Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Pundamilia07,
Je, kwanini Mh Lwakatare hajisafishi katika tuhuma ambazo aliambiwa kuwa alifanya ubadhirifu wa fedha ya chama?
Kukaa kimya maana tutaelewa kuwa tuhuma zilikuwa ni za kweli.
Mkuu siasa za Bongo ndio hizo.. Lwakatare hawezi kujisafisha ikiwa hakuna madai ya tuhuma hizo wazi. Alichokifanya ni kuwasilisha tuhuma hizo kama zilivyotoka na kama umesoma vizuri hotuba zote zimekuwa zikimlenga Mh. Mwenyekiti na wajumbe waliohudhuria kupata jibu japo ufafanuzi..

Ina maana kama kungekuwa na jibu la hoja zake Mwenyekiti au wajumbe wangesherehesha lakini kama ilivyoandikwa hoja zote za Lwakatare ni simulizi ama vile alivyoambiwa na watu fulani.. Hakuna mtu ndani ya CUF anakubali kusimama na kutoa shutuma hizo dhidi ya Lwakatare wala kusimamisha madai hayo kama mshuhuda..Kifupi Lwakatare kisha tafutiwa FITNA, and he has to go!.. katika siasa za fitna siku zote hakuna masimulizi wala explanations.. watu hawawezi kukutazama machoni, Ukianzisha tu watu hugeuza shingo zao wakaondoka.. life goes on!
 
Pamoja na yote haya jambo moja linaniumiza moyo ni kwa jinsi poverty inachangia kuua uzalendo wa raia. Just think kama anayoeleza ni ukweli naamini aliingia upinzani kwa nia ya kupigania haki kwa wote kama baba wa taifa alivyofanya kwa welfare ya watu wote; think of who are now paying the price of uzalendo wa hawa watu wawili? The family ofcourse then just ask your self wanaofanya ufisadi ili kulinda hadhi zao na familia zao ni kosa lao au kosa la mfumo ambao kutokana prisoners dilema hakuna anaethubutu kujitoa mhanga kwani the risk is very high.

Ebu tukae kwa utulivu tukubali kujenga welfare kwa watu wote then atakaetufisadi tutajua hata tukimhukumu hatutamwonea huruma.

How can we do that?

Kuna kitu kinaitwa 'afirmative measures' tunaitumia sasa kwa wanawake ili kuwajengea uwezo wakushiriki katika maendeleo ya nchi kutokana na disadvantage ya mfumo dume. Then we can do that to all the people waliotoa mchango kwa taifa hili ambao wataathirika kwa kubadili mfumo iliopo; then from there tuweke system iliyo democratic yenye kuweza ku involve majority kwenye production na kwenye ku question if few are monopolising the power to decide on things.

Can we do that JF? Its not through comfrotation but through negotiation. How many are volunteering for that?

Hii kutegemea vyama naona imefail long time a go kwasababu risk ni kubwa kwa individuals kwani hakuna safety nets kwa wazalendo wachache.

Binafsi sijawahi kuwa member wa chama chochote lakini napenda opposition kwasababu sioni raha yoyote ile ya ku-enjoy favours za chama tawala while masses are suffering for not having even a single meal a day. I have continued with studies not because of anything my happiness will be to come up with a kind of revolution into raising up the standard of living of atleast 30% of rural poor to just have basic needs of food shelter and clothing. And if I will ever reach this objective even if I die the following day after realising this I will die like a bilionnaire. The knowledge is already with me am struggling wit the strategy to implement the ideas na hii ya vyama naona usiku tu bora niangalie ustaarabu mwingine.
 
Pundamilia07,
Mkuu siasa za Bongo ndio hizo.. Lwakatare hawezi kujisafisha ikiwa hakuna madai ya tuhuma hizo wazi. Alichokifanya ni kuwasilisha tuhuma hizo kama zilivyotoka na kama umesoma vizuri hotuba zote zimekuwa zikimlenga Mh. Mwenyekiti na wajumbe waliohudhuria kupata jibu japo ufafanuzi..

Ina maana kama kungekuwa na jibu la hoja zake Mwenyekiti au wajumbe wangesherehesha lakini kama ilivyoandikwa hoja zote za Lwakatare ni simulizi ama vile alivyoambiwa na watu fulani.. Hakuna mtu ndani ya CUF anakubali kusimama na kutoa shutuma hizo dhidi ya Lwakatare wala kusimamisha madai hayo kama mshuhuda..Kifupi Lwakatare kisha tafutiwa FITNA, and he has to go!.. katika siasa za fitna siku zote hakuna masimulizi wala explanations.. watu hawawezi kukutazama machoni, Ukianzisha tu watu hugeuza shingo zao wakaondoka.. life goes on!

Mkandara,
Tunapoongelea siasa na wanasiasa jina Julius Kambarage Nyerere ni jina kubwa sana katika nyanja hizo.

Ninakumumbuka katika hotuba yake maarufu sana ya mwishoni katika uhai wake aliyoitoa pale Kilimanjaro Hotel (sasa Kempinski) alisema kuwa mke wa Kaisari anatakiwa awe safi wakati wote, tuhuma yeyote kwa mke wa Kaisari ni sawasawa na kosa lenyewe na kinachofuata ni adhabu.

Sasa Mh tayari amekwishaambiwa sababu za msingi za kutokupendekezwa kwa jina lake ni kuhusiana na ubadhirifu wa fedha za chama. Kwangu mimi kwa mwanasiasa makini hii ni tuhuma nzito hasa pale ambapo katika maelezo yake hajasema kuwa CUF walikanusha mahali popote. Leo hii inawezekana CUF wameishikilia hiyo tuhuma ya ubadhirifu wa fedha za chama kama 'turufu' yao ya mwisho kwa Lwakatare na ndiyo maana waliweza kumtaka mtama kingunge kama yeye kiurahisi kabisa.

Ingekuwa tunataka kuleta simulizi za kwenye biblia basi Lwakatare si sawasawa na Samson.
 
Pundamilia07,
Hapana mkuu mimi siitazami picha hii kama unavyoitazama. Kwanza kumbuka maelezo yote aliyoambiwa Lwakatare ni nje ya kiofisi, hakuna barua wala maelezo yalitolewa na uongozi wa CUF kwa nini jina lake halikuteuliwa kugombea tena kiti hicho, jambo ambalo hata mke wa Kaisali asingeweza kujisafisha maadam talaka imeshatolewa..Unajisafisha ili iwe nini?...utajisafisha wakati tuhuma zinapowekwa mbele yako na hujapoteza ndoa lakini sii baada..Lolote utakalo sema halina turufu kwani mume kisha fikia maamuzi ya kuvunja ndoa hata kama hukufanya baya lolote...kifupi ameshakuchoka!

Uamuzi uliofikiwa ni sawa na ule wa Mzee Malecela alipotaka kugombea Urais, jina lake liliondolewa hata kabla ya wajumbe kupiga kura. Kama kweli Lwakatare angekuwa hivyo wanavyodai basi hapakuwa na haja ya kuondoa jina lake maanake kura asingezipata..sidhani kama wajumbe wangeweza kumchagua mtu wa aina hiyo tena chama chenyewe CUF!..Hivyo binafsi nina imani kabisa kwamba viongozi wa juu wa CUF walikosa imani na mtu huyu yapo maswala mazito zaidi ya madai yaliyotolewa pengine hata hizo tuhuma za kuhamia Chadema ama yawezekama pia msimamo wake kuhusiana na swala la RA linapingana na mtazamo wa viongozi wa CUF kina Lipumba..

Kifupi mkuu wangu CCM wamekwisha ifanya kazi wanayotakiwa kuifanya kabla ya uvhaguzi wa mwaka 2010..Vyama vya Upinzani vimebakia dhaifu kabisa, kujitoa kwa Zitto, Lwakatare na wengine kibao watafuata wakiwa na sababu za msingi kabisa..
Mwisho wa picha nzima mkuu wangu - NJAA mkuu wangu njaa ndiye adui mkubwa wa Umaskini angalia kilio chote cha Lwakatare kimeishia wapi?..kalia na tumbo lake akatiwe japokuwa kidogo maanake haoni mbele (future) nje ya CUF pamoja na majigambo yote yaliyotangulia...
 
Muda mfupi uliopita Mh. W.M.Lwakatare alikuwa na mkutano wa hadhara na wanachi wa jimbo la Bukoba mjini, Katika uwanja maarufu wa mikutano wa uhuru.
Inasemekana Lwakatare aliitisha mkutano huu ili kueleza wanachama wa CUF na wapenzi wake kisiasa nini kimetokea na kumlazimisha ajiuzulu uongozi wote ndani ya CUF na kuamua kurudi hapa jimboni.
Aliwaeleza kila kitu cha mapungufu, kilichoko katika chama chao na ubovu ulio katika uongozi wa juu wa chama.

Mwisho aliwauliza watu waliohudhuria mkutano huo je wanaonaje aendelee kukaa katika chama cha CUF au ahamie Chadema? Umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria ni watu wawili tu walionyoosha mkono kwamba aendelee kubakia CUF na wengine wote katika mkutano walinyoosha mkono walipoulizwa ni wangapi wanataka ahamie Chadema.

Hakutoa uamuzi pale pale lakini aliomba samahani kwa wananchi kwamba ingawa wengi wameomba hivyo, bado atahitaji muda kutafakari yeye pamoja na familia yake kabla ya kuja na uamuzi kamili.

Mwisho aliendelea kuuza vitabu viwili ambavyo vilikuwa vikieleza yale yaliyomsibu hadi akaachia uongozi ndani ya CUF. Bila shaka ni vile ambavyo tayari tumeshapewa hapa JF.

Chadema mpooooooooooooooooooo?????????????????????????? mmesikiaaa????????????? njia nyeupe kwenu jimbo la Bukoba mjini 2010. Kazi kwenu.

Aliyenipatia habari hakunipa na picha hivyo safari hii mtaniwia radhi.

Habari ndiyo hiyo.
 
We knew this was coming, and still more..just a matter of time,, tutamsikia huyoooo kaondoka CUF jumla. Ndo ameshaanza kampeni hivyo!
 
Mshaurini huyu Lwakatare kama anataka kwenda CHADEMA ajitoe tu taratibu kwani hiyo haki anayo.

Njia anazoanza kutumia sasa za kuonyesha CUF wana matatizo kumbe lengo lake ni kuhama zitamfanya hata huko CHADEMA wasimwamini.

Ukimtukana mpenzi wakati unadai talaka kila mtu anajua una chuki.

Hayo anayowaambia CUF yana make sense kama anabaki CUF lakini kama anahama basi katumia njia mbaya.
 
Mwisho aliwauliza watu waliohudhuria mkutano huo je wanaonaje aendelee kukaa katika chama cha CUF au ahamie Chadema? Umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria ni watu wawili tu walionyoosha mkono kwamba aendelee kubakia CUF na wengine wote katika mkutano walinyoosha mkono walipoulizwa ni wangapi wanataka ahamie Chadema.

Kwanza nikushukuru Mkuu kwa kutujuvya habari hii. Lakini mbona imekaa kushotokushoto, nikimaanisha kuwa maeneo niliyoyapigia mstari na italiki katika stori yako. Nilipata kajifikra kuwa huwenda ww umejaaliwa sana mwenzetu na macho ya uoni wa mbali, kiasi kuwa umeweza katika "umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria", kubaini mikono ya watu wawili tu, na tena umati huo wooote uliuona ukinyooosha mikono ukitaka Mh. Lwakatare ahamie CHADEMA.
 
Inasemekana Lwakatare aliitisha mkutano huu ili kueleza wanachama wa CUF na wapenzi wake kisiasa nini kimetokea na kumlazimisha ajiuzulu uongozi wote ndani ya CUF na kuamua kurudi hapa jimboni.Mwisho aliwauliza watu waliohudhuria mkutano huo je wanaonaje aendelee kukaa katika chama cha CUF au ahamie Chadema? Umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria ni watu wawili tu walionyoosha mkono kwamba aendelee kubakia CUF na wengine wote katika mkutano walinyoosha mkono walipoulizwa ni wangapi wanataka ahamie Chadema
inamana hata hao wanachama wa CUF waliokuwapo hapo mkutanoni wameamuwa kukihama chama cha CUF pamoja nae na kwenda chadema isipokuwa hao wawili tu ?
 
Siku Imefika!
unapoona mambo kama haya yameanza kutokea, kwa ma-striker wakali katika siasa za Tanzania kuhamia katika timu kali ujue ya kuwa muda wa kushinda ligi ya mabingwa umekaribia.
ni vyema Viongozi katika ngazi mbalimbali za uongozi Tanzania wakajifunza kuthamini michango ya wenzao na si kufanya vyama kama NGOs zao na kuwafanyia hiyana wenzao pindi wanapokuwa wameshika usukani.
pia nawapongeza wakazi wa Bukoba Mjini kwa kumchagulia mpambanaji wao Chama Makini ili aweze kufanya siasa halisi na zenye nia ya kuleta ukombozi wa kweli.
 
Mpiganaji Lwakatare naamini familia yako itabariki na kuheshimu maamuzi ya wananchi wa Bukoba Mjini.Hivyo tunaisubiria kwa hamu siku ya kubatizwa rasmi na kuungana na wapambanaji wenye nia ya kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Naweza kusema kuwa nchi hii haina siasa za kweli, kilichopo ni hisia binafsi za wanasiasa na kufuata mikumbo. Kinachoonekana hapa ni kutaka kukipaka chama picha ya uislaam. Ni ukweli ulio wazi kuwa bw Rwakatale alikuwa mhimili mkubwa wa kuondoa dhana ya uislaam iliyojengeka katika jamii ya kitanzania juu ya chama cha CUF. Amini usiamini udini sasa unaingia tanzania tena kwa kasi kubwa.
 
Kama ripoti ni accurate (sadly I find myself prefacing most of my positions with that phrase, due to the obvious unreliability of our "press") huyu jamaa si kiongozi, ni mzugaji tu.
 
Tabia kama hizi za wanasiasa kama Lwakatare ni tabia za wanasiasa njaa, wanajiuza kwa kupitia umaarufu fulani, wadau mnakumbuka ya Danny Makanga na "Bwana Mapesa", nini matokeo yake, kanunuliwa na mafisadi akatumiwa yupo wapi sasa? Na Lwakatare naona anaelekea huko huko, anajipitisha pitisha zone za Makamba tu,karibuni naye atamfuata Tambwe Hiza. Anajinadi CHADEMA, anajua hasa anakolenga shabaha yake. Tusubiri tuone.
 
Kwanza nikushukuru Mkuu kwa kutujuvya habari hii. Lakini mbona imekaa kushotokushoto, nikimaanisha kuwa maeneo niliyoyapigia mstari na italiki katika stori yako. Nilipata kajifikra kuwa huwenda ww umejaaliwa sana mwenzetu na macho ya uoni wa mbali, kiasi kuwa umeweza katika "umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria", kubaini mikono ya watu wawili tu, na tena umati huo wooote uliuona ukinyooosha mikono ukitaka Mh. Lwakatare ahamie CHADEMA.

Umenena vyema!! Mkutano ulikuwa wa chama cha CUF, na wanachama wote wa CUF isipokuwa wawili tu walimtaka ahamie Chadema, hapo kuna walakini wa kuripoti au habari imekuwa exagerated kwa malengo maalumu, hata kama kuna chembe ya ukweli ndani yake.
 
Last edited:
Kwanza nikushukuru Mkuu kwa kutujuvya habari hii. Lakini mbona imekaa kushotokushoto, nikimaanisha kuwa maeneo niliyoyapigia mstari na italiki katika stori yako. Nilipata kajifikra kuwa huwenda ww umejaaliwa sana mwenzetu na macho ya uoni wa mbali, kiasi kuwa umeweza katika "umati mkubwa sana uliokuwa umehudhuria", kubaini mikono ya watu wawili tu, na tena umati huo wooote uliuona