M-Pesa ni Gharama Sana ! , Soma Hii Muhimu

M-Pesa ni Gharama Sana ! , Soma Hii Muhimu

Pamoja na kulalamikiwa sana kuhusu gharama za miamala ya M-pesa ikiwamo kutoa, kutuma na kuhamisha fedha kuwa gharama kubwa mno na za kinyonyaji, lakini kumbe kuna zaidi.
Nilikuwa sijui kuwa kwa M-pesa hata kuangalia salio unatozwa fedha, fedha inakatwa kwenye akaunti yako.
Jamani watanzania, kwanini tusiigomee M-pesa ????
Kuna mitandao mingi ambayo ni bure

Its the fact ndg!! wapo ghali sana with no reason za maana!!
 
eti kwa nini tusiogomee..... kwa nini usiseme tu mimi nagomea badala ya kutaka kuwaconvince na wengine tena kwa shoddy reasons... kila huduma hata benki kuangalia salio unakatwa itakua iyo!!!!!!!!
 
ni afadhari tunyonywe lakini tupate huduma tunayoitaka kuliko bure,unakwenda bank unakaa masaa 5 kwenye foleni na unapokaribia kufika dirishani tu ,unakuta muhudumu anaongea na simu kjwa dakika zaidi ya 10 wakati wewe unasubiri huduma! potelea mbali bora hii hii mpesa,mara nyingine unakwenda kwenye atm kuchukua pesa na una dharula,unakuta atm haifanyi kazi au inafanya kazi na pesa hakuna! kipi bora? uibiwe lakini upate huduma au usiibiwe lakini usipate huduma? mpesa unapata huduma muda na wakati wowote na sehemu yoyote,iwe mjini au kijijin,lakini hizo bank zenu mwisho ni sehemu zenye lami na umeme tu...naifurahia huduma ya mpesa mpaka basiiiiii...
 
Pamoja na kulalamikiwa sana kuhusu gharama za miamala ya M-pesa ikiwamo kutoa, kutuma na kuhamisha fedha kuwa gharama kubwa mno na za kinyonyaji, lakini kumbe kuna zaidi.
Nilikuwa sijui kuwa kwa M-pesa hata kuangalia salio unatozwa fedha, fedha inakatwa kwenye akaunti yako.
Jamani watanzania, kwanini tusiigomee M-pesa ????
Kuna mitandao mingi ambayo ni bure

kila sehemu kuangalia salio unakata sasa sijui unalalama nini ukiona unaonewa ni bora uweke hela zako kwa kibubu sawa mkuu..
 
Huyu ana matatizo. hizi huduma zimetoa ajira kwa watu. wengi sasa hao wanaokuhudumia mishahara itoke wapi kama sio hayo makato. Unapnda bure nenda Mombasa ule papai la bure huduma ya vinywaji bure ila jioni ulale uache mlango wazi kidogo ili mlipa bili akifika asipate usumbufu kugonga mlango ni kusukuma tu.
 
Pamoja na kulalamikiwa sana kuhusu gharama za miamala ya M-pesa ikiwamo kutoa, kutuma na kuhamisha fedha kuwa gharama kubwa mno na za kinyonyaji, lakini kumbe kuna zaidi.
Nilikuwa sijui kuwa kwa M-pesa hata kuangalia salio unatozwa fedha, fedha inakatwa kwenye akaunti yako.
Jamani watanzania, kwanini tusiigomee M-pesa ????
Kuna mitandao mingi ambayo ni bure
This is the world of business class.
Hamia TTCL
Ahsante kwa maoni.
 
Pamoja na kulalamikiwa sana kuhusu gharama za miamala ya M-pesa ikiwamo kutoa, kutuma na kuhamisha fedha kuwa gharama kubwa mno na za kinyonyaji, lakini kumbe kuna zaidi.
Nilikuwa sijui kuwa kwa M-pesa hata kuangalia salio unatozwa fedha, fedha inakatwa kwenye akaunti yako.
Jamani watanzania, kwanini tusiigomee M-pesa ????
Kuna mitandao mingi ambayo ni bure

Mkuu ungefanya utafiti wa kuangalia watoa huduma wengine wanachaji gharama kiasi gani, reliability ya huduma zao, upatikanaji wake, na time utakayotumia n.k. n.k.

