-Ni jiji pekee duniani ambalo mabomu ya serikali yamelipuka ovyo mara kadhaa na kuwauwa watu na kuharibu mali zao bila kufidiwa kihalali na wakati halali.
-Ni jiji pekee duniani wakazi wake wanafanya gwaride bila kupenda,asubuhi wanaelekea katikati ya mji na jioni wanarudi walikotoka.
-Ni jiji pekee ambapo nyumba zote za serikali zimeuzwa na watumishi wake wanaishi mahoteli ya kifahari.
-Ni jiji pekee ambapo wahindi wanang'ang'ania vijumba vya wanafunzi njini ingali wana uwezo wa kujenga za kwao.
-Ni jiji ambalo askari ni wengi lakini usalama ni mdogo sana
-Ni jiji pekee barabara zake zina matuta kila mahali eti watu wanagongwa sana
-Ni jiji pekee utakuta chupa zilizoisha maji zimetupwa barabarani zimejaa mikojo.
-Ni jiji pekee ukimgonga mtembea kwa miguu basi raia huchukua sheria mkononi kwa kukuua na kuchoma gari lako.
-Ni jiji pekee mwanamke akipata bwana anakuwa amepata muwekezaji, utakoma kwa kutoa pesa, voucher na kodi ya chumba.
-Ni jiji pekee watoto wengi hushuhudia wazazi wao wakifanya mapenzi kisingizio hapa mjini chumba ni kimoja.
-Ni jiji ambalo ukiwa baa mtu uliyekaa naye meza moja atakwambia yeye ni usalama wa taifa.
-Ni jiji pekee wauza mafuta ya magari wanaweza kugoma kuuza mafuta bila kuogopa serikali.
-Ni jiji pekee kuingia mahabusu bure lakini kutoka lazima uwe na hela.
endeleeni!!!!