Mathayo Fungo
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 319
- 510
“Mimi sioni tabu kumwambia (Magufuli) tugawane mbao”. Haya ni maneno aliyoyatamka Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mkele, Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo ameitoa sambamba na kauli zingine nyingi ambazo zinaonesha dhamira ya dhati ya Maalim Seif Sharif Hamad kuvunja Muungano endapo tu atachaguliwa kuwa Rais katika Visiwa hivyo.
Ameendelea kusema hata kama Rais Magufuli atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi atamwambia Rais Magufuli abaki na Tanganyika na yeye (Maalim Seif) Zanzibar. Hii ni kauli inayoashiria wazi kuwa Mgombea huyu hana nia njema na Muungano ambao umedumu na kuenziwa na Marais wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar, kwa takribani miaka 56 tangu uasisisiwe na Waasisi wake, Hayati Mzee Abeid Aman Karume na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mnamo Aprili 26, 1964.
Tunapenda kumkumbsha Maalim Seif na Chama cha ACT Wazalendo kuwa dhambi ya ubaguzi mnayotaka kuitekeleza haitawaacha salama watanzania kwani itaathiri maisha ya watanzania wa pande zote ambao kwa miaka yote wameishi na kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii mahali popote bila kubaguliwa wala kubughudhiwa.
Uimara na utulivu wa Muungano huu ambao ni mkongwe zaidi barani Afrika, umekuwa wa kutolewa mfano na kuzifanya nchi nyingi kuunda umoja ikiwemo Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Afrika Mashari na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kuzitajakwa uchache.
Ni rai yetu kwa Wazanzibari na watanzania kwa ujumla, kuwakataa viongozi wa aina ya Maalim Seif ambae hata hajaingia madarakni anaanza kuonesha wazi wazi kuwagawa watanzania. Tuchague kiongozi kutoka Chama kitakachowaunganisha watanzania na kuwapa uhuru wa kufanya shughuli zao mahali popote bila kubaguliwa wala kubughudhiwa kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.