Maafa makubwa Gymkhana Club

Maafa makubwa Gymkhana Club

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
4,974
Reaction score
793
Wachezaji wa golf waliokuwa wakicheza katika viwanja vya Dar es Salaam Gymkhana Club leo jioni, wamekumbwa na maafa makubwa baada ya mvua kubwa kuanza kunyesha zikiambatana na upepo mkali.

Wachezaji hao ambao wengi wao ni wahadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, walijificha ndani ya mojawapo ya vibanda vilivyopo uwanjani hapo. Upepo mkali uliokuwa ukivuma uliangusha mti mkubwa uliokuwa kando ya kibanda hicho na kuwaangukia wachezaji hao.

Baadhi walijitahidi na kujinasua kutoka ndani ya kibanda hicho, lakini mtu moja ambaye ametambuliwa kama Prof. Kamuzora, aliangukiwa na gogo kubwa la mti huo na kuchukuwa muda mrefu kuweza kumuondoa chini ya hilo gogo, kwa ushirikiano wa polisi wa kituo kidogo cha mtaa wa Shaban Robert, wafanyakazi wa club na wachezaji.

Baada ya kuondolewa Prof. Kamuzora alikuwa ameumia vibaya sana kichwani na uso umeharibika vibaya. Taarifa tulizopata baada ya kufikishwa hospitali zimedhibitisha kuwa Prof. Kamuzora amefariki dunia.

Picha ya marehemu akiwa anacheza Golf katika viwanja vya Gymkhana.
 
Nami nipo jirani ya eneo hili na taarifa hizo ni KWELI KABISA.
 
Sad news.

Mimi mwenyewe nipewe taarifa kuwa paa la kibanda changu limechukuliwa na upepo. Lakini hakuna maafa.

Hiki ni kimbunga.
 
he he he hii balaa tea, pole sana kwa familia. kweli upepo ulikuwa mkali sana mpaka ukakata umeme. nafikiri watu wengi waliokuwa barabarani wanaweza kuwa wameumia ngoja tuangalie taarifa ya habari leo
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!

Sina uhakika kama idara yetu ya hali ya hewa ilitoa tahadhari ya ujio wa kimbunga hiki kwa watu vya kutosha au ndo kama kawaida tunajiendea tu!!!
 
dah,prof kamuzora mungu amrehemu,ntamkumbuka kwa kunifundisha computer,kwa waliopita udsm alifundisha AS 217,ndo head of dpartment wa STATISTICS,
 
dah,prof kamuzora mungu amrehemu,ntamkumbuka kwa kunifundisha computer,kwa waliopita udsm alifundisha AS 217,ndo head of dpartment wa STATISTICS,
 
dah,prof kamuzora mungu amrehemu,ntamkumbuka kwa kunifundisha computer,kwa waliopita udsm alifundisha AS 217,ndo head of dpartment wa STATISTICS,

I think he is C.L Kamuzora. Mwalimu wangu wa Statistics enzi hizoooo. St 100.
Jina lake la Kwanza Crisant ( SP)
 
This cannot be happening! Its difficult to swallow! I think I will only believe it when I see the UDSM notice boards on Thursday. Its a sad day.
 
Dah!
Pole kwa wafiwa wote.
Mungu amlaze mahali pema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom