Wizara ya Nishati yatuhumiwa kumwaga rushwa kwa wabunge na waandishi wa habari. Takukuru ingilieni

Samson Kwayu

Member
Jun 9, 2022
18
90
Kwa mara ya kwanza katika siasa za Tanzania na kwenye bunge la bajeti tunashuhudia jinsi wizara ya nishati inavyonunua waandishi wa habari na wabunge katika jitihada za kuhakikisha bajeti yao inapitishwa bika mikwamo.

Ni utamaduni mpya sana wa kiutendaji na kwa kweli haijapata kutokea kama taifa tukafika kiwango cha waziri kama January Makamba kutoa mamilioni ya fedha kama rushwa kwa wabunge ili tu bajeti ya wizara yake isikwame. Anakodisha coaster nzima imejaa waandishi kwenda bungeni Dodoma kwa ajili ya kuandika na kufanya propaganda za bajeti yake wakati waandishi hawa hawa walizibwa mdomo wakati wa madudu yake kwenye ripoti ya CAG.

Tuna taarifa za uhakika wiki mbili nyuma Mbunge Deo Mwanyika akifanya kikao na waziri huyu jijini Dar Es Salaam hoteki ya Serena na kukabidhiwa zaidi ya 700m TZS kwa ajili ya kuwatukiza wabunge wanaowaita wana viherehere kutosumbua wakati wa kusomwa kwa bajeti ya wizara ya nishati. Jambo hili tulikisema wazi lakini vyombo husika vinamuogopa huyu bwana na hawajathubutu hata kumuuliza tu Deo Mwanyika anagawa pesa kwa wabunge kwa ajili ya kazi gani.

Kwa nini wizara hii imekuwa na matukio ya rushwa hivi? Wanatoa wapi fedha za kufanya haya mambo? Majibu ya hili ni mepesi na CAG ametusaidia kusema waziri January anatoa wapi pesa za kufanya matukio haya.

Tanesco imekuwa na hadithi kila siku za kusaini mikataba ya kuzalisha umeme lakini bado nchi iko gizani na mgao upo kimya kimya. Miradi hii ni kiini macho na ni sehemu ya upigaji hela kwa sababu haina tija na haina tofauti na RICHMOND na ESCROW.

Jana tumeona mkurugenzi wa tanesco bwana Maharage anasaini mkataba badala ya katibu mkuu wa wizara! Haya ni maajabu yaliyopitiliza na watu hawa wawili wanaifanya hii wizara wanavyotaka huku wakitazamwa tu.

Kutoka bungeni tuanambiwa siku 2 kabla ya kusomwa bajeti ya wizara ya nishati wabunge wote mbali na kuhongwa pesa wamepewa coupon za kuchukua majiko ya gesi 100 kila mmoja kupelekea wananchi.

Hivi kuna rushwa zaidi ya hii? Wabunge 320 wote wamepewa mitungi ya gesi akiwemo Msukuma,Mdee na Tabasamu ili tu waingiwe ganzi kwenye kushughulika na hii wizara wakati wa kusomwa bajeti. Hivi wabunge mmesahau madudu ya January Makamba kama waziri kwenye ripoti ya CAG? Mmesahau wizi unaofanywa tanesco? Mmesahau vyura wanavyolipiwa mamilioni hila utaratibu?

Kwa hali ilivyo watanzania mnatakiwa kuanza kukabidhi haya mambo kwa Mungu ndiye pekee atayayeingilia kati lakini mkitegemea bunge hili hakuna kitu watawafanya hawa watu kwa kuwa wao ni sehemu ya huu uchafu.
 
Kitendo cha wabunge kukubali rushwa ya mitungi ya gesi 100 kila mbunge na spika anatetea eti wao ni wawakilishi wa wananchi kimesababisha nimewadharau sana.

Spika anatetea eti ni kawaida, kama ni kawaida mbona wizara ya kilimo haitoi mufuko 100 ya mbolea ya ruzuku kwa kila mbunge akagawe jimboni?

Mbona wizara ya ujenzi hawagawi mifuko ya saruji 100 kwa kila mbunge akagawie wananchi.

Hii nchi kama watu wanategemea wapiga dili kama Februari watuletee maendeleo basi tumechelewa sana.
 
Back
Top Bottom