Maalim Seif: Muungano lazima ujadiliwe

niko hapa zanzibar hakika harakati za wazanzibar serikali ya tz isijaribu kuzizuia maana iko siku zitalipuka kila nyumba niiangalia kama siyo mlangoni basi ni ukutani ina vipeperushi vinasema hivi..walipindua wazanzibar tujitawali, kudai uhuru wa zanzibar siyo dhambi,tunataka muungano wa mkataba...vipeperushi ni vingi zaidi ya nane na kilakimjakinaujumwake na nikisikiliza mazungumzo yao ni juu yamuungano hawautaki kbisa..nitavia-upload baadae
 
wadai inamaana gani kusema eti ukiwa nchini ni nchi mbili lakini ukitoka nje ni nchi moja, wanasema koti likikuchsha si una livua basi na wao muungano umewachosha..
 
[h=1]Koti la Muungano linatubana- Maalim Seif[/h]Posted on January 13, 2013 by zanzibariyetu


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad leo amekutana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kutoa maoni yake binafsi kuhusiana na mtazamo wake juu ya katiba mpya ya Tanzania ambapo amesema koti la Muungano linawabana wazanzibari kwa sasa wanahitaji kubadilishiwa jengine la kiasi chao.
“Koti la Muungano sasa linatubana sana, na kwamba tunahitaji kushona koti jipya kulingana na hali zetu za sasa”, alisema Maalim Seif mbele ya tume ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Maalim Seif ambaye amekuwa kiongozi wa Kwanza mashuhuri kukutana na tume hiyo katika utaratibu wa ukusanyaji wa maoni amesema katika kipindi cha miaka 49 ya Muungano bado hakujakuwa na nia njema ya kutatua kero za Muungano, hali inayopelekea kuongezeka kwa kero hizo na kuleta usumbufu kwa wananchi hasa wa Zanzibar.

Amesema kutokana na hali hiyo ni vyema muundo wa Muungano ukaangaliwa upya, na kusisitiza msimamo wake wa kuwepo Muungano wa Mkataba ambapo kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili ndani na nje ya nchi na baadae kushirikiana katika mambo ya msingi ambayo yataamuliwa na pande hizo mbili.
Maalim Seif ambaye ametoa maoni hayo nyumbani kwake Mbweni Zanzibar amefahamisha kuwa muundo wa

Muungano wa serikali mbili uliopo sasa hauwezi kutatua kero za Muungano baada ya kuwepo kwake kwa kipindi cha miaka 49 bila ya kuonyesha mafanikio ya kuridhisha ya kutatua kero hizo.
Amesema katika kipindi hicho tume na kamati kadhaa zimeundwa katika kushughulikia kero za Muungano, lakini mafanikio yake ni madogo, hali inayotia wasiwasi wa kuongezeka kwa kero hizo badala ya kutatuliwa.

Amefahamisha kuwa Zanzibar imekuwa muathirika mkubwa wa Muungano uliopo hasa katika Nyanja za kiuchumi na siasa, baada mshirika wake wa Muungano (Tanganyika) kutoweka, na kutumika jina la Tanzania kwa maslahi ya upande mmoja wa Muungano.

Maalim Seif anatarajiwa kukutana na waandishi wa habari hapo kesho katika hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar, ili kuyatolea ufafanuzi maoni hayo na kuyaweka bayana kwa wananchi wote maelezo yake aliyoyatoa katika tume ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Baada ya kuona 2015 inakaribia anatafuta umaarufu ili aendelee kushika ile nafasi yake ya kudumu ya kugombea urais
 
Mbona haiambii tume kuhusu nafasi za ajira katika balozi. Hiyo si kero ya muungano kulingana na Seif.
Koti likikubana unalivua, yeye anataka kubadilisha, ha!
Ndiyo maana napinga zamu za urais, kwa bahati mbaya huyu aweza kuwa rais wa muungano kama itakuwa zamu yao!
Mola tuepushe na balaa hilo yarabi!
 
Linawabana au linawapwaya? Watu wako milioni 1.3 wameungana na watu mil 43 hafu bado unasema umebanwa? Huoni kwamba umepwaya? Namhurumia maalim!
 
Mbona haiambii tume kuhusu nafasi za ajira katika balozi. Hiyo si kero ya muungano kulingana na Seif.
Koti likikubana unalivua, yeye anataka kubadilisha, ha!
Ndiyo maana napinga zamu za urais, kwa bahati mbaya huyu aweza kuwa rais wa muungano kama itakuwa zamu yao!
Mola tuepushe na balaa hilo yarabi!

Basi kama Urais utakuwa kwa zamu kati ya watu 1.3m dhidi ya 42m basi na bara tuweke Urais huwe kwa zamu kwa makabila. Hapo ndo itakuwa shughuli.
 
Maalimu Seif wewe kweli Kiboko.Ulianza na Sera ya Serikali TATU;Baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais na kuonja utamu wa Madaraka unahubiri Serikali MBILI;Ukinogewa sawaswa utakuja na hoja ya Serikali MOJA.
 
Mbona haiambii tume kuhusu nafasi za ajira katika balozi. Hiyo si kero ya muungano kulingana na Seif.
Koti likikubana unalivua, yeye anataka kubadilisha, ha!
Ndiyo maana napinga zamu za urais, kwa bahati mbaya huyu aweza kuwa rais wa muungano kama itakuwa zamu yao!
Mola tuepushe na balaa hilo yarabi!
Hivi hawa watu bado wapo tu?
Mie nilizani waliishajitenga tayari
 
Inaonekana koti mmelipenda sana mnaogopa kubaki na tsheti.. lingekuwa linabana kivile mngelivua siyo kusubiri mvuliwe..
Hivi bado wako tuu, mie nilizani waliishajitenga
Halafu nasikia na wangoni nao wamesema safari hii urais zamu yao na mkoa wa Rukwa unataka kujitenga
 
Bonyeza web chini

ZanziNews : Tumechoka mgombea Urais kuchaguliwa Dodoma - Vuai

[h=1]MAALIM SEIF: KOTI LA MUUNGANO LINATUBANA[/h]Written by Elbattawi // 13/01/2013 // Habari // 5 Comments


MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema koti la Muungano kwa sasa linawabana Wazanzibari. Na kuongeza: Kwa kipindi cha miaka 49 ya Muungano huo bado hakuna nia njema.
Maalim Seif ambaye ni kiongozi wa kwanza wa juu wa Serikali kukutana na Tume hiyo katika utaratibu wa kukusanya maoni, alisema hakuna nia njema katika kutatua kero za Muungano, hali inayopelekea usumbufu kwa wananchi hasa upande wa Zanzibar.
Maalim Seif alikutana na Tume hiyo leo nyumbani kwake Mbweni, Unguja amapo alisema Muungano wa Serikali mbili uliyopo sasa hauwezi kutatua kero zinazowakabili wananchi:
“Koti la Muungano linatubana sana na tunahitaji kushona koti jipya kulingana na hali zetu za sasa,” alisema Maalim Seif mbele ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba.
Alishauri kutokana na hali hiyo ni vyema muundo wa Muungano ukaangaliwa upya na kusisitiza msimamo wake wa kuwepo Muungano wa mkataba ambapo kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili:
“Tuna miaka 49 ya Muungano bila kuonyesha mafanikio ya kuridhisha ya kutatua kero za wananchi…sasa tunahitaji kushona koti, ili kila nchi iwe na mamlaka yake ya ndani na nje,” alisema Maalim Seif.
Alisema katika kipindi hicho Tume na Kamati kadhaa zimeundwa katika kushughulikia kero za Muungano, lakini mafanikio yake ni madogo, hali inayotia wasiwasi, kuongezeka kwa kero hizo badala ya kutatuliwa.
Maalim Seif alifahamisha, Zanzibar imekuwa muathirika mkubwa wa Muungano uliyopo, hasa katika nyanja za uchumi na siasa, baada mshirika wake ‘TANGANYIKA’ kutoweka, na kutumika jina la Tanzania kwa maslahi ya upande mmoja wa Muungano.
Maalim Seif ambaye pia ni katibu mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) kesho anatarajiwa kukutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar.
Aidha, Maalim Seif atatumia mkutano wake wa kesho, kuweza kufafanua maoni yake hayo na kuweka bayana kwa wananchi wote maelezo yake aliyoyatoa kwa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya..
 
Linawabana au linawapwaya? Watu wako milioni 1.3 wameungana na watu mil 43 hafu bado unasema umebanwa? Huoni kwamba umepwaya? Namhurumia maalim!
Tatizo mtu kua kiswahili si lugha ya kwanza
kubanwa nikikubwa ndio kinachobana kidogo au mingi kukielemea kichache ndio huko kubana.
kupwaya nikuover size yani yani kupata kikubwa kuliko mahitaji yako.
 
Na kama koti lakubana,si ulivue?nini wasubiri jingine ilhali hili linakubana sana?livue ati!
 
Hamna haja ya muungano kama hainufaishi pande zote nanunua gari zanzibar bsdo nalipa kodi maana ya muungano ni nini bado mpaka passport yakisafiria ndo niingie zanzbar wao wakija free what is that ?????!!!??
 
Na kama koti lakubana,si ulivue?nini wasubiri jingine ilhali hili linakubana sana?livue ati!
Ukibanwa na koti si busara kilivua na kusamehe kuvaa koti bali busara nikutafuta litalokufaa wakati hule ila ukikosa ndio unasamehe kuvaa koti
 
Hakika kama koti dogo kwa nini usilivue? Hawa watu wa zenji tabu tupu kila kukicha lawama ebu livueni hilo koti. Bara wanafaidika na nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom