MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

MAAJABU: Nyoka afa na mmiliki wake Songea

eti nyara za serikali hapana hapo sijaona nyara yao kumbe ndio anashikilia roo ya kijana mdogo ivo
 
Nyoka John maghembe atueleze alivyohamishiwa kwa huyo jamaa na document zake zote za kuonesha uhalali wa kumilikiwa na huyo marehemu.
 
Uongo huo! Msom
Kwa macho na masikio yango niliona na kusikia tukio hilo likiendelea.Nyoka huyo alipigwa na mwenye nyoka alisihii sana asipigwe na baada ya nyoka huyo kufa jamaa alizitokwa na povu mdomo na kufa.lakini cha ajabu zaidi ilipofika mida ya saa kumi na moja jioni kaka wa marehemu alikuja kumtafuta njoka yule na kuuliza kama amekatwa kichwa,alipoambiwa hajakatea kichwa aliomba aonyeshwe huyo nyoka na ndio alipoonyeshwa then akasema kwao wamekataa kuweka msiba kwa sababu wanaamini ndugu yao hajafa na ndipo ndugu yule alipotoa kiroba kidogo dogo na kumchukua nyoka yule then akapanda pikipiki nakuondoka nae...Chaajabu zaidi ilipofika asubuhi inasemekana maiti ya kijana yule iliyolazwa monchwali ya Haspitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo songea(Homso)ilipotea na kutoweka monchwali hapo na hakuna anaejua wapi ilipo maiti hiyo.

C& P[/QUOT

Mkuu huo ni uongo Wa kutupwa kabisa. Maiti itoweke Mochwari kivipi? Hilo la kutoweka maiti umelishuhudia au umesimuliwa?
 
Watanzania ni vizuri kuheshimu imani za watu kwa mujibu wa katiba ya 1977, jeshi la polisi kamateni hao waliongilia uhuru wa mtu wa kuabudu.
Wananchi waliua nyoka ambaye kuuawa kwakw hakuna shida yeyote huyo aliye kufa mwenyewe ana anamapungufu yake kiafyasababu hiyo ni kwa mujibu wa sheria
 
Actually Kuna njia ya kiyasansi yakuelezea hicho kifo nadhani inaitwa mental suicide kutokana na imani yake maelezo ya mganga kwamba nyoka akifa nae anakufa imani Ni kitu kikubwa na cha ajabu Sana
 
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) amefariki baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.
Nadhani ifike kipindi sasa tuelewe kwamba humi
Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.

Source: Nyoka wa maajabu afa na mmiliki wake mkoani Songea | Bongo5.com
Tuelewe tu kwamba kuna existence ya dunia ya kiroho.. Ile ambayo si ya kimwili au kwa akili zetu za kawaida. There are two worlds ambazo tunaishi nazo.. Huu ulimwengu tunaouona na kujumuika nao kiuhalisia.. Lakini kuna ulimwengu wa kiroho ambao ndio upo in background unaodictacte haya yote tunayoshuhudia na kuyaishi tukiyaappreciate physically. Aliyesema suala la kuunganisha nafsi kati yake na nafsi nyingne kiroho... Hii ndo ushahidi. Ipo. Ni sayansi ambayo wazungu walibidi waiterm "science beyond Britannica". Ni masuala yanayotokea na yanatokea kiuhalisia baada ya nguvu fulani kufanya kazi yake lakini kuelezea kisayansi hapo ndipo changamoto inapokuja. Haiwezekani kuelezea kisayansi masuala ya kiroho but they happen for real!!!. Ni suala la kawaida watu kutumia nguvu za giza (in spiritual realm) kuwezesha mambo yatokee itakivyo kiuhalisia (physically). Roho zinazofanya hayo hutumia viungo.. Au miili hii hii ya wanyama au viumbe vyovyote vile ili kufullfil the intended purpose. Lazima vitu vilivyopo physically vitumike ili mambo ya kiroho yajidhihirishe kiuhalisia. Hivyo basi msishangae nyoka tu kutumika kwenye hili lakini nawaambieni hata hao Mende na Inzi mnaowaua kila siku majumbani mwenu ni watumishi wakubwa sana kutekeleza shughuli za kiroho giza majumbani mwenu.
 
Makanisa na misikiti itumike kikamilifu kuwahubiria waumini wake na pia kukemea kuachana na Imani za kichawi na kishirikina kwani imani hizo zinaangamiza, zinakufanya uwe mtumwa wa kiakili, pia ni kikwazo cha maendeleo ya wananchi kwa ujumla wake.
Mkuu hii kitu ni very personal, makanisani humo wengine wanakwenda na hiziri kwanye handbag.
 
NYoka JOHN ni nyara ya serikali. Hawa waliomwuuwa serikali imewachuliaje.
 
Yaan watu wengine bhana unatembea Na nyoka mfukoni kweli ona sasa.
 
Back
Top Bottom