Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) amefariki baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.
Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.
Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.
Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.
Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.
Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.
Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.
Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.
Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.
Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.
Source: Nyoka wa maajabu afa na mmiliki wake mkoani Songea | Bongo5.com
Sijui kwanani vijana tunakuta na tabia hizi, kule nyumbani kigoma nimeshuhudia kijana mdogo nae anamiliki joka kubwa tu. Mambo hizi zaman ilikuwa ni Kwa wazee tuKuna watu unaweza kuona wanatembea ukadhani ni watu kumbe sio watu ni majoka!
Hawa jamaa wachawi sana hovyo kabisa.songea ni jambo la kawaida
Hao mapolisi wanaongea tu bila kufanya uchunguzi wowote. Hawana ujuzi wa kujua mtu ameuliwa na nini kabla ya kufanya uchunguzi wa marehemu.
Kwanza siamini kabisa kwamba hii story ya kweli.
Samahani Sana mkuu.
Kwani nyoka ana "dudu" inayoweza kupenya kwa mwanamke?!!!!! looooh! bora nife maskini jamani, ushirikina hapanaKuna story moja huko kusini nasikia joka lilikuwa kila siku limfanyie mama wa mwenye duka vitendo vya udhalilishaji (siwezi kuandika hapa) ndipo baba anatakiwa nae apite. Kila siku wanauza kufuru.Hicho kibarua mama lazima akifanye kila siku ya MUNGU.
Wangekuwa na namba zako ungeweza kumuokoa marehemu mkuu.Iko hivi haya madude/madudu kuna watu huwa wanaishi nayo lakini kwa masharti
Wengine ni ya urithi
Wengine waliyapata kwenye ishu za kutafuta kinga dawa utajiri na kadhalika
Sharti mojawapo ni kwamba siku ukiona huwezi kulilea tena unalirudisha ulipolitoa au unapewa maelekezo ya kwenda kulitupa
Ukikiuka masharti likafa nawe unakufa, hicho ndio kilichomtokea Komba
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hao wananchi wenye hasira kali?Wangekuwa na namba zako ungeweza kumuokoa marehemu mkuu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji115]Rafiki yangu mmoja alimaliza ualimu, alipangiwa shule huko kwenye mipaka ya Msumbiji, tena shule yenyewe kijijini, ukisharipoti kwa mwalimu mkuu unafahamishwa kwa mwekiti na katimu wa kijiji.
Basi alinipa story kuwa kijijini waliona nyoka mkubwa anatembea, yeye alistuka sana, ile anataka kupiga kelele watu walisema aahh si nyoka wa Fulani yule, basi ananiambia Sky, yani kama kawaida yani kama kusema kuku wa Fulani au mbwa wa Fulani, alichoka. Alipigana mpaka alipata uhamisho.
Sijui nitumie lugha gani nipunguze makali (anaingia chimbo na ulimi)Kwani nyoka ana "dudu" inayoweza kupenya kwa mwanamke?!!!!! looooh! bora nife maskini jamani, ushirikina hapana
[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji13] [emoji13] [emoji12] [emoji12] [emoji115] [emoji23] [emoji23]Sijui nitumie lugha gani nipunguze makali (anaingia chimbo na ulimi)
unatumia akili kubwa kujibu vitu vidogo mwili kontena akili kisoda stupidUna simu kubwa sana hapo unayoweza itumia ku access ramani ya Tanzania au hukusoma Jiografia shule ya msingi?
Watakacho fanya nikukanusha uwepo wa uchawi kwakua njia zake haziko wazi.Nasubiri wana Sayansi wa JF walitolee Maelezo ki sayansi hili swala!
bado kaliSijui nitumie lugha gani nipunguze makali (anaingia chimbo na ulimi)
huyo alishang'atwa na nyoka sumu ikawa inamuingia taratibu.
Pumzika kwa amani huko uliko.
Amen.
mwili umeshafanyiwa autopsy au post-mortem ?
Na kama bado mmejuaje sababu ya kifo?
ha haHuyo muendesha boda boda amenichekesha sana. Eti aliona kitu kinamtekenya, kugeuka hivi, salalee akakutana na bichwa la nyoka! Akaruka akatupa piki piki hukoo! Weee chezea na dawa ya sumu ya nyoka kuuzwa laki saba na nusu!