M/kiti wanawake chadema ahujumiwa

Katika hali isiyo ya kawaida Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) ameachwa katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu licha ya kuomba huku makamu wake, katibu mkuu wake, naibu katibu mkuu wake wakiteuliwa. hali hii ni picha mbaya kwani katika kura zilizopigwa na wanawake chadema mwezi august alikuwa namba 2 kabla hawajatoa visingizio vya uchaguzi kuharibika baada ya kuona wateule wao wakiwa wamefeli kwa mbali.
mchakato wa uteuzi uliofanyika na vigogo kina dr. slaa, mbowe na lissu umepelekea wanawake wengi wenye sifa kuachwa huku dada wa tundu lissu ambaye hana uzoefu wala mchango ndani ya chama akipewa ubunge, mke wa dr. slaa rose kamili naye kazawadiwa ubunge kutokana na kuwa kimya wakati wa sakata la mchumba na ilikuwa moja ya makubaliano ya ukimya wake. kama kawaida ndesamburo kaingiza binti yake na mkwewe katika ubunge na waliosalia wengi ni wapenzi wa vigogo.
katika hali hiyo tunashindwa kupima demokrasia wanayoipigia kelele kila siku.
cha kushangaza ni kitendo cha Dr. Mkumbo kuaibisha taaluma yake kwa kujitokeza mbele ya umma wa watanzania na kusema kuwa yeye ndie aliyeweka vigezo vya uteuzi, ni kwa nini asingewashauri kuruhusu demokrasia? ni kweli ktk demokrasia kuna vigezo vipi? mbona hata wenye sifa kubwa akiwemo huyo mwenyekiti wa wamama ambaye kapigania chama kwa miaka, ana elimu na uzoefu mkubwa kaachwa?
huu ni ubabaishaji wa hali ya juu.
Hayati Chacha Wangwe katika uhai wake alipigania sana haki ndani ya chadema na mojawapo ni uteuzi wa viti maalum kinddugu, kifamilia, kiukoo na kimapenzi.
katika hali hii hiyo demokrasia itajengwa vipi?

Bila shaka wewe mchawi...

Malalamiko yako ya ki-makamba na kinana kapekeleke kule Mtaa wa Nhkrumah, maana ndio wanapigana majungu, yule aliyekataliwa kuwa hana akili sawasawa kuweza kuongoza jumuiya ya akina-mama wa Makamba, si ndiye aliteuliwa Mkuu fulani wa Wilaya?? ...Hiyo akili ya kuongoza wilaya aliipata wapi??....Majungu tu....

Poleni sana...:evil:
 
..naona kama aliyeweka orodha ya viti maalum ya chadema ameshamjibu mtoa huu upupu. na hii ndio ishara itakayokuwa bungeni 2010-2015, jamaa wanatoa upupu, peoples' power wanajibu kwa hoja na ushahidi. haya sikuikifika wasilana na MS ulete upupu mwingine!
 
Nadhani hili swala la Viti maalumu litakwisha 2015. Kwa nini tuwe na hivi viti anyway? why? Nilidhani Mkutano wa Beijing utakuwa umemaliza swala la usawa. Kina mama inabidi wapande Majukwaani, wapo kama kina Halima Mdee, wamejaribu na wameshinda. Wapo kina Anna Kilango. Kwa nini wengine wasijaribu? Kwa nini Mohonga akujaribu Kigoma mjini? Kazaliwa Kigoma, kakulia Kigoma, kasoma UDSM na anaijua politics.

Chadema waangalie zambi ambayo inawatafuna CCM leo isije ikawapata. Mfumo wa kutengeneza special favor, huuu ni mfumo hatari sana. Sijui vigezo vya uchaguzi vilivyo tumika, na siwafahamu waliochaguliwa. Lakini ni wazi kabisa kwamba Chadema kinakuwa sasa, basi nilazima uwekwe mchakato wa kusaidia chama kisimame vizuri bila kuteteleka. Kichague watu ambao wana vigezo vya uongozi bila kuangalia Dini, Kabila, jenda, undugu na n.k.

Naamini Kitila ni mtu mwenye uwezo, basi ni dhahiri kabisa kama watu aliowachagua walikuwa na vigezo vya uongozi. Tunataka watu watakao simama kidete kutetea Watanzania, na sio watakao shangilia kupewa mashangingi.

