Maalim Seif: Muungano lazima ujadiliwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif: Muungano lazima ujadiliwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Dec 4, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema hakuna mambo yaliyoainishwa kuwa ni matakatifu ambayo hayatakiwi kuguswa wakati wa kujadili Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano, hivyo aliwataka Wazanzibari wajiandae kutoa maoni yao juu ya Katiba wanayoitaka, ikiwamo mfumo wa Muungano wenye masilahi kwao.

  Alisema kutokana na Rais Jakaya Kikwete kutia saini muswada uliopitishwa na wabunge kuhusu katiba mpya, hatua inayofuata ni kuundwa tume ya kuratibu maoni ya wananchi juu ya katiba hiyo, na wananchi wanapaswa kujiandaa kutoa maoni bila woga, bali la muhimu ni kuhakikisha katika maoni yao hawatoi lugha chafu.

  Alisema tume hiyo itakayokuwa na wajumbe wanaotoka Zanzibar na Tanzania Bara, itatoa fursa ya kipekee kwa wananchi wa Tanzania, hivyo itakuwa nafasi ya kipekee kwa Wazanzibari kueleza nini wanataka, likiwamo suala la mfumo au muundo wa Muungano.

  “Nyinyi Wazanzibari na ndugu zetu wa Tanzania Bara ndio tuliovaa kiatu (Muungano) na aliyevaa kiatu ndiye anayejua msumari unachomea wapi, au anayelala kwenye kitanda ndiye anayejua kunguni wake,” alisema Maalim Seif.

  Hata hivyo, alisema kwamba litakuwa ni jambo la maana zaidi Wazanzibari wakiwa na msimamo mmoja juu ya mambo wanayotaka katika katiba mpya na waweke kando itikadi zao za kisiasa katika jambo hilo.

  Alieleza kwamba ni vema wakaendelea na na msimamo kama ule waliouonesha wakati wa kutoa maoni juu ya rasimu ya muswada wa katiba mpya ulioandaliwa mara ya kwanza, kabla ya kuwasilishwa bungeni, ambapo Wazanzibari kwa kauli moja waliupinga na ukarekebishwa.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Hofu yangu ni baadhi ya watu kuburuzwa kukidhi matakwa ya kundi linalotaka kauli moja! kanakwamba wanasomeshwa a e i o uuu!
   
 3. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  .....mpaka hapa tulipofikia, yaani kusainiwa kwa muswada na kuwa sheria, wazanzibari wameshinda, walikuwa wamoja, waliweka mambo walioyaona ni ya msingi kama taifa (zanzibar), tumebaki sisi huku Tanganyika, na akina sendeka wetu, akina rage wetu, (kwa uchache) ambao fikra zao ni posho tu na sio Tanzania ya kesho (mtazamo wangu, mm nawaona hivyo)
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Tanganyika tutakuwa wamoja siku mkuu wa nchi akiwa mzanzibar na pengine ndipo Tanganyika itazaliwa upya.

  That's nature.....

  Nje ya hapo tupate kiongozi ambaye hana masilahi ktk mfumo wa sasa
   
 5. s

  semundi Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hakuna umoja utakao endelea kama CCM hawatakubali kubadilisha sheria ambazo zimemlimit mwananch wa kawaida kuwa huru ktk mchakato mzima wa katiba mpya. na wasipokuwa makini lazima damu imwagige nchi hii.
   
 6. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanganyika kazi yao kugonga meza kama majuha,wako kichama zaidi maskini hawaelewi umuhimu wa katiba tunayotaka kutunga.......go maalim seif go ili wadanganyika wapate akiri waache ushabiki wa kipuuzi.......ili baadae wakizinduka tuzichape!!!!!
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hakuna mtu atakayetuzuia kuzungumzia Tanganyika yetu. Tutaizungumzia hata usiku wa manane wakati wao wamelala.
  Tunaidai Tanganyika na lazima itapatikana. Haiwezekani tuwe koloni la zanzibar. I say haiwezekani. Ni muda tu ngoja tuone.
   
 8. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Siyo muda mrefu Zanzibar itafunguwa minyororo ya mkoloni mweusi
   
 10. k

  king11 JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  maalim ni mwarabu hana sifa za kuamulia watanzania
   
 11. k

  kigu Senior Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wazanzibar wapo huru kujadili muungano, na kutoa maoni yao katika tume ya katiba mpya, na wao kama serekali (SUK) wanawaunga mkono.

  source ITV habari mudamfupi uliopita leo.
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja.
   
 13. s

  sanga malua JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ataweweseka sana mwaka huu. maoni watatoa lakini muungano hauvunjiki.
   
 14. B

  Bob G JF Bronze Member

  #14
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mwache ajimalize mwenyewe huyo mroho wa madaraka na muuaji wa Cuf bara na asiependa kuguswa
   
 15. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,314
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  ilivunjika soviet union itakuwa nyinyi ??? Tuko 2012
   
 16. K

  Kipimbwe JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kabla yakuvunjika muunano tujikumbushe terms of trade ya viazi vyetu,maharage na mtama wa maka(mpunga) toka Mbeya na Moro then ndo tuvunje nyie chezeeni supply chain tu mbaya zaidi mnamchezea actor kwenye chain.Kiukweli tende sio menu jamani
   
 17. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,314
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  kwani kabla ya huo muungano unafikiri watu wakila hayo maharage na viazi na ugali , hivi vinaliwa kwa sababu ya njaa tu ???

  Ugali watu hata walikuwa hawali , sembe wakila wafungwa
   
 18. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #18
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hiyo safi kabisa ndio wako huru hakuna wakuwabugudhi
   
 19. K

  Kipimbwe JF-Expert Member

  #19
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kwamwewe relax.Inaonekana umepanic.Jambo la msingi nikujadili nakueleweka sentensi yako haieleweki inyooshe ueleweke.Tunakuwekeni mjini then mnataka tuvunje muungano. Embu tuambie sasa kama mnakula kwasababu ya njaa si mtakufa tukiacha kuwalisha?Maana yake ni kwamba bei haitakuwa hii ya sasa mtakuwa mnaimport ambayo huku bara tunaongeza kitu tunaita trade balance kwenu?
   
 20. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yeye ni nani Tanzania hii? Ikiwa Shein ni Wazari yeye ni katibu wa kata? Eti wanajidanganya na ma vyeo hewa tu
   
Loading...