Baada ya kulinganisha na kuchambua takwimu zako ndipo ungekuja na mapendekezo ambayo pengine yangepelekea kutuaminisha kwamba Vodacom wanachaji gharama kubwa kutumia huduma yao ya Mpesa.

Lakini kwa kukusaidia tu, jaribu yafuatayo:

1. Fungua account benk ya NBC au NMB au benki yoyote na tumia huduma mbali mbali kama unazopata kupitia Mpesa.
2. Jiunge na Airtel money ama tiGo pesa na tumia huduma mbali mbali kama unazotumia kupitia Mpesa
3. Au hata jaribu kuweka pesa zako kwenye Saccos ama vibubu alafu ukitaka kumtumia hela ya matumizi mzee wako aliye Makongorosi au Mkuranga, tuma kwenye basi.

Ukishajiuliza mambo hayo utakuja na jibu kuwa Mpesa ni huduma nafuu na yenye uhakika kuliko huduma nyingi sana hapa Tanzania. Unatuma sh. 100,000 Songea, mtu unayemtumia anapata hela instantly kwa gharama ya sh. 1000 afu unasema ni gharama sana? Washa gari nenda NMB ka deposit km 20 toka ulipo ka deposit kwenye account yake uone ita ku cost sh. ngapi?

Hawa watu wamewekeza miundombinu, wameajiri watu, wameweka ma agent nchi nzima karibu kila kitongoji/mtaa alafu wewe unasema sh. 50 wanayokukata kuangalia balance ni kubwa sana???

Hauko serious mkuu!
 
ukiona hivyo jua kafulia..na tarehe zenyewe hizi?maana mtu kama una hela izo deductions ni minor sana....halo haloooo!! umefulia hadi inzi wamehamia kwa jiraniii!!
 
dunia ya sasa vitu vya bure vimeisha,hakuna sehemu utaweka ela bure,hiyo ni biashara lazima na wenye vibanda nao wapate,mnagawana,ata labda utengeneze kibubu cha mbao uweke
 
msituburuze M-pesa ni ghari sana viwango vyao vya huduma ebooo! acha atetee wanyonge bwana
 
Nenda airtel utalijua jiji.ukikosea tu hupati fedha yako...kuna mtu ana mwezi wa 4 alikosea kutuma mpaka leo hajrudishiwa 100,000 yake baba.vodacom angalau.


kwaheri
​
 
Pamoja na kulalamikiwa sana kuhusu gharama za miamala ya M-pesa ikiwamo kutoa, kutuma na kuhamisha fedha kuwa gharama kubwa mno na za kinyonyaji, lakini kumbe kuna zaidi.
Nilikuwa sijui kuwa kwa M-pesa hata kuangalia salio unatozwa fedha, fedha inakatwa kwenye akaunti yako.
Jamani watanzania, kwanini tusiigomee M-pesa ????
Kuna mitandao mingi ambayo ni bure

Hata tigo nao wanakata.
 
kwa hiyo hao wafanyakazi unataka walipwe na mawe acha upuuzi
 
kwa hiyo ulitaka M-pesa itowe sadaka usha wahi kujua gharama ya kujenga hata mnara mmoja tu wa mawasiliano kwa nini watanzania tume kuwa wa kulalamika kila kukicha?
 
Mkuu Richard Mlangi ushauri wako mzuri,kuna haja ya hizi mamlaka za udhibiti pamoja na kampuni za simu kumuangalia mtumiaji wa mwisho wa hizo huduma kuliko kumbebesha gharama zote.Kwa tunaotumia hiyo huduma mara kwa mara inatuumiza.Angalau kidogo huu ushindani umesababisha turudishiwe gharama kiasi kwa njia ya muda wa maongezi!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na kulalamikiwa sana kuhusu gharama za miamala ya M-pesa ikiwamo kutoa, kutuma na kuhamisha fedha kuwa gharama kubwa mno na za kinyonyaji (ukilinganisha na mitandao mingine ya simu), lakini kumbe kuna zaidi.
Nilikuwa sijui kuwa kwa M-pesa hata kuangalia salio unatozwa fedha, fedha inakatwa kwenye akaunti yako.

My Opinion:
The responsible authorities should standardize and control this mobile banking business to protect the customers and ensure fair trading !

Nahisi itakuwa ndio mara yako ya mwanzo na mwisho kupost ujinga humu..... hahahahha dah umeipata mkuu pole yako
 
Hata Tigo Pesa ukiuliza salio wanakata sh 50/=
 
Back
Top Bottom