Mchaga Tajiri
Member
- Mar 14, 2023
- 10
- 16
Kuna tabia ambayo imeshika kasi kwa baadhi ya maafisa habari binafsi na hata wa Serikali.
Wanapoandaa matukio yao mara nyingi huwa wanavyombo vya habari ambavyo wamevialika, anapofika Mwandishi wa Habari ambaye hayuko kwenye orodha yao wengine huzuiwa kuchukua matukio Kwa kigezo kwamba hawako kwenye bajeti ambayo wameiandaa.
Au wakati mwingine anapofika mwandishi wa habari anaulizwa wewe ni wa chombo gani? Anapotaja chombo chake anaambiwa kwamba wewe sijakualika ni nani aliyekupa taarifa?
Hali hii sasa imesababisha hata Waandishi wa Habari wenyewe kwa wenyewe kushindwa kupeana taarifa zinazotokea kwenye maeneo yao kwa kuhofia kuulizwa na wadau wao waliowaalika kwa nini wameongeza watu wengine ambao hawako kwenye orodha.
Pamoja na yote wakati mwingine wapo baadhi ya waandishi ambao hata wakipewa nafasi ya kuchukua matukio na wanajua fika hawako kwenye orodha ya malipo wamekuwa ving'ang'anizi kuwasumbua wadau kuwapatia pesa kilazima akijua fika hayuko kwenye orodha.