Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Ziara ya Rais Hanang ilitakiwa kuwa very brief, kuangalia madhara yaliyotokea, atoe pole, basi. Nina Imani Rais alishapewa ripoti nzima ya hali ilivyo Hanang na hivyo alikuwa walau na picha ya yaliyojiri, leo ilikuwa kwenda kuwaona waathirika na aongeze nguvu kwa waathirika angalau kuwa sehemu nzuri wakati wanasubiri utaratibu mwingine.

Kama ni kutoa ripoti/salamu nyingine baada ya kuwatembelea wahanga angeweza kufanya hivyo ofisini, wengine tukaangalia mubashara bila kuongeza gharama nyingine ambazo hazina msingi.

Sasa watu wanaandaa mkutano mzima utafikiri anaenda kwenye mikutano yake ya kawaida ya hadhara, nguo za CCM zimetaradadi, mnaenda mpaka na wasanii? Mnazidi kutumia rasilimali kwenye mambo ambayo hayana maana.

Wasanii wenyewe wanaimba upuuzi, eti Rais umeacha vinono Dubai umekuja kutuona hanang! Kwani ni hisani hiyo? Si ni majukumu yake kama Rais kuwa mstari wa mbele kuwajali wananchi anaowatumikia?

Haya mmeamua kufanya yote hayo basi nendeni kwenye point bado mnaanza uchawa! Hao waathirika hawahitaji yote hayo, wanahitaji misaada ya hali mali, wanahitaji kuwa salama, wahitaji faraja, sio uchawa na mambo ambayo hayana maana.

Kwenu nyuki wa mama.

Screenshot 2023-12-07 165141.png

Huyu Hangaya nchi imeshamshinda.

Amekuwa dhaifu kuliko Dhaifu mwenyewe..na watu wanatumia huo udhaifu wake kupiga, ndio maana wanamsifu kila uchao ili aendelee kulala wao watafune.
 
Siasa ni sanaa Mkuu.

ACHA WASANII WACHOTE HADHIRA.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Nchi hii imekuwa na kiwango kikubwa Cha wapumbavu,na mbaya zaidi hawajitambui kuwa ni wapumbavu.
Mtu mwenyewe mpumbavu amebeba maono ya wapumbavu.
 
Ziara ya Rais Hanang ilitakiwa kuwa very brief, kuangalia madhara yaliyotokea, atoe pole, basi. Nina Imani Rais alishapewa ripoti nzima ya hali ilivyo Hanang na hivyo alikuwa walau na picha ya yaliyojiri, leo ilikuwa kwenda kuwaona waathirika na aongeze nguvu kwa waathirika angalau kuwa sehemu nzuri wakati wanasubiri utaratibu mwingine.

Kama ni kutoa ripoti/salamu nyingine baada ya kuwatembelea wahanga angeweza kufanya hivyo ofisini, wengine tukaangalia mubashara bila kuongeza gharama nyingine ambazo hazina msingi.

Sasa watu wanaandaa mkutano mzima utafikiri anaenda kwenye mikutano yake ya kawaida ya hadhara, nguo za CCM zimetaradadi, mnaenda mpaka na wasanii? Mnazidi kutumia rasilimali kwenye mambo ambayo hayana maana.

Wasanii wenyewe wanaimba upuuzi, eti Rais umeacha vinono Dubai umekuja kutuona hanang! Kwani ni hisani hiyo? Si ni majukumu yake kama Rais kuwa mstari wa mbele kuwajali wananchi anaowatumikia?

Haya mmeamua kufanya yote hayo basi nendeni kwenye point bado mnaanza uchawa! Hao waathirika hawahitaji yote hayo, wanahitaji misaada ya hali mali, wanahitaji kuwa salama, wahitaji faraja, sio uchawa na mambo ambayo hayana maana.

Kwenu nyuki wa mama.

Kufa Kufaana!
 
Ccm na chadema wote wapuuzi tuu
Baada ya ccm kupoteza mvuto kwenye jamii, wanafanya Kila wawezalo cdm nayo ionekane ni kama wao. Na mahali popote wananchi wanapoonekana kuikubali cdm waziwazi ni lazima wakomolewe na serekali.

Kuna mlevi mwingine wa madaraka Hadi alifikia kusema hawezi kupeleleka maendeleo walipochagua upinzani, ama kawaambieni cdm wawaletee maendeleo. Aliamini fedha za umma ni zake, na anaweza kuzitoa kama hisani. Kama Kuna kosa limefanyika nchi hii, ni kuendelea kulazimisha ccm ikae madarakani kwa shuruti. Hizi siasa zote za kipuuzi ni kutokana na ccm kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti, huku ikiwa imeshapoteza mvuto na kuchokwa na kizazi hiki.
 
Cha msingi misaada ifike kwa walengwa, isije ikaishia kwenye kamati ya maafa, maana hii nchi inajulikana
 
Back
Top Bottom