- Ni jiji pekee ambalo mtu hujenga kwanza na kuomba kibali baadaye = Ujenzi holela
- Ni jiji Pekee ambalo halina building codes katika ya jiji (city center)
- NI jiji Pekee ambalo mtu hujenga jengo la hata orofa 18 bila kujenga maegesho ya magari
- Ni jiji pekee ambalo mtu akiwa na matofali ya kutosha na viezekeo basi hujenga ghorofa popote -cheki pale Kariakoo
- Ni jiji pekee ambalo 80% ya makazi yake ni holela (unplanned)
- Ni jiji pekee ambalo ukiwa unatoka katika ya mji umbali hata wa km 10 bado kuna foleni ya kutisha kutoka nje ya jiji kimara, mbezi, tegeta, mbagala)
- Ni jiji pekee ambalo 70% ya maeneo yake yananuka kinyesi
- Ni jiji ambalo huwa na mito mingi sana kwa muda mfupi wakati wa mvua (kutiririsha choo)
- Ni jiji pekee ambalo weekend huwa na foleni kubwa katika ya mji- miji mingi huwa hakuna foleni watu wanaenda mashambani/ picnic etc
- Ni jiji pekee ambalo lina nyumba nyingi za wageni kuliko idadi ya wageni wanaoingia jijini- Guest houses nyingi kuliko makanisa na misikiti
- Ni jiji pekee ambalo watu wake wengi hawajitambui na hawajui haki zao
- Ni jiji pekee Duniani ambalo 95% ya magari ya kuzoa taka yenyewe tu ni takataka
- NI jiji pekee ambalo mtu anaweza kuanzisha baa, ukumbi hata katikati ya makazi ya watu bila shida
- NI jiji Pekee ambalo mtu anaweza akaamua kufunga barabara na maisha yakaendelea tu
- Ni jiji pekee ambalo wakazi wake wengi hawajawahi kumiliki chombo cha moto zaidi ya pasi
- .....
- ......