Maajabu ya biashara ya uchimbaji wa madini ya dhahabu

Maajabu ya biashara ya uchimbaji wa madini ya dhahabu

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,638
Reaction score
3,641
Hi ni biashara pekee ambayo mtu au mchimbaji anaweza kukukopesa hata milioni 50 bila kuandikishana au kuwepo na shahidi yoyote.
20250323_134034.jpg


Ni biashara ambayo mtu anaweza kukuuzia udongo ambao hauna uhakika wa kilichomo ndani.
20250323_135516.jpg


Ni biashara ambayo pamoja na mtu anaweka pesa kubwa, ila wanaamini uchawi kwa asilimia 90

Biashara ya dhahabu ni biashara ambayo inaweza ikakufanya milionea kwa mwezi mmoja na ikachukua pesa zako zote ukawa maskini ndani ya miezi mitatu.

Ardhi ina siri nyingi sana na pesa ina siri nyingi sana.

Unaweza ukachimba shimo au duara ukaambulia udongo tu, ila mwenzako akachimba pembeni tu akapata utajiri.

Pamoja na pesa walizonazo wachimbaji wa dhahabu, hakuna mtu mwenye pesa za kuwekeza kwa kiwango kikubwa cha kutumia sayansi kama wazungu.


Dhahabu ambayo tayari imechimbwa ni kama asilimia 3 tu ya dhahabu ambayo haijaguswa Tanzania.

Nimefanya kazi kwenye uchimbaji miiaka nane hakuna kitu utanidanganya kwenye dhahabu.
 
Mengi uliyoandika hapo ni ya kweli.

Tatizo hawa wachimbaji wa kibongo akili ya kuwekeza baada ya kubongoa (kupiga pesa) hawana. Wengi akili yao iko porini tu kuwa ndio kwenye pesa za haraka.

Madogo wa Chunya wakipata vibunda vya dhahabu wanakimbilia kununua magari "crown" na kuona fahari kupark Chunya Pazuri au viwanja vingine vya starehe. Porini kukibuma anauza gari unamkuta anatia huruma

Wachimbaji wengi ambao baada kubongoa wakawekeza kwenye vyanzo vingine vya mapato maisha yao hayatetereki hata ikitokea wameporora kwenye madini

Hii biashara ni nzuri pia ukiwa mnunuaji wa madini kutoka kwa wachimbaji unakuwa hauko katika risk
 
Ulikua poli gani mimi nimepiga nyarubezi, mavota, kanegere, dutwa, mwakitolyo na nikaja nikamalizia mwime hakika nikijifunza mengi japo kwa mateso sana. Kule watu wanatenda dhambi hadi shetani mwenyewe anashangaa na kujifunza dhambi mpya ila all in all ukitaka uwe kwenye angalau safe side basi we kuwa broker au kota ununue dhahabu iliyotayali, bado machimbo nayadai ipo siku nitarejea
 
Kwenye level ya kumiliki mgodi yaan toka eneo mpaka wafanyakazi
Siyo rahisi kama unavodhani kijana kabla ya kuanza kuzalisha unao msuli wa kurun gharama za chakula na vifaa million kuiisha ndan ya masaa matano ni jambo la kauwaida sana kama kweli unataka kuwekeza huko jipe muda na uende maeneo matatu kujifunza nenda kahama,geita na chunya take time to learn otherwise you will perish
 
Hiyo Biashara wqnafanikiwa ni wale wenye waganga konki

Mtu akikukopesha kizembe ujue kachungulia kwanza kwa mganga wake

Akinunua mawe ujue kapereka kipande kwa mganga wake kachungulua kwanza hawa wwtu wao hawahitaji gold detector

Biashara yenye ushirikina wa kiwango cha SGR,
 
Siyo rahisi kama unavodhani kijana kabla ya kuanza kuzalisha unao msuli wa kurun gharama za chakula na vifaa million kuiisha ndan ya masaa matano ni jambo la kauwaida sana kama kweli unataka kuwekeza huko jipe muda na uende maeneo matatu kujifunza nenda kahama,geita na chunya take time to learn otherwise you will perish
Nipe ABC mkuu kuliko kunikatisha tamaa mpunga ninao wa kutosha ninachozungumzia hapa teknolojia kulipa wafanyakazi kwangu sio shida
 
Hio
Nakupata sana yani swala kuwekeza wataalamu mtu yupo bora kuwekeza waganga.
Acha nitunze maeneo yangu ambayo PPm bado inanipa matumaini mpaka nikamilishe vibari.
Hiyo ppm ni nn mkuu
 
Nipe ABC mkuu kuliko kunikatisha tamaa mpunga ninao wa kutosha ninachozungumzia hapa teknolojia kulipa wafanyakazi kwangu sio shida
Uchimbaji wa dhahabu una tofautiana kulingana maeneo kwa mfano gharama za kuchimba chunya ni tofauti na kahama kitu ambacho naweza kukushauli ni kuwa nenda field ukajionee na ujifunze, kuwa na hela siyo tatizo sisi baada ya kufanya uchimbaji bila technology tulipata hela ya kutosha tukaamua kutumia geologist ili tuwe na uhakika na tunachofanya ajabu hapo ndo tukafirisika kabsa so take time and make risk calculation before investing your money
 
Back
Top Bottom