MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

Watu wanauliza kwa nini asimuume kabla wakati alikuwa kamkumbatia? au nyoka alipata sumu ghafla?
Nyoka ana timing ya kumshika hawez kukudunga na kwa mujibu wa baba yake alikua ana tabia ya kudaka nyoka
 
Si nimesoma ktk habari leo kuwa nyoka alizikwa peke yake lakini ilibidi wamkate kichwa?
 
Nyoka ana timing ya kumshika hawez kukudunga na kwa mujibu wa baba yake alikua ana tabia ya kudaka nyoka
Kwa nini aseme mkimuua nyoka na mie nitakufa? endelea kutupa majibu Watanzania ni washirikina sana lakini linapokea tukio kama hili kila mtu anakana. Lazima baba mtu ajitetee si majirani wote walikua wanajua nyendo zao.Anafanya hivyo ili aishi kwa amani na kanisani inawezekana ndio mkusanya sadaka huku nyumbani wanamasnake.
 
Duuh jamani jamani watu wanafiwa na watu wa karibu ambao walikuwa ni kila kitu kwao baada ya hapo maisha yanaendelea ndo itakuwa nyoka? Ila hujatueleza huyo nyoka alikuwa anamsaidia nini..yaani ni kwa namna ipi nyoka anaweza kuwa msaada kwa binadamu hadi kuwa na mahaba ya hivyo baina yao
 
Wanasayansi wa bongo walioshindwa kutatua hata tatitizo la nzi wanaowashambulia wagogo na kuwafanya wawe vipofu unawataka kutolea ufafanuzi jambo gumu kiasi hiki watakuja kweli kwenye uzi huu unadhani?
 
Japo Sayansi haiamini Uchawi ila Sayansi yenyewe ni Uchawi wa hali ya juu, sawa na mbweha na mbwamwitu tu.
Uchawi wa sayansi ni upi mkuu??........kutengeneza sufuria ni uchawi?kutengeza nguo ni uchawi??kutengeneza karatasi ni uchawi???kutengeneza mbege ni uchawi???kutengeza kijiko ni uchawi???kutengeneza sabuni ni uchawi???kutengeneza juice ni uchawi???kusaga unga ni uchawi???(kumbuka hayo yote ni sayansi)
 
Kwa asili Wangoni sio wazawa,, hivyo kwa sisi Wa Tanzania si rahisi kujua haya madudu yao ya Afrika kuzini.
 
Kwa lugha rahisi sana huyu mmiliki wa nyoka ndg Komba (26) mkazi wa Songea alikuwa na MAHABA. Yawezekana alikuwa anamtegemea sana ktk maisha yake.

Hivyo huyu nyoka alikuwa sehemu ya akili na mwili wa ndg Komba.

Hivyo kitaalamu kilicho muua Komba ni tele-empathy (telempathy), kwa kiswahili ni midadi. Midadi huja pale ambapo mtu amebeda hisia kali juu ya kitu/mtu. Komba alikuwa anamhurumia nyoka wake kiasi kwamba alikuwa anayabeba maumivu ya kipigo cha nyoka.

Nyoka wake alipokufa, Komba akawa amepatwa na maumivu ya kihisia kwa kiasi kikubwa na kupelekea kinga yake kushuka mno.

Pia ktk mwili wake palitokea reactions ambazo ni negative kwa afya na uhai wake ndiyo maana akaanza kutokwa mapovu na hatimaye kifo chake. Kuna Uhusiano Mkubwa Sana Kati Ya Hisia Na Uhai.
Midadi ndio sababu kuu
 
Back
Top Bottom