M4C: Lema aelekea Ujerumani

Magesi

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
2,587
573
Baada ya kufanya uzinduz wa tawi la CHADEMA mjini london kwa mafanikio makubwa kamanda GODBLESS LEMA ameondoka nchini uingereza na kueleke katika mji wa Frankfut nchini kufungua matawi ya CHADEMA katika muendelezo wa M4C.
 
chanja mbuga kamanda daima tupo nanyi kuelekea kwenye ukombozi wa kweli...aluta continue!!!
 
Wanajuuuuuuuuuuuuuuuta kumvua ubunge!
Viva CDM! Mpaka kieleweke!2015 siyo mbali kazeni buti!
 
Ponda raha mkuu manake hayo matawi yenyewe hayana manufaa zaidi ya kuongeza mzigo wa matumizi kwa chama.Eti go Lema upuuzi mtupu
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.
 
Ponda raha mkuu manake hayo matawi yenyewe hayana manufaa zaidi ya kuongeza mzigo wa matumizi kwa chama.Eti go Lema upuuzi mtupu

Kiaje mkuu?mie mvts hizi nazihofu sana,,zinasambaza ujumbe acha kabisa kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Ponda raha mkuu manake hayo matawi yenyewe hayana manufaa zaidi ya kuongeza mzigo wa matumizi kwa chama.Eti go Lema upuuzi mtupu

Mnatumia kodi zetu vibaya, badala mfungue matawi vijijini mnakimbilia nchi za nje, hivi kuna manufaa gani huko? Naipenda chadema ila kwa mwendo napata wasiwasi nanyi. Hizo garama anazotumia ni za kwake binafsi au za chama? Si ruzuku hio? Kodi zetu? Upuuzi mtupu makamanda wangu mnaoufanya. Huku serengeti hatuna matawi ya chama, sasa hapo mnajitanua nje huku ndani pamejaa? Watz hebu tuache hizi siasa uchwara!
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.

Muda huu M4C inaenda kitongoji kwa kitongoji, mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba na KITANDA kwa KITANDA Wilaya nzima ya KILOMBERO.. Unajipya?.
 
Muda huu M4C inaenda kitongoji kwa kitongoji, mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba na KITANDA kwa KITANDA Wilaya nzima ya KILOMBERO.. Unajipya?.

tz ina vitanda vingapi huko vijijini? itachukua muda gani kuvifikia vyote? ili upate na muda wa ziada wa kufikia hivyo vya watz wa majua, khalafu nyie mnakuwa wa kwanza kumshambulia kikwete kuwa anatumia raslimali vibaya kwa kusafiri nje ya nchi. hapa tofauti iko wapi sasa. mkishauriwa hamtafakari ubishi ndio silaha yenu.
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.

Jua lwako ya cdm yanakuhusu nini? kila timu ina strategies zake za ushindi.
 
Baada ya kufanya uzinduz wa tawi la CHADEMA mjini london kwa mafanikio makubwa kamanda GODBLESS LEMA ameondoka nchini uingereza na kueleke katika mji wa Frankfut nchini kufungua matawi ya CHADEMA katika muendelezo wa M4C.

Mkuu watu waliohudhuria ni Kumi tu tena nane niwakutoka huku kwetu kaskazin hahaha hayo ndio mafanikio?
 
Kashafungua matawi saba aliyotangaza atafungua Uingereza?
Kashakutana na Meya wa London kama alivyosema?
 
Hivi uingereza, marekani, ujerumani na wenzao wanaojiita wameendelea, vyama vyao vya siasa vina matawi bongo? Acheni ulimbukeni.
 
Kakimbia aibu, baada ya kufungua tawi lililokosa wanachama, linalo ongozwa na wauza unga, hakuna mtanzania mwenye akili timamu ataejiunga na chadema chini ya ma-drug dealers, sielewi Lema kaenda UK kwa dili gani na hawa madealers
 
Back
Top Bottom