Maajabu ya Rangi 3 za msingi

Maajabu ya Rangi 3 za msingi

Ray lee black is the absence of color. huo mchanganyiko huleta hali ya kushindwa kuakisi rangi ya aina yoyote ile kutoka kwenye mwanga mweupe. hivyo kinachotokea hapo ni giza a.k.a weusi.
nimekusoma mkuu
 
Hapa duniani inakadiriwa kwamba kuna rangi takribani milioni 6 mpaka 7 ambazo zinaweza kuonekana kwa kutumia macho bila msaada wa kifaa chochote kile!

Pia inafahamika kwamba rangi hizo zote zinatokana na mchanganyiko wa rangi tatu za msingi ambazo ni Nyekundu, Kijani, na Kibluu. Mfano rangi ya Chungwa, Udhurungwi, Zambarau n.k hupatikana kwa kuchanganya rangi hizo tatu kwa uwiano flani ili kupata matokeo tarajiwa.

Lakini vile vile mchanganyiko wa mwanga wa rangi tatu za msingi huleta mwanga wa rangi nyeupe, hivyo tunasema mwanga wa rangi nyeupe ni mchanganyiko wa rangi zote duniani, na consequently ukiutawanya mwanga mweupe utaziona rangi hizo zote.

Utaalam/ujuzi huu umekuwa muhimu sana katika ugunduzi wa taa za LED zenye mwanga mweupe na ambao huokoa umeme kwa asilimia 90%! Hapo awali iliwezekana kutengeneza 'light emitting diode' (LED) zenye kutoa mianga yenye rangi nyekundu na kijani, baada ya miaka mingi ya uhangaikaji iliwezekana kutengeneza 'LED' zenye kutoa mwanga wa bluu na hivyo muunganiko wa hizo tatu uliwezesha utengenezaji wa taa za LED nyeupe na kuleta mapinduzi katika teknolojia zenye kuokoa nguvu ya umeme!


Topic kama hizi ni nzuri sana kwani zina mafundisho kwa anaezipitia. Ahsante.

Kwa kuweka sawa kidogo na kuongezea utamu ili watu waelewe vyema kuhusu "primary colors":

Hizo rangi tatu ulizozitaja ni kwa ajili ya "display" za elektroniki au (umeme) kitaalam huitwa "additive combination of colors".

Lakini rangi tatu za "primary" za kuchorea au ku print au kufanya "dye" za nguo ni "magenta, yellow an cyan" na kitaalam huitwa "subtractive combination of colors".

Ni kuweka sawa tu ili ufahamu wa watu upanuke.
 
Inawezekana mi sio mtaalam kuliko ww,ninachofaham rangi za msingi ni red,blue,yellow...labda unieleweshezaidi

Soma post namba 24, nimejaribu kuelezea tofauti ya hilo. Mleta mada hajakosea na wewe pia hujakosea.
 
Rangi za msingi.....

Umenikumbusha somo la sanaa.....

Nilikuwa nachukiiiiiia kile kipindi
 
Topic kama hizi ni nzuri sana kwani zina mafundisho kwa anaezipita. Ahsante.

Kwa kuweka sawa kidogo na kuongezea utamu ili watu waelewe vyema kuhusu "primary colors":

Hizo rangi tatu ulizozitaka ni kwa ajili ya "display" za elektroniki au (umeme) kitaalam huitwa "additive combination of colors".

Lakini rangi tatu za "primary" za kuchorea au ku print au kufanya "dye" za nguo ni "magenta, yellow an cyan" na kitaalam huitwa "subtractive combination of colors".

Ni kuweka sawa tu ili ufahamu wa watu upanuke.
Ahsante kwa ufafanuzi murua kuhusu hilo swala la yellow..
 
Rangi za msingi ni rangi zisizopatikana kwa kuchanganya rangi zingine ila kutoka kwazo unaweza changanya na kuzalisha rangi yyte,ie nyekundu nyeusi njano buluu na nyeupe,
 
BujiBuji, weusi si rangi bali ni 'hali'. Infact hakuna kitu kama rangi nyeusi hapa duniani, kwanini nasema haya?!

Ili rangi iwe rangi inabidi iwe na uwezo wa kutoa mwanga wa rangi husika, mfano utakuta kuna taa zinazotoa mwanga wa bluu, 'orange', kijani n.k, lakini hatakuta taa inayota mwanga mweusi!

Weusi ni hali ya kushindwa ku-reflect/kuakisi rangi yoyote ile kati ya zile rangi milioni takrian 7 zilizopo kwenye mwanga mweupe, na badala yake huzinyonya rangi hizo zote na kuacha hali ya giza kwenye eneo husika, ambapo wewe umeamua kuita ni 'rangi nyeusi', lakini neno sahihi ni 'hali ya weusi'...!

Kitu cha bluu hunyonya rangi zote zilizo kwenye mwanga mweupe na kuakisi/ku-reflect rangi moja tu ambayo ni rangi ya bluu.., hali kadhalika kwa rangi zingine zote.., lakini vitu vyenye hali ya weusi havina uwezo huo!

Sio rangi, mwanga mweusi unapatikanaje!
 
Naona taa za LED kwa ajili ya majumbani sasa zimekuwa bei nafuu sana, hizi zinapunguza gharama za umeme kwa kiwango kikubwa mno, kwani inefficiency kupitia heat loss ni ndogo sana, LED oyeeee
 
Bila Shaka unamzungumzia moudy physics... Mchikichin hiyo aise pale tumepitia wengi
 
Back
Top Bottom