua vile vyakula nikamaindi kinoma hadi nikamfata personally kumblame, kwann anatupa constant food mwezi mzima. Akaniambia ujue we pia utakuwa baba one day utajua namaanisha nn.

After 5 years today naona he was very very correctly. Baada ya mie pia kuwa na familia na kuipambania ili wale kila siku. Nilimkumbusha one day alinicheka Sana akasema hayo ndo maisha ya mwanaume aliye na familia..



Uzi huu nauanzisha ili tulio wababa woote tupeane experience namna ya kuhandle familia.

Karibuni Sana wadau so that we can share our beloved father's experience
Nilikua namuomba mshua pesa za shule miaka ya 1993 huko, sometimes ananitoa na mala ananichapa kibao ananiambia nenda shule, nikaanza maisha ya kujitafutia mwaka 1996 to date, aisee ni nouma... Hakuna siku familia yangu isihitaji chakula, mavazi, afya na mengineyo mengi toka nimekua nayo kuanzia 2005,ila niseme tu wazi kwamba tunajitahidi sana na MUNGU anatupigania mbaya kabisa. Sometimes nafunguliwa geti nitoe kiStarlet changu nje nisepe kwenye mihanjo, majirani wananitazama kwa namna ya mtu aliyefanikiwa sana, kimoyo moyo nasema Asante MUNGU ila bado niko na shida kibao, nikikaa nikatafakari wanachoniona nacho watu na nikikumbuka nilikotoka, na majukumu niliyo nayo sasa hivi, hua ninamazoea ya kusema kimoyo moyo "MUNGU nisaidie na kuniokoa ili watoto wakue.

Hakuna kama BABA
 
Dah huu uzi umenifanya nimuonee sana huruma dingi, kipindi kile niko dogo nilikua sijielewi yale ,aisha yakukompea na majirani, eti baba fulani kannunua tivii sisi hatuna nikawa namchukia dingi bila sababu,

Kuna siku nilikua napiga stori na anko akaniadithia kua mshua alikua ikifika likizo yeye hapumziki anaenda magodown kufanya vibarua mpaka likizo inaisha anarudi job daah niliumia sana,

Kifupi ngoja wikiendi niende nikamuangukie asee.
 
Mzee wangu namkumbuka kwa mengi.
Ila nikiwa dogo nilimkuta kakaa kwenye kimsingi cha home akaniambia mwanangu kichwa kinaniuma upande mmoja...nikamuuliza kwanini?!akaniambia mko sita humu ndani wote mnahitaji ada....nazipata wapi.
Mwisho wa siku wote tulirudi shule....ila Mungu wa mbinguni amrehemu huko alipo maana kwenye suala la kutupatia elimu alifaulu asilimia mia.
Salute kwa baba wote waliohai na waliotangulia mbele ya haki.
 
Kama sio baba yetu kutufuatilia shuleni nisingekuwa hapa nilipo.
.
.
Sisi tumesoma St. Kayumba kuanzia shule ya msingi ila niliweza kushindana na yeyote aliyesoma international schools.
.
.
Nyumbani ilikuwa kazi na shule. Lakini pia mimi baba ndiye aliyenifundisha kuendesha baiskeli, kucheza mpira wa miguu, basketball, etc
.
.
He was an all round ever present figure in my life growing up
.
.
Kikubwa, FAMILIA YAKO NI MAAMUZI YAKO, IPE KIPAUMBELE.
.
.
Hakuna mtu alikulazimisha kuwa na mke au watoto ulionao. Usiwafanye kama nyongeza kwenye maisha yako, wafanye kipaumbele. Huo ndo ujumbe wa mzee wangu kwetu.



Sent from my SM-G950U1 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante kwa Baba yangu pia alinipenda na anaendelea kunipenda sana na mpaka nami nilivyokuwa Baba nami naipigania familia yangu Mungu ni mwema na namshukuru sana.
 
Du kiongozi ungeweka tu kwa wamama pia waone maana kila mara utasikua nani kama mama. Nilichojifunza kwa wazazi wangu wote baba na mama walikuwa wakipendana kwa hali ya juu na kushirikiana kwa dhati kutulea kwa upendo. Nani kama mama na baba. Sema sisi wazazi wa karne hii ni majanga.
 
Back
Top Bottom