Maafisa Utumishi wagoma kuruhusu Mabenki kutoa mikopo ya watumishi. Yawezekana ni hujuma?

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Wiki jana nimeingia benki moja Mikoa Fulani nikakuta watumishi wamejikusanya kwa majonzi. Baadhi yao niliwafahamu Na nilipowadodosa wakadai mikopo yao kukwamishwa na maafisa utumishi.

Walidai kupewa majibu hayo na maafisa wa benki. Kuwa maafisa utumishi wamegoma kuingiza makato kwenye mfumo wa mishahara ambapo ndiyo taratibu ili mikopo itolewe kwa walengwa.

Wengi walionekana kuhuzunishwa na Jambo hilo .\

Nikajiuliza, ni nini kimesababisha maafisa utumishi hao kutotoa majibu ya uhakika au wahusika kurekebisha mfumo ili wahitaji wa mikopo waweze kupata stahiki zao.

Ni majuzi tuu tuishuhudia mfumo wa Lulu au ulipaji umeme ukihujumiwa na kuzua keep kwa watumiaji umeme nchi nzima. Ambapo Baada ya Waziri Mkuu kuingilia kati, na massa machache baadae tatizo likaisha.

Je, hapa Nako kuna umuhimu wa Wa Waziri Mkuu kuingilia kati ili Watumishi hawa wapate stahiki zao?
 
🤣 🤣 🤣 kila njia kwenye awamu hii inaweza kuwa sahihi mkuu,usishangae mtu mwenye master's ni dereva-wengine huficha baadhi ya vyeti ili wafanikiwe kujikwamua
Hakuna kitu kama hicho hata kama umeingia kama dereva wanakufanyia recategorization fasta maana upungufu ni mkubwa sn
 
Back
Top Bottom