M4C: Lema aelekea Ujerumani

Mnatumia kodi zetu vibaya, badala mfungue matawi vijijini mnakimbilia nchi za nje, hivi kuna manufaa gani huko? Naipenda chadema ila kwa mwendo napata wasiwasi nanyi. Hizo garama anazotumia ni za kwake binafsi au za chama? Si ruzuku hio? Kodi zetu? Upuuzi mtupu makamanda wangu mnaoufanya. Huku serengeti hatuna matawi ya chama, sasa hapo mnajitanua nje huku ndani pamejaa? Watz hebu tuache hizi siasa uchwara!

Wewe mwongo tu . Mbona hujawaita? Kule ulaya ameombwa kwenda kufungua matawi, ameshakwenda kutimiza wajibu huo . Akirudi opereresheni sangara inaingia huko kwenu Bwagamoyo. Mtazimia mwaka huu
 
I decide to differ. Binafsi siungi mkono ufunguaji wa matawi nje ya nchi ikiwa sehem nyingi vijijini hazijafikiwa. CDM hadi leo kuna wilaya haijazifikia kama vile lringa vijijini,kilolo,mfindi nk.achilia mbali Kata na vijiji.
Kuna kata nyingi sana Tz hazina hata tawi la chama na hata viongozi wa chama. Ni aibu kwa chama kwani kura nyingi wanazopata CCM zinatoka huko vijijini ambako elimu ya ukombozi haijawafikia.

Tz haina utaratibu wa kupiga kura kwa watu walioko nje ya nchi kwamba CDM inatafuta kura huko nje ya nchi. Sasa badala ya kutafuta kura kwa wananchi badala yake tunapoteza hela nyingi kuzurura ulaya wakati hata mwitikio wa watu kule ni mdogo.

Wakati umefika tuelezane ukweli,sio kila anaekosoa CDM haitakii mema,binafsi inaniuma kuziona harakati kama hizi zenye tija ndogo kipindi hiki mhimu kutafuta kila kura ktk kona zote za nchi.
Ndugu yangu kasungura (ruzuku) kenyewe kadogo! ukipopularise CDM nje mapato yanaongezeka na uwezo wa kusambaa ndani unaongezeka. That is common sense. It is part of resource mobilization.
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.

wewe funga mdomo wako! Hata sie twafahamu kwamba vijiji na vitongoji ndio vinatupa kura.
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.

Haikuhusu, hayawahusu wape ushauri huo CCM maana M4C inafumua vijijini kama mchwa
 
Baada ya kufanya uzinduz wa tawi la CHADEMA mjini london kwa mafanikio makubwa kamanda GODBLESS LEMA ameondoka nchini uingereza na kueleke katika mji wa Frankfut nchini kufungua matawi ya CHADEMA katika muendelezo wa M4C.

Huu ni ujuha wa hali ya juu. Hapa Tanzania hata wilaya nyingine haziijui chadema wewe unachoma fedha za walipa kodi kwenda kwenye shopping yako binafsi wakati tunaambiwa uliangukia pua uingereza. Huko unakokwenda ndo kabisaaa unajiharibia na kupoteza muda!
 
Haikuhusu, hayawahusu wape ushauri huo CCM maana M4C inafumua vijijini kama mchwa

Acha ujinga wewe! Chama hakishindi uchaguzi kwa wanachama wake tu! Unapewa ushauri wa bure halafu unaleta nyodo. Kwa aina yako ya ushabiki au ufuasi, Vhadema hawahitaji adui mwingine.
 
Acha ujinga wewe! Chama hakishindi uchaguzi kwa wanachama wake tu! Unapewa ushauri wa bure halafu unaleta nyodo. Kwa aina yako ya ushabiki au ufuasi, Vhadema hawahitaji adui mwingine.

Nani kakuomba ushauri kama si kuweweseka? Matumizi yako ya maneno "ujinga" etc inadhihirisha ulivyofika mwisho wa kufikiri ili mradi unalamba miguu ya wanaokupa riziki ya leo.
 
CHADEMA inapiga kote kote ni muhimu kuwafikia diaspora ili kufikia 2015 baada ya uchaguzi warudi kuja kufanya kazi nchini watu wapo nje ya nchi si kwa sababu ya maisha mazuri huko bali ni kutokana na hali duni na uongozi mbovu ndani ya nchi, Chadema itarejesha majembe nchini waongoze halmashauri na miji ili kuendana na kasi ya ulimwengu na si kuwapa wanajeshi wastaafu wanachojua ni kukagua stock ya mabomu ya machozi tu kuwapiga wapinzani.
 
Acha ulimbukeni, hatufunguwi matawi based on your opinion. Wewe lazima ni gamba gumu
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.

Team ya CHADEMA iko Morogoro sasa, na itaenda wilaya na kata zote na vijiji, itafanya hivyo kwa mikoa minne ya kanda ya kati! Unataka kujua nini zaidi! Lema yuko kwenye kazi maalum ambayo amepangiwa na chama!
 
Huu ni ujuha wa hali ya juu. Hapa Tanzania hata wilaya nyingine haziijui chadema wewe unachoma fedha za walipa kodi kwenda kwenye shopping yako binafsi wakati tunaambiwa uliangukia pua uingereza. Huko unakokwenda ndo kabisaaa unajiharibia na kupoteza muda!
Juha ni wewe taja jina la hyo wilaya ambayo hawaijui CHADEMA achafkramagamba M4C INASANYASANYA WACHA UDUNYA UTAIPENDA MUDA SI MREFU
 
Huu ni ujuha wa hali ya juu. Hapa Tanzania hata wilaya nyingine haziijui chadema wewe unachoma fedha za walipa kodi kwenda kwenye shopping yako binafsi wakati tunaambiwa uliangukia pua uingereza. Huko unakokwenda ndo kabisaaa unajiharibia na kupoteza muda!

Ni wilaya gani hiyo mkuu wasio ijua Chadema?tusaidie nasi tujue please!alafu hv Chadema kumbe siku hizi nao wamekua serikali kwa kukusanya kodi?
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.

Ifakara ni ccm ilifanya mkutano jana.
 
Baada ya kufanya uzinduz wa tawi la CHADEMA mjini london kwa mafanikio makubwa kamanda GODBLESS LEMA ameondoka nchini uingereza na kueleke katika mji wa Frankfut nchini kufungua matawi ya CHADEMA katika muendelezo wa M4C.
Kama lengo la ziara hizi ni kufungua matawi ya chama huko, sioni kama ni priority. Tunazo sehemu nyingi sana humu nchini zenye maelfu ya wapigakura zinazohitaji hili vuguvugu. Nguvu hizi na rasilmali kiduchu zilizopo zingeelekezwa huko kwani ndiko kunakohitajika elimu zaidi kuliko kwa hawa walio majuu ambao sidhani kuwa wanahitaji kwenda kuelimshwa na Lema juu ya nnini wanachohitaji kulikomboa taifa lao.
 
Hakika wanasiasa ni walewale, uzururaji uleule wa jk, hakuna tofauti.
Ponda Raha mkubwa.
 
wakati mwingine nashindwa kuwaelewa hawa cdm, nilitegemea nisikie aelekea kijiji fulani, hawa wa majuu siunaweza kutana nao huku mtandaoni, hebu tumieni akili imarisheni chama vijijini acheni ulimbukeni kama hawa wengine.
Mkuu nafikiri wanachokifanya CDM wako sahihi. Vijijini wameshaanza kwani operation wanazofanya unafikiri zina malengo gani? Kilichobaki sasa pamoja na kuendelea kjieneza vijijini ni kukubalika kimataifa. Niliwahi kuanzisha mada ya CDM waanze kujiimarisha kimataifa na wasisahau kwenda Israel lakini ilifutwa. Huu ndio wakati muafaka wa wao kufanya hivyo katika kuelekea kushika dola.
 
Back
Top Bottom