Mkuu,
Hivi Watz tutayumbishwa na vijimambo mpaka lini?? Issue hapa si Lipumba kuondoka CUF, issue ni kwa nini kama yeye ni mzalendo kweli aondoke kipindi hiki kigumu namna hii. Tulitakiwa tuondoe u-mimi kwanza tuuweke u-taifa letu mbele.
Angesubirisha speed yake kidogo kwanza, uchaguzi upite. Nia yetu ni moja tu; Tuing'oe ccm madarakani. Mengine kama nani awe nani, nani apewe ruzuku gani hayo ni baadaye.
Kama hili moja tu hakuliona, sidhani hata kama atakuja na sababu kuubwa kiasi gani tutamsikiliza tena. Kachelewa huyo, treni ya Safari ya Mabadiliko nje ya ccm ishapita hiyo
Aiseee nimekuelewa sana.
Tunahitaji watu wanaoandika vitu kea hoja kama wewe, sio porojoporojo
Kundi la wanachama wanaojiita kamati ya SAIDIA CUF ISIFE wamekutana jana vikao kwenye eneo la Mbagala Dar es salaam.Kupanga mikakati ya kumtimua Seif Sharif Hamad CUF.Walikuwa na wawakilishi kutoka bara na visiwani baadhi ya mambo wanayosimamia kutaka seif hammad aondoke ni haya
UPANDE WA BARA:
1.Kuionea CUF bara kwa sababu ya ruzuku.Hela nyingi za ruzuku zimekuwa zikienda Zanzibar kutumika kuimarisha CUF Zanzibar na bara wakinyimwa na kulaumiwa kuwa CUF haikui Tanzania bara wakati hawawezeshwi kifedha kama wenzao wa Zanzibar.
2.Kitendo Lipumba kufanyiwa fitna na Seif hadi kusababisha aachie ngazi CUF baada ya kuchoshwa na vitimbwi vya Seif
UPANDE WA ZANZIBAR:
1.Wanachama wenye misimamo mikali wa CUF Zanzibar wanasema wao na akina Seif na DUNI HAJI walikula yamini kuwa wao ni wazanzibar na lengo ni kuwa na Nchi ya Zanzibar na kuupiga vita muungano uliopo na kutokubali kuwa sehemu yake kwa namna yeyote ile.Kitendo cha DUNI haji kwenda kuwa mgombea mwenza katika muungano ambao hawautaki ni usaliti wa hali ya juu mno hivyo wanataka SEIF aondoke na usaliti wake
2.Wanachama wa kawaida wa CUF walikuwa wanamwona Duni ndiye ambaye ni tishio kwa Seif Sharif Hamad na ndiye ambaye anaonekana kuwa ana uwezo wa kuwa katibu mkuu wa CUF.Na seif alikuwa kila wakati anawaza hata kuongea kuwa Duni haji atamshughulikia siku moja.Na ulipokuja huo mwanya akaamua kumtosa kumtupa bara kwa CHADEMA ili aondoe tishio ndani ya CUF.Na mikakati yake imefanikiwa bila Duni haji kujua kuwa kategewa ili aondoke kwenye siasa za CUF ili SEIF Sharif Hamad aishi kwa raha ndani ya CUF.Wanachama wa kawaida wanataka Seif SHARIFF Hamad aondoke Duni wao arudi CUF haraka .
Ndio amekuwa mtoaji wa maamuzi ndani ya Cuf kwa kuingilia madaraka ya mwenyekiti hili ndilo lililomuondoa Prof Lipumba katika uenyekiti, ameua cuf bara kwa maslahi Zanzibar, ruzuku ya chama yote kwa 80% imepelekwa zanzibar.
Prof Lipumba alikuwa anataka kujua maslahi ya cuf ndani ya ukawa kuhusu ruzuku itokanayo na kura za urais. Lipumba ana Mengi moyoni hajayasema tuvute muda.
Tangu lini umeanza kuishi kwenye moyo wa Lipumba ?
Kama alivyo zito tatizo act chama cha waha
Wewe kabila gani!
Ujana majiyamotoMimi ni mtanzania
Ujana majiyamoto
Akili ndogo haingozi kubwa hill mlitambue,
kama lipumba amejiuzulu kwa sababu ya ruzuku basi hafai kuwa kiongozi na ni msaliti wa watanzaNIA wapenda mabadiliko ,kiterndo cha kujitoa katikati ya mchakatoni kusaliti ukawa,kwa sababu hizo sababu alizozitoa ni dhaifu na zingeweza kujadiliwa kwenye vikao usika,inaonyesha atakuwa amechukua mzigo ili kusaliti ukawa.
Daaah!! Magamba mnahaha sana aisee. Mtaongea kila aina ya utumbo ili eti msambaratishe UKAWA. Sasa kwataarifa yenu nihivi, ukawa inawatu makini, huyo msaliti mlompa hela mkidhani kuondoka kwake kutagawa watu kaondoka mwenyewe kama mlivomuona, hakufuatwa na hata mjusi wala hatakaa amege hata mtu mmoja kutoka Cuf wala ukawa. Ninachowaasa wana ukawa nikwamba kazeni buti, msiteteleke hata sekunde moja. Huo nimkakati wa ma Ccm wanaogopa huo moto wenu wakusimamisha mgombea mmoja ktk kilajimbo, wanajua hawatakaa watoke safari hii kwahiyo wanajaribu kununua watu wanadhani nimuhimu ndani ya Ukawa ili umoja huu udhoofike. Mnachopaswa kujua nikwamba bado wataendelea kurubuni wengi wenu humo, ila msikate tamaa. Wapo watu mtawapa majimbo kuwa wagombea, mwisho wasiku wataingia mitini kimizengwe ili wagombea wa Ccm wapite bila kupingwa. Ila sisi wananchi tunatambua kazi kubwa mnayofanya kwania yakujenga nchi, tunawasihi msikatishwe tamaa nahao wasaliti wachache. Kumbukeni msemo usemao {kwenye safari ya mamba kenge hawakosekani} Viva UKAWA.