Maalim Seif ni tatizo CUF

Maalim Seif ni tatizo CUF

Mwacheni prof...aendelee na mambo yake.....
 
Lipumba alitaka tu yeye ndo agombee urais ndo baada ya UKAWA kuona mbali na kubana akazira. Hafikirii amegombea tangu vyama vingi vinaanza na hakubahatika kupata na akazidiwa na CHADEMA iliyoibuka hivi karibuni ikashika hadi nafasi ya pili. Anazingua et kumkaribisha Lowasa ndo tatizo ilhali yeye ndo alikuwa wa kwanza kumsafisha pindi kuna tetesi za kumkaribisha. Anatufanya kama wajinga anazan kujua na kutambua unafiki hadi tuwe maprofesa. We are grown up enough to be cheated.
 
C.V. unataka uone nini? Kwani anaomba kazi, huyu mwanasiasa. Kiongozi si lazima awe msomi mkubwa, chukua mfano wa Raisi aliyestaafu wa Brazil Lula De Silva hakuenda shule alizaliwa katika familia masikini amefanya kazi mpaka ya umachinga na shoeshine, mwishoe katika viwanda vya magari lakini tizama ameweza kuiinua kiuchumi nchi yake katika kipindi alichokua Raisi.
Mraisi na wafalme wa baadhi ya nchi za kiarabu hata shule hawajaenda, lakini tizama nchi zao, suala ni kiongozi anatakiwa muadilifu mwenye kufikiria maendeleo ya nchi na wanananchi wake na siyo yake binafsi na waliokua karibu yake.
 
Ndio amekuwa mtoaji wa maamuzi ndani ya Cuf kwa kuingilia madaraka ya mwenyekiti hili ndilo lililomuondoa Prof Lipumba katika uenyekiti, ameua cuf bara kwa maslahi Zanzibar, ruzuku ya chama yote kwa 80% imepelekwa zanzibar. Prof Lipumba alikuwa anataka kujua maslahi ya cuf ndani ya ukawa kuhusu ruzuku itokanayo na kura za urais. Lipumba ana Mengi moyoni hajayasema tuvute muda.

Ni tatizo kwa sababu amewachana kwamba ninyi ndio mmemrubuni lipumba kwa maprosoo?
Ni tatizo kwa sababu hanunuliki kirahisi?
 
Basalehe kagembeya udiwani?kutwa kin ukuu mpaka lini?gombeya us change na ushekhe 'naona a spends siyasa
 
Kuna jambo ambalo wafuasi wa Lipumba wanalifumbia macho. Hivi uzuri wa Lipumba ni upi ilihali tangu awe mwenyetiki CUF ina wabunge kidogo Bara?

Kwa ukweli CUF imemvumilia sana Lipumba na kumuacha hadi ajiuzulu mwenyewe. Alitakiwa afukuzwe siku nyingi. Nina shaka kama CUF walikuwa wanafanya tathmini ya ukuaji wa chama.

Kilichombeba Lipumba ni usomi wake ambao bila shaka ume tumika zaidi kuwa black mail CUF kuliko kuwasaidia.
 
OK kwa hio na SAADA MKUYA kuwa mgombea mwenza wa John Magufuli ni sawa na waislam wote wa CCM kuruhusu BIBLIA kuwa juu ya QURAN...heheheh
Yeyote anayejenga hoja kupitia udini, ukabila au Ukanda amefilisika kichwani
 
Kila siku anaimba ccm chali chali kifo cha mende. Mara ccm ndembe ndembe huku ana lake moyoni. Yeye mwenyewe ndio kafa kifo cha mende. Ha ha ha
 
CCM mkubali yaishe watu wameshafanya uamuzi tayari, hata UKAWA wakiweka fisi lazima itashinda uchaguzi. Tusaidieni kwa kutuondolea mapandikizi sisi huku field tuko ngangari kinoma.
 
Cuf ina nguvu kubwa Zanzibar bara ni kama imekufa sababu ya mwenyekiti asiye na vision. Haiwezekani kwa miaka 16 ya uenyekiti badala Cuf iinuke bara inazidi kudorora. Maalim lazima awe mkali haiwezekani yeye afanye kazi kwa bidii na kuinua CUf visiwani huku mwenyekiti amekaa na kutulia kama mwanamwali halafu anatanguliza ruzuku. Kwa kazi gani? Wabunge 2 bara? Aondoke aondoke mwana kwenda asiye na bidii wala juhudi.
 
Si mmoja tu yule wa lindi tu sidhani kama yuko mwingine
Hata mimi nawaza nguvu ya lipumba ni wapi maana hata kwao Tabora hana wabunge!
 
Back
Top Bottom