Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

Kama kuna chama ambacho msajili anapaswa kukifuta haraka basi ni CUF. Haiwezekani mtendaji mkuu wa chama anahubiri waziwazi tena bila kificho utengano wa kitaifa halafu anatazamwa tu!

Tanzania ni moja na mipaka yake lazima ilindwe kwa gharama zote. Hoja zake alipaswa azitolee kama mwananchi wa kawaida kwenye Tume ya Katiba na sio majukwaani. Tendwa upo?

Kaka hayo ni mawazo binafsi ya Maalim seifu,sasa chama cha cuf kifutwe kwasababu kinaukataa mungano,kwanini kisifutwe chama cha CCM kwa kung'ang'ania mungano usio na mwelekeo kwa pande zote mbili,je na chadema nacho kifutwe kwa kuwa na sera ya serikali tatu

waswahili wanasema wenye nguvu wape hapa utaona kisiasa CCM wako peke yao kwa huu msimamo wao wa mungano,kwa mantiki hiyo CCM cdio chama kinachotakiwa kifutwe
 
Maalim Seif Sharif Hamad ahutubia mkutano mkubwa wa hadhara kisiwani Pemba hii leo na anasema:

"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba.

Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje. Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna.

Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau
hilo.

Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu. Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili.

Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa Kw
maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni.

Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."


Kama utasoma kwa Umakini Speech hii utaona Dhulma wanayofanyiwa wazanzibar na CCM
Kwa staili hii hata maadui watakuheshimu Maalim Seif .
 
Mkuu ubarikiwe sana kwa kuiweka vidio hii nimeisikiliza kwa makini maalim seif anatisha mi nilijua yupo ktk serikali haongei kumbe anamwaga vitu balaa kweli maalim anatafuta ukombozi wa wazanzibar uwe unatuwekea vidio zake mana ktk tv hawatoi
Lakini mkuu yeye ndo aliuchelewesha muungano wa kweli kwa kumsaliti mzee jumbe.
 
huvi kuna nini kilichojificha katika muungano huu ambacho hakitakiwi kijuilikane mpaka inafikia mtu akiamua kuuzungumzia anatiwa hatiani na kuonekana kama anatenda dhambi?! Inawezekana ile dhana ya sheikh ilunga hassan ya kwamba zanzibar inatawaliwa na watanganyika kwa 'mfumo kristo' kupitia mgongo wa muungano hapa ndio inajidhihirisha! Na ndio maana wazanzibari hatuipendi chadema, na itakua ni ndoto chama hichi kua cha kitaifa mpaka tutakapojitenga na watanganyika.

swadakta
 
Wengi munazungumza kwa jazba. Ukweli ni kuwa Jaji Warioba ameleta kitu ambacho wahafidhina hawakufikiria kinawezekana. Sasa ni kujipanga kwa maslahi ya kizazi kipya.
Serikali mbili zimepitwa na wakati na serikali moja haiwezekani. Tungeliweza kuishi kwa usalama kama ingelikuwa kuna haki sawa na heshima kwa pande zote mbili. Manung'uniko ya muungano yameleta kero za muungano ambazo kila leo zinazidi kuongezeka.
Miaka hamsini serikali imeshindwa kutatua kero. Kwanini tufikiri kero zitatatuka sasa.
Bila kuijua historia ya muungano ni vigumu kuthamini mchakato huu.
Wengi wanaopinga serikali tatu au mamlaka kamili hawafahamu kinachowasibu watanzania au wazanzibari walala hoi. Wiki hii viongozi wakuu bara wamekwenda visiwani kununua ardhi. Tuwaulize wanafikiria kuna nini ambacho sisi hatukijui kinacho wafanya kukimbilia huko?.
Siasa ni mchezo mgumu kwa wenye fikira fupi. Tuna kura "referendum" baada ya kupitishwa hiyo rasimu. wananchi wataamua.
Na pia lazima ipate 2/3 ya bunge la bara na baraza la wawakilishi vinginevo haipiti. Kwa hivo tusubirini tuone tutafika wapi. Litakalo tokea lolote, muungano kama ulivo haupo tena. Mabadiliko yanakwenda na wakati. Usipokubali kubadilika, wakati utakubadilisha.
 
Namshangaa analalamika wakati yeye ni sehemu ya serikali ya zanzibar na ndio wenye maamuzi na zanzibar yao.

Hapana HANA MAMLAKA YOYOTE, mwenye mamlaka ni Makamu wa pili wa Rais! Yeye ni kama picha tu au danganya toto ya UMOJA WA KITAIFA.
Sijui nitapigwa "ban" kwa comment hii...
 
Hapana HANA MAMLAKA YOYOTE, mwenye mamlaka ni Makamu wa pili wa Rais! Yeye ni kama picha tu au danganya toto ya UMOJA WA KITAIFA.
Sijui nitapigwa "ban" kwa comment hii...

Kama ni kweli hii hatari, inamaana yeye majukumu yake ni yepi hasa.

Au raha yake ni kuongozwa na misafara ya ving'ora.?
 
Maalim Seif ndie kiongozi wa wananchi wa zaznzibar kwa KURA. Dr. Schein ni kiongozi wa Zanzibar kwa KUTANGAZWA.
Inajulikana na kila Mzanzibari kuwa Maalim Ndie aliyeshinda kwa zaidi ya 72% ya kura za wazanzibari isipokuwa kwa vishindo vya Mkapa na Ali hasani Mwinyi, ilibidi Maalim arudi nyuma kwa usalama wa raia wa Zanzibar.
Siku ile waliletwa majeshi kutoka bara na Ali hasani akasema yeye hajali hata wakiuliwa watu mpaka damu zikafika kitovuni lakini lazima Schein awe raisi.
Kwa hekma kubwa Raisi Amani Karume akaongea na Maalim, kuinusuru Zanzibar, asiuliwe hata mtu mmoja. Ndio maana ukimuona Maalim anaongea "with full confidence" sababu anajua Shein amewekwa kidhulma tu.
Wazanzibari wanazidi kuichukia CCM kwa dhulma wanayoifanyia Z'bar. Unachokipnda ndicho utakacho kivuna.
 
Swala ni kuifuta katiba ya "smz", mana nayo ni tatizo kwa watanganyika.
 
mwenye wimbo wa taifa wa z'bar au-copy na ku-paste hapa, pamoja na kifungu cha katiba kuhusu mamlaka yake kama dola/nchi.
 
Kwani z'bar inataka mamla kamili kutoka wp? Nachojua zbr itaendelea kuwa sehemu ya mabeberu wa tanganyika.seif km unataka z'bar huru uondoke visiwani alisema dr.shein.chezea wababe wa ccm nini? Hakuna cha mamlaka au dola huru zanzibar mbele ya makaburu ndani ya sisiemu
 
Sidhani kama huyo jamaa anawasemea wapemba na waunguja zaidi kusaka madaraka kunamtesa
 
Maalim Seif Sharif Hamad ahutubia mkutano mkubwa wa hadhara kisiwani Pemba hii leo na anasema:

"Mimi sitafuni maneno kwamba ni muumini wa Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa itakayofuatiwa na mashirikiano kati yake na Tanganyika kupitia Muungano wa Mkataba.

Namshangaa leo anakuja kiongozi wa Zanzibar anasema tuna bendera na muhuri na wimbo wa taifa, hayo yanatosha. Hivi huyu anajua anachokisema au anatumikia maslahi ya waliomtuma? Una bendera gani hii ambayo mwisho wake Chumbe? Mimi nataka niione bendera ya Dola ya Zanzibar inapepea Umoja wa Mataifa, New York pale. Nataka tuwe na Paspoti ya Zanzibar, nikisafiri nitoe Paspoti ya nchi yangu. Nataka tuwe na Ofisi za Kibalozi za Zanzibar katika nchi za nje. Leo hata mamlaka ya kiuchumi hatuna.

Tumeamua rasilimali yetu ya mafuta na gesi asilia yasiwe mambo ya Muungano, mpaka leo Tanganyika wamekwamisha, wanatuzuia tusinufaike na rasilimali zetu tukajenga uchumi wetu. Wanasema tuna viwango na mfumo mmoja wa kodi lakini bidhaa zikitoka Zanzibar wanazitoza ushuru tena. Lengo ni kuua uchumi wetu ili hatimaye tudhoofike na tusalimu amri kwao. Yaguju! Wasahau hilo.

Leo hata katika mikutano ya kimataifa, viongozi wetu wa Zanzibar hawapewi heshima ya uwakilishi wa nchi yetu. Inafika mahala hata Naibu Waziri tu wa Bara anaongoza ujumbe wa Tanzania wakati kuna Waziri kamili kutoka Zanzibar lakini haheshimiwi. Tutarejesha mamlaka yetu kamili.

Tuwe na Benki Kuu, tuwe na sarafu yetu ya Zanzibar, tupange uchumi wetu kwa maslahi ya watu wetu. Tunataka tuwe na uanachama katika jumuiya na mashirika yote ya kimataifa. Tuwe na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zanzibar. Tuwe na uwezo wa kuingia mikataba na nchi za kigeni.

Hayo ndiyo tunayoyataka. Tukisema hivi hatuna maana tunataka ugomvi na Tanganyika. Hapana! Tunataka tuwe majirani wema na Tanganyika kama tutakavyokuwa na ujirani mwema na Kenya. Hayo yatafikiwa kupitia Muungano wa Mkataba wa Madola mawili huru kamili."


Kama utasoma kwa Umakini Speech hii utaona Dhulma wanayofanyiwa wazanzibar na CCM
Aache ujinga yeye si ndio aliwasaliti wenzake walipotaka kuvunja muungano kwa kuandika barua UN badala yake akamwambia Nyerere deal likafa
 
Maalimu ndiye mwanasiasa anayenistaajabisha sana kwa kufanikiwa kuvuta ufuasi mkubwa huku akiwa na historia yenye misimamo tata sana ya kisiasa. Sijui amewezaje kuaminika kiasi hicho. Namuona kama ni mtu mbinafsi aliyefanikiwa kuhamisha akili za wafuasi wake toka kwenye mantiki hadi kwenye unazi usiomithilika. Watu wamejitoa mhanga wa damu huku yeye akijiunga na wadhulumaji kwenye utawala bila simile kwa kisingizio cha muafaka wa kitaifa! Sijui kama fidia kwa wahanga wa 2001 ilikuwa sehemu ya mjadala kufikia "muafaka wa kitaifa". Hata madaraka yake hayakujadiliwa bali iliachwa kwa Rais (wa CCM) kumpangia majukumu!

Nikichukulia kuwa ndiye kielelezo kikuu cha Wazanzibari kutaka mamlaka kamili ndipo ninapofikia hitimisho kwamba tusahau kabisa habari ya muungano; uwe wa serikali moja, mbili, tatu, n.k. Badala yake tutafute tu muafaka wa nchi zetu mbili kubakia na ushirikiano wa kimaslahi nje ya muungano.
 
kaka hayo ni mawazo binafsi ya maalim seifu,sasa chama cha cuf kifutwe kwasababu kinaukataa mungano,kwanini kisifutwe chama cha ccm kwa kung'ang'ania mungano usio na mwelekeo kwa pande zote mbili,je na chadema nacho kifutwe kwa kuwa na sera ya serikali tatu

waswahili wanasema wenye nguvu wape hapa utaona kisiasa ccm wako peke yao kwa huu msimamo wao wa mungano,kwa mantiki hiyo ccm cdio chama kinachotakiwa kifutwe

mkuu jaribu ku up date ubongo wako. Tendwa sio msajiri wa vyama vya siasa pia shariff hamad hazuiliwi kujadili lolote kuhusu mijadala ya msitakabali wa taifa letu.
 
Back
Top Bottom