Ni kawaida sana mapaka hayo kujirarua hasa kipindi ambacho yanatafuta kuendelea kuwa mfalme wa mapaka .... nikimaanisha ni kawaida ccm kupitia tafran kipindi cha uchaguzi sio mara kwanzaSalaam!
Tukiwa wadogo, tulipenda sana kuwinda mapaka shume na kuyashambulia kwa mawe,
Yaani sie tulipoona mapaka tu jalalani, tulivizia, tukakusanya mawe yetu na kuanza kuyashambulia kwa ghafula, furaha yetu ilikuwa ni kuona mtaa wetu haui makao ya mapaka shume.
Sasa siku ya siku ikafika, tukiwa Katika harakati zetu za kuwinda mapaka shume, tukaliona paka shume moja jalalani, kama kawaida yetu Kila mmoja akakusanya mawe yake na kuchukua position yake kwa Siri kulizunguka jalala tayari kwa mashambulizi.
Tulipopeana ishara ya kushambulia, Kila mmoja akarusha jiwe kumuelekea paka, jiwe moja litatua kichwani mwa paka shume, jiwe hillo lilirushwa na rafiki YANGU mmoja alikuwa left handed,
Paka alipopigwa jiwe lile, aliruka juu na kurudi chini, sasa kwa kawaida yetu, tungejiandaa kurusha mawe awamu ya pili na tatu, jambo moja la ajabu lilitufanya tusite kidogo kuendelea kumshambulia paka shume.
Alianza kutoa milio ya ajabu, akaanza kujirarua mwenyewe ngozi yake na kujitoboa Hadi macho kwa makucha yake, anaruka juu na kujivuringisha kwa hasira muda wote alijikita Katika kujidhuru mwenyewe mwili wake, alikimbilia mahali na kujiviringa kwenye kamba na akafanikiwa kujitia kitanzi na kuning'inia,aliendelea kujidhuru bila kukoma!
Sie kuona hayo, tukaona mambo yamekorogeka, tukakimbilia mbali na mazingira Yale na kukaa na kuendelea kutizama tukio lile ambalo tulianza kumhurumia Tena paka yule.
Sasa kuna tabia Fulani zimeanza kuonyesha na chama Fulani ambazo naona zinafanana na kuchanganyikiwa kwa paka yule, tabia hizi zinaanza kutufanya kuacha kukishambulia na badala yake tunaanza kukihurumia.
Nawasilisha 🙏
Mambo ya utoto hayo,kwa hiyo unajiona mjanja na kujisifu kabisa kutesa na kuuwa mnyama asiweza hata kujitetea? hiyo ni psycopathy man, hauna tofauti na mnaowashutumu kuteka, kutesa na kuuwa watu hata wao wangetesa kupiga na kuuwa mnyama pia asiyeweza kujitetea bila ya hutuma yoyote ile …
Hii ya saaa inatisha zaidi,Ni kawaida sana mapaka hayo kujirarua hasa kipindi ambacho yanatafuta kuendelea kuwa mfalme wa mapaka .... nikimaanisha ni kawaida ccm kupitia tafran kipindi cha uchaguzi sio mara kwanza
Mambo ya utoto hayo,
Labda WEWE umeelewa kama yyai ndani ya uzio, hukuchanngamana na wenzio Katika makuzi
Ukiwa unatembea barabarani, kanyaga ardhi kwa makini maana kuna viumbe vingi mno unaviua visivyoweza kujitetea.na haujutii chochote? yaani haujisikii vibaya kupiga na kutesa mnyama mpaka kifo ambayo hana uwezo wa kujitetea ? …
Another hunter😃Umenikumbusha mbali sana
Yategemea umri wako tu .....kama gen z kidogo mengi yalikupita ila ccm hali mbaya zaidi ilikuwa 2015 ...na mwaka 1995 ila mwaka 2025 ccm haina tu strong candidateHii ya saaa inatisha zaidi,
Na ukumbuke pia ccm haikutajwa kwenye Uzi huu🙏
Naah shh 🤫Another hunter😃
Ccm haikutajwa humu,Yategemea umri wako tu .....kama gen z kidogo mengi yalikupita ila ccm hali mbaya zaidi ilikuwa 2015 ...na mwaka 1995 ila mwaka 2025 ccm haina tu strong candidate
Hata sasa huwa nashangaa,Kikos cha ukatili
Ila huku bongo paka akipita Jiwe
Kwa Wazungu nyau analelewa vizur hadi anapelekwa hospital
Chama hakijatajwa,Kwamba chama chetu pendwa ni PAKA LA MAPAKA?
kwa hiyo unajiona mjanja na kujisifu kabisa kutesa na kuuwa mnyama asiweza hata kujitetea? hiyo ni psycopathy man, hauna tofauti na mnaowashutumu kuteka, kutesa na kuuwa watu hata wao wangetesa kupiga na kuuwa mnyama pia asiyeweza kujitetea bila ya huruma yoyote ile.
kwa kifupi una check boxes zote za kuwa psycopath …