Kama Chadema ikiendelea kwenye njia njema iliyo anza nayo, basi wengi tutajiunga.. Nilishawai kumwambia Zitto hofu yangu ni baadhi ya viongozi wa Chadema wanaweza kukifanya hichi chama kikawa kama NCCR mageuzi, sababu ya UMIMI and special favors. Yet the jury is still out.
 
Ndani ya CCM kuna watu wafuatao;
  1. Yusuph Makamba na January Makamba
  2. Jakaya Kikwete na Ridhiwani Kikwete (na mdogo wake Miraji Kikwete)
  3. Samwel Sitta na Margret Sitta
  4. Zainab Kawawa na Vita Kawawa
  5. John Samwel Malecela na Ane Kilango Malecela
  6. Dr Abdalla Kigoda na Aisha Kigoda
Na wengine weeeengi wenye mahusiano....hao waliopo kwenye listi unawafahamu nyadhifa zao na jinsi gani walifika walipo sasa? Unasemaje kuhusu hawa?
 
Ama kweli mwaka huu, mara huyu karopoka, mara yule kakurupuka na je Bungeni kutatokea nini? Naomba pasitokee tetemeko litokanalo na hoja za nguvu, bali nguvu za hoja....

Ipo siku giza na mwanga vitajitenga, tena, siku hiyo yaja ambapo wapiganaji wa kweli ndani ya CCM na CHADEMA watajulikana wazi wazi bila kificho kwa wanachi. Enyi wabunge, kumbukeni mmeahidi nini kwa wananchi. Wananchi wamefungua mafaili ya AHADI za wagombea, haya, kazi kwa wagombea mlioshinda!
Hayo ndiyo maneno:smile-big:
 
Wapo Zanzibar na CUF yote!
Mkuu nilijua tuu utanijibu pole sana mjomba sema nina furaha teacher wangu kaingia mjengeno(bungeni) lazima wanawake wote wawe na heshima kwa sababu huyu mama na watoto wake yupo very strong hata kumchana live bila ya chenga mwanamke anaye uleta umambo leo
 
mod tunaomba kijana awajibishwe na matusi yake tafadhali hili sio jukwaa la matusi pls

kweli sisiem hajui matusi au mnajitia ujinga maana kuanzia makamba,na yule msomali kinana

Unaonyeshwa madhali ya kutumwa na kufanya vitu for money itakupeleka huko careful
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) ameachwa katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu licha ya kuomba huku makamu wake, katibu mkuu wake, naibu katibu mkuu wake wakiteuliwa. hali hii ni picha mbaya kwani katika kura zilizopigwa na wanawake chadema mwezi august alikuwa namba 2 kabla hawajatoa visingizio vya uchaguzi kuharibika baada ya kuona wateule wao wakiwa wamefeli kwa mbali.
mchakato wa uteuzi uliofanyika na vigogo kina dr. slaa, mbowe na lissu umepelekea wanawake wengi wenye sifa kuachwa huku dada wa tundu lissu ambaye hana uzoefu wala mchango ndani ya chama akipewa ubunge, mke wa dr. slaa rose kamili naye kazawadiwa ubunge kutokana na kuwa kimya wakati wa sakata la mchumba na ilikuwa moja ya makubaliano ya ukimya wake. kama kawaida ndesamburo kaingiza binti yake na mkwewe katika ubunge na waliosalia wengi ni wapenzi wa vigogo.
katika hali hiyo tunashindwa kupima demokrasia wanayoipigia kelele kila siku.
cha kushangaza ni kitendo cha Dr. Mkumbo kuaibisha taaluma yake kwa kujitokeza mbele ya umma wa watanzania na kusema kuwa yeye ndie aliyeweka vigezo vya uteuzi, ni kwa nini asingewashauri kuruhusu demokrasia? ni kweli ktk demokrasia kuna vigezo vipi? mbona hata wenye sifa kubwa akiwemo huyo mwenyekiti wa wamama ambaye kapigania chama kwa miaka, ana elimu na uzoefu mkubwa kaachwa?
huu ni ubabaishaji wa hali ya juu.
Hayati Chacha Wangwe katika uhai wake alipigania sana haki ndani ya chadema na mojawapo ni uteuzi wa viti maalum kinddugu, kifamilia, kiukoo na kimapenzi.
katika hali hii hiyo demokrasia itajengwa vipi?

Tazama hapa mkuu,
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/23075-sophia-simba-uwt-vs-naomi-kaihula-bawacha-2.html
 
Back
Top Bottom