Zanzibar 2020 Maalim Seif Sharif Hamad unataka kutugawa Watanzania kwa faida ya nani?

“Mimi sioni tabu kumwambia (Magufuli) tugawane mbao”. Haya ni maneno aliyoyatamka Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mkele, Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.

Kauli hiyo ameitoa sambamba na kauli zingine nyingi ambazo zinaonesha dhamira ya dhati ya Maalim Seif Sharif Hamad kuvunja Muungano endapo tu atachaguliwa kuwa Rais katika Visiwa hivyo.

Ameendelea kusema hata kama Rais Magufuli atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi atamwambia Rais Magufuli abaki na Tanganyika na yeye (Maalim Seif) Zanzibar. Hii ni kauli inayoashiria wazi kuwa Mgombea huyu hana nia njema na Muungano ambao umedumu na kuenziwa na Marais wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar, kwa takribani miaka 56 tangu uasisisiwe na Waasisi wake, Hayati Mzee Abeid Aman Karume na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mnamo Aprili 26, 1964.

Tunapenda kumkumbsha Maalim Seif na Chama cha ACT Wazalendo kuwa dhambi ya ubaguzi mnayotaka kuitekeleza haitawaacha salama watanzania kwani itaathiri maisha ya watanzania wa pande zote ambao kwa miaka yote wameishi na kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii mahali popote bila kubaguliwa wala kubughudhiwa.

Uimara na utulivu wa Muungano huu ambao ni mkongwe zaidi barani Afrika, umekuwa wa kutolewa mfano na kuzifanya nchi nyingi kuunda umoja ikiwemo Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Afrika Mashari na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kuzitajakwa uchache.

Ni rai yetu kwa Wazanzibari na watanzania kwa ujumla, kuwakataa viongozi wa aina ya Maalim Seif ambae hata hajaingia madarakni anaanza kuonesha wazi wazi kuwagawa watanzania. Tuchague kiongozi kutoka Chama kitakachowaunganisha watanzania na kuwapa uhuru wa kufanya shughuli zao mahali popote bila kubaguliwa wala kubughudhiwa kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.
Watanzania ni akina nani?
Najua kuna wa-Zanzibar na Wa-Tanganyika.
Sasa kama anagawa wa-Tanzania basi ni kwa faida ya waTanganyika na wa-Zanzibar.
 
Kuna point sana hapa tumalizane tu hakuna tabu wabaki na nchi yao zanzibar na sisi bara tuite Tanganyika na Wao Zanzibar.
1.Faida za Tanganyika ni nyingi na mlizifaidi ikiwemo Hifadhi za wanyama mlituondea sana kwenye utalii mno.kuna milima , waterfalls,mazao,umeme na pia biashara zenu zilikuwa zinaenda kwa sababu ya muungano huu eti bahari hata sisi ipo huko,mlifaidi hata maziwa yetu makuu mf. Lake Manyara,Lake Victoria na mengine.

Nendeni tu wala hamtutishiii
 
Katika Muungano kuna mipaka yake.Kwamfano majeshi ni sharti la Muungano, majeshi yana gharama kubwa.Zanzibar akiwa nje ya Muungano anaweza kupata ulinzi kutoka baadhi ya mataifa makubwa bila yeye kugharimia kitu,labda taifa kubwa wao kugharimia ustawishaji wa Zanzibar.
Ok, but katika nyanja za uzalishaji mf. Mwani kwasehemu kubwa hutakiwa kufanywa na private sector. Sijui kuna nini kwwnye fikra za wazanzibari kwenye maeneo haya, sijui kwanini anatafutwa wa kulaumiwa
 
Jamani Matajiri wa pemba na wengine wa ZNZ watawekeza kwenye soko gani , na hizi nyumba zao zilizoko huku bara itakuwaje??

Aaahh hilo si tatizo, kwani si wengine wameekeza hata nairobi na mombasa kenya, na maisha yanaendelea..............!
 
Mimi staki kumungunya maneno,tukivunja muungano kwa jazba,usishangae wakaja watu na visasi kuwa wazenj wote rudi kwenu.
Mimi nimeona General Idd Amin alivyowafukuza zaidi ya 70,000 wahindi Uganda.

Pia nimeona Kenya mara kunapokuwepo msuguano wa kisiasa kati ya Tanzania na Kenya,mara nyingi watanzania waliopo Kenya watakamatwa ,kupigwa na kuharibiwa mali zao.

Hii ni tabia yetu.
Nakuunga mkono, nadhani wabara walioko zanzibar itawabidi wapigembizi ili kujiokoa. Utaelewa ninachosema ukienda zanzibar ukasikia kinachonenwa juu wabara
 
The conduct of the upcoming elections in Tanzania has important consequences not only for Tanzania, but for the entire East African region. Tanzania’s history of peaceful multi-party elections stretching back 25 years has made it a model on the continent.

The United States government reaffirms unequivocally that it does not support any specific candidate or party in Tanzania’s upcoming elections. The United States supports the democratic process itself. We support a genuinely free, fair, transparent, and peaceful electoral process, before, during, and after election day. This includes ensuring the safety of all contestants, respect for the rule of law, and the absolute impartiality of the authorities in charge of managing the elections.

The United States, along with other democratic nations, will be paying close attention to actions of individuals who interfere in the democratic process or instigate violence against the civilian population before, during, or after the elections. We will not hesitate to consider consequences for those found to be responsible for election-related violence or undermining the democratic process.

We welcome the calls by the leading candidates for a peaceful and transparent electoral process, and we urge them and their supporters to take measures to decrease tensions and avoid inciteful rhetoric.

By U.S. Embassy Dar es Salaam | 1 October, 2020 | Topics: Press Releases
Hili la Ku undermine Democratic process Mahera ajiandae na jela.
 
Umeandika upuuzi, yule anayesema hapa sitaleta maji mkichagua tofauti na chama changu huyo ndiyo anahubiri umoja na kusema watatumia dola kubaki madarakani ndiyo umoja? shame on you
Achague watu wa kugoma na kumpinga nani anataka huo upuuzi. Hata Mbowe ukimbishia anakutolea dirishani, sembuse kumgomea. Ndio maana manyumbu wenu walikubali kumpa 1.5M, bila kubisha bisha. Chama saccos cha mbowe kimejiozea tu, majinga jinga ndio watawachagua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom