Yaani CAG anagundua makosa ya budget ya 2020-2021 halafu anaitoa 2022 lakini wakubwa wanaipeleka mbele katikati ya budget ya 2023-2024. Hivyo matatitizo ambayo yamegunduliwa yanaweza yakawa yanaendelea kwa miaka 2 kabla ya kufanyiwa kazi!. Lakini cha ajabu kama kweli Bunge kazi yake ni kushauri ni kwanini ushauri wa ripoti ya 2020-2021 usubiri mpaka mwisho wa mwaka 2023 kujadiliwa kama mawazo yao yana tija? Bunge linasema mawazo yao hayasikilizwi sasa yatasikilizwaje na serikali wakati ni miaka zaidi ya miwili tokea yatokee! na wakati mwingine serikali inakuwa imeanza kuyatafutia njia ya kuyatatua. Mfano CAG kagundua tatizo la maunuzi ya ndege je serikali kwa muda huu ambao bunge halijadili wala kutoa mawazo watawezaje kufanya maamuzi ambayo hayawezi kusibiri miaka! ukizingatia hii ni tender ya ujenzi? halafu baadae wanalaumu serikali haisikilizi. Kwani kikao cha Bunge kikiisha kuna ubaya gani kuongeza wiki mbili kujadili ripoti badala ya kupeleka mbele miezi 7!!!