Maajabu: Furaha ya CCM ni kwa Nyalandu kuondoka CHADEMA na si kujiunga na CCM?

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,860
Mabibi na mabwana kumekuwa na shamra shamra nyingi hasa kutokea kwa wale makada nguli wa chama mboga mboga kuwa bwana Nyalandu katoka Chadema.

Ajabu ni kuwa furaha zimeelekezwa kwenye kuwa bwana huyu asiyekuwa na jina ndani ya Chadema, ametoka Chadema wala si kuwa kajiunga na CCM!

Maajabu zaidi ya Mussa ni kuwa, kwa Chadema: "kuondoka kwake ni mithili ya kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu mno, kwa mchukuzi."

Wajameni, kwanini CCM wanashangilia hivi kuwa huyu bwana katoka Chadema? Kwanini CCM hawashangilii kuwa kwa kajiunga nao? Kwamba labda sasa wamepata jembe mahiri la kulimia kweri kweri?

Kwamba, kuwa promo zote anazopewa huyu bwana, ni kuwa katoka Chadema na si kuwa kajiunga na CCM?!

Hiiiiii bagosha, pana nini hapa?

Au huyu bwana ana siri gani nzito ambazo CCM walikuwa zimewakosesha kabisa usingizi kila walipokumbuka kuwa huyu bwana yuko huko? Kwamba sasa ni heri mno katoka huko, na kuwa angalau sasa watapumua kwa nafasi waliniambia na kujimwaya mwaya?

Aliwabana nini CCM Nyalandu kuwa Chadema? Mbona hatuoni shamra shamra za kuwa huyu bwana sasa atawafaa na nini huko CCM?

Au labda tuseme ni yale mambo ya kumpongeza tu, kwa kuwa alishindwa kabisa kuziimba zile nyimbo zake za Sayuni alizozizowea alipokuwa huko?

Wajameni, furaha na shamra shamra hizi, sababu zake tafadhali.

Ninawasilisha
 
Chadema inatakiwa kukimbiwa na kila mwenye akili.
Hivyo ukiona watu wanafurahi nyalandu kuondoka jua kuwa wanafurahi chadema kukimbiwa
 
Kama CDM watampokea yeyote toka CCM kwa mbwembwe, basi kitakua sio chama cha siasa bali ni kikundi cha kisanii.
 
Nilikuwa namuona PM Majaliwa akimwangalia Nyalandu kwa kebehi jana wakati anasoma lile gazeti lake. Body language yake ilikuwa ni kama anasema umerudi kufuata vyeo maana Magu kafariki.
Kwani Nyalandu alipoondoka CCM hakuwa na cheo?
 
Chadema inatakiwa kukimbiwa na kila mwenye akili.
Hivyo ukiona watu wanafurahi nyalandu kuondoka jua kuwa wanafurahi chadema kukimbiwa

Kama wenye akili ni aina ya Nyalandu wakimbie tu. Kitendo cha cdm kuendelea kukubalika na wananchi ni jinamizi kubwa sana kwa ccm, mpaka wanaccm wasio na impact yoyote ndani ya cdm wanaporudi ccm eti wanafurahi! Wamerudi akina Lowassa, Sumaye nk Lakini ccm bado imezidi kutegemea vyombo vya dola kutangazwa washindi. Inabidi uwe mwendawazimu kuona Nyalandu kurudi ccm ni pigo kwa Cdm.
 
Kila lakheli katika safari ya ubalozi, umezichanga karata vyema, utazeeka vizuri
 
Kama wenye akili ni aina ya Nyalandu wakimbie tu. Kitendo cha cdm kuendelea kukubalika na wananchi ni jinamizi kubwa sana kwa ccm, mpaka wanaccm wasio na impact yoyote ndani ya cdm wanaporudi ccm eti wanafurahi! Wamerudi akina Lowassa, Sumaye nk Lakini ccm bado imezidi kutegemea vyombo vya dola kutangazwa washindi. Inabidi uwe mwendawazimu kuona Nyalandu kurudi ccm ni pigo kwa Cdm.
Kama chadema ina mwamini mtu asie na akili kama Nyarandu basi hicho chama ni cha hovyo!
 
Jana Jk alikuwa na Furaha sana baada ya Waziri wake wa Mwisho wa Maliasili na Utalii kurejea Chamani, kashindwa kujizuia hadi wamekumbatiana!
 
Kwanini mtu uumie hivi hadi uanzishe mada kabisa ya mtu kuhama chama ulicho wewe?

Hii ni kutotambua kuwa mtu anaingia kwenye siasa mainly kwa ajili ya nafsi yake either kwa ajili ya kipato, power au umaarufu na sio kwa ajili ya kukuburudisha wewe na nafsi yako. Ukijua hilo utaacha kukimbiza na wanasiasa kuapizana...oh wasalitii.
 
Mpiga dili karudi kwenye chama cha wapiga dili, halafu kuna misukule wanashangilia tu wao wamesharidhika kuwa wanawashangilia wenzao wakija kupewa vyeo wao wapo tu.
Mbona wakati anahamia huko chadema mlishangilia na mkampa na cheo kabisa Cha mwenyekiti Kanda ya Kati na mjumbe wa kamati kuu? Kwa nini hawajakupa wewe mwenyeji?
 
Walivyosalitiwa na John Magale Shibuda Mbowe aliahidi kutopokea Mtu yoyote toka CCM na kumpa fursa ya kugombea

Mroho hana Kiapo,…Lowassa alipokuja na 'umate mate' akapokelewa
Kama CDM watampokea yeyote toka CCM kwa mbwembwe, basi kitakua sio chama cha siasa bali ni kikundi cha kisanii.
 
Kama wenye akili ni aina ya Nyalandu wakimbie tu. Kitendo cha cdm kuendelea kukubalika na wananchi ni jinamizi kubwa sana kwa ccm, mpaka wanaccm wasio na impact yoyote ndani ya cdm wanaporudi ccm eti wanafurahi! Wamerudi akina Lowassa, Sumaye nk Lakini ccm bado imezidi kutegemea vyombo vya dola kutangazwa washindi. Inabidi uwe mwendawazimu kuona Nyalandu kurudi ccm ni pigo kwa Cdm.
Mnarudia uchaguzi wa Kanda ya Kati?
 
Nyalandu hakuwa na uzito wowote ndani ya Chadema na ndiyo maana aliondoka,na Nyalandu amerudi CCM kwa sababu yule dhalim hayupo tena CCM.
Hakua na uzito? Mbona mlimpa uenyekiti Kanda ya Kati na ujumbe wa kamati kuu?
Unataka kusema ujumbe wa kamati kuu hauna uzito?
 
Kama chadema ina mwamini mtu asie na akili kama Nyarandu basi hicho chama ni cha hovyo!

Wala hata haiendani na nilichokisema, aliyesema mwenye akili ni yule niliyemquote. Pitia alichokisema kisha iingize utashi wako kwenye maoni yangu.
 
Back
Top Bottom