TUNTEMEKE
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 4,587
- 579
Katika hali isiyo ya kawaida Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) ameachwa katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu licha ya kuomba huku makamu wake, katibu mkuu wake, naibu katibu mkuu wake wakiteuliwa. hali hii ni picha mbaya kwani katika kura zilizopigwa na wanawake chadema mwezi august alikuwa namba 2 kabla hawajatoa visingizio vya uchaguzi kuharibika baada ya kuona wateule wao wakiwa wamefeli kwa mbali.
mchakato wa uteuzi uliofanyika na vigogo kina dr. slaa, mbowe na lissu umepelekea wanawake wengi wenye sifa kuachwa huku dada wa tundu lissu ambaye hana uzoefu wala mchango ndani ya chama akipewa ubunge, mke wa dr. slaa rose kamili naye kazawadiwa ubunge kutokana na kuwa kimya wakati wa sakata la mchumba na ilikuwa moja ya makubaliano ya ukimya wake. kama kawaida ndesamburo kaingiza binti yake na mkwewe katika ubunge na waliosalia wengi ni wapenzi wa vigogo.
katika hali hiyo tunashindwa kupima demokrasia wanayoipigia kelele kila siku.
cha kushangaza ni kitendo cha Dr. Mkumbo kuaibisha taaluma yake kwa kujitokeza mbele ya umma wa watanzania na kusema kuwa yeye ndie aliyeweka vigezo vya uteuzi, ni kwa nini asingewashauri kuruhusu demokrasia? ni kweli ktk demokrasia kuna vigezo vipi? mbona hata wenye sifa kubwa akiwemo huyo mwenyekiti wa wamama ambaye kapigania chama kwa miaka, ana elimu na uzoefu mkubwa kaachwa?
huu ni ubabaishaji wa hali ya juu.
Hayati Chacha Wangwe katika uhai wake alipigania sana haki ndani ya chadema na mojawapo ni uteuzi wa viti maalum kinddugu, kifamilia, kiukoo na kimapenzi.
katika hali hii hiyo demokrasia itajengwa vipi?