FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,617
- 46,713
Hapa duniani inakadiriwa kwamba kuna rangi takribani milioni 6 mpaka 7 ambazo zinaweza kuonekana kwa kutumia macho bila msaada wa kifaa chochote kile!
Pia inafahamika kwamba rangi hizo zote zinatokana na mchanganyiko wa rangi tatu za msingi ambazo ni Nyekundu, Kijani, na Kibluu. Mfano rangi ya Chungwa, Udhurungwi, Zambarau n.k hupatikana kwa kuchanganya rangi hizo tatu kwa uwiano flani ili kupata matokeo tarajiwa.
Lakini vile vile mchanganyiko wa mwanga wa rangi tatu za msingi huleta mwanga wa rangi nyeupe, hivyo tunasema mwanga wa rangi nyeupe ni mchanganyiko wa rangi zote duniani, na consequently ukiutawanya mwanga mweupe utaziona rangi hizo zote.
Utaalam/ujuzi huu umekuwa muhimu sana katika ugunduzi wa taa za LED zenye mwanga mweupe na ambao huokoa umeme kwa asilimia 90%! Hapo awali iliwezekana kutengeneza 'light emitting diode' (LED) zenye kutoa mianga yenye rangi nyekundu na kijani, baada ya miaka mingi ya uhangaikaji iliwezekana kutengeneza 'LED' zenye kutoa mwanga wa bluu na hivyo muunganiko wa hizo tatu uliwezesha utengenezaji wa taa za LED nyeupe na kuleta mapinduzi katika teknolojia zenye kuokoa nguvu ya umeme!