Maajabu kuhusu Kaburi la Abushiri

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,600
31,273
Hakuna kitu kinachomweka Mtafiti katika hali ngumu kama pale anapoelezwa miujiza katika utafiti wake.

Hapa anakuwa katatazika kwa sababu mafunzo yake hayajamtayarisha katika hilo.

Mtafiti yoyote anakuwa hana shida pale anapoangalia utafiti kwa jicho lake na kuona mabadiliko ya anachokitafiti.

Hapati shida kalamu inaandika kile kilichopo machoni pake na jicho la kamera halikadhalika litaweka picha hatua kwa hatua.

Hili haliwezekani katika muujiza.

Hili haliwezekani kwa sababu muujiza kwa kawaida unatokea mara moja na haujirudii wala si kitu ambacho kinaweza kupimwa na kutazamwa katika maabara au popote pale.

Nimepokea pongezi nyingi kuhusu niliyoandika na kuzungumza katika video kuhusu historia ya kaburi la Abushiri.

Nami huwaeleza wanaonipongeza kuwa mimi sijafanya lolote.

Kaburi la Abushiri limekuwapo kwa miaka 135 hadi hivi sasa na wenyeji wa Pangani wakilijua lilipo kizazi baada ya kizazi na kwa miaka hiyo ni sawasawa na vizazi vitatu au vinne hadi sasa.

Hawa waliopo hivi sasa Pangani walionipeleka mimi kuona alipozikwa Abushiri, hawa ni vilembwe.

Hawa ndiyo wanaostahili pongezi na kushukuriwa.

Si mimi mpuliza zumari au ukipenda Mpiga Filimbi wa Hamelin.

Naogopa kufanywa Mmishionari Johannes Rebmann ambae mwaka wa 1846 alipelekwa na Wakikuyu kuuona Mlima Kilimanjaro lakini waandishi wa historia wanamtaja yeye kama mvumbuzi wa mlima huo Rebmann akaikubali sifa hiyo.

Historia hii ikafanywa maarufu na kusomeshwa kwenye shule zote.

Abushiri amenyongwa Pangani na wakati ule hapo aliponyongewa palikuwa nje ya mji.

Waislam kama ilivyo ada wakaichukua maiti yake kwenda kuzika.

Lakini Abushiri hakuzikwa kwenye makaburi ya mji wa Pangani bila shaka Wajerumani hawakulitaka hilo kwani angezikwa kwenye makaburi wanayozikwa watu wa Pangani hofu yao ilikuwa Waislam na ndugu zake watakuwa wanakwenda kumzuru.

Hili hawakulitaka.

Walitaka Abushiri asahauliwe asiache kumbukumbu yoyote wala athari kwa vizazi vijavyo.

Bushiri akazikwa mbali na mji mahali pweke ambako hapana watu kwa nyakati zile.

Lakini bila shaka ndugu na jamaa zake walijua lilipo kaburi la Abushiri.

Kila miaka ilivyosogea mbele mji wa Pangani nao ukawa mipaka yake inatanuka hadi kulifikia kaburi la Abushiri na kulizingiira kwa ujenzi wa nyumba.

Leo kaburi la Abushiri liko Mtaa wa Uhindini mtaa uliopambika kwa nyumba nzuri zenye mjengo wa kizamani.

Kaburi la Abushiri limezungukwa na makazi ya watu.

Mtaa huu wa Uhindini wakiishi Wahindi tajiri wafanyabiashara na nyumba zao hadi leo ukiziangalia zinadhihirisha hali yao miaka hiyo.

Hawa ndiyo waliokuwa majirani wa kaburi la Abushiri kwa miaka mingi na hakuna shaka kuwa walilijua kaburi la Abushiri na ikawa ni simulizi ya kupashana habari kutoka kizazi hadi kizazi mpaka kutufikia sisi.

Safari kutoka karne ya 19 hadi leo karne ya 21.

Kwa miaka hiyo yote zaidi ya karne moja hapo hapakujengwa nyumba.

Imekuwaje pakaja kujengwa ni swali linalohitaji jibu.

Aliyejenga nyumba juu ya kaburi la Abushiri anasema yeye hakuwa anajua kama kiwanjani hapo kazikwa Abushiri hadi mmoja wa wazee wa Pangani jina lake Khalifa baada ya kuona ujenzi alimkabili na kumtahadharisha.

Tayari msingi wa nyumba ulikuwa umeshajengwa na mafundi wakamweleza wamekuta mawe ya ukuta lakini hawakujua kuwa hayo mawe ni kutoka ukuta wa kaburi.

Ujenzi wa nyumba ukaendela kupandisha kuta za jengo hadi kufikia kuweka linta wamalize kuta na kuanza kazi ya kupaua.

Hapa ndipo nimehadithiwa kuwa maajabu yakaanza kutokea katika ujenzi.

Mafundi wanafunga linta lakini wakifika asubuhi wanakuta pamebomolewa.

Watafunga linta upya na asubuhi kukicha wanakuta pamebomolewa tena mara nyingine.

Mwenye nyumba akaamua yeye na baba yake na ndugu wengine wakeshe usiku mmoja kulinda kuangalia nani atajitokeza kubomoa.

Palipoadhiniwa adhana ya kwanza sala ya Alfajir wakaona pamekucha na hali ni shwari wakaondoka kwenda msikitini kusali.

Waliporudi baada ya sala wakakuta pamebomolewa.

Taarrifa hizi zikafika hadi kwa masheikh kuwa katika ile sehemu alipozikwa Abushiri pana ujenzi wa nyumba na yametokea mambo kadha wa kadha.

Ushauri wa masheikh nimeelezwa ulikuwa pafanyike kisomo yaani dua na pachinjwe mnyama.

Nimeelezwa kuwa yule aliyeleta mbuzi kuchinjwa pale penye ujenzi alipigwa na watu wanaompiga hawaonekani.

Mpashaji wangu habari labda kuhofu kuwa ninataabika na kisa hiki akaniambia, ‘’Wote walioshiriki katika ujenzi wa nyumba iliyoko kwenye kaburi la Abushiri, mafundi na watu wengineo wako hai ukitaka naweza kukupeleka kwao uwasikilize wewe mwenyewe kwa masikio yako."

Nyuma ya mtaa wa pili kutoka Mtaa wa Uhindini ndipo lilipo kaburi la Abushiri.

PIA SOMA
- Historia ya Kaburi Abushiri bin Salim 1840 - 1889

1718722814001.png

1718722849752.png
1718722890654.png

1718722917061.png

Safi sana. kaburi lenyewe lipo wapi
 
we mzee bana, umenimalizia mb zangu bure tuu hujaonyesha kaburi lolote
Smith...
Si adabu kuniita wee mzee.

Ungeweza kusema, "Mzee ..." kisha ukasema uyatakayo.
Nyumba imejengwa juu ya kaburi la Abushiri.

Kaburi liko chini ya msingi wa nyumba.

Angalia ni watu wangapi wameingia kwenye YouTube Channel yangu kuangalia hii stori ya Abushiri.

Watu 6, 301 and counting.
Hakuna hata mmoja aliyetoa lugha chafu kwangu.

Kuwa na adabu.
Huo ndiyo uungwana.

1718827391947.jpeg
 
View attachment 3021028
Alikuwa muarabu?Al harith ni kabila la waarabu wa Oman
 
Mnaongoza sana kwenye falaki na uchawi hayo mambo ya dua na kuchinja sijui mbuzi ni uchawi na ushirika na majini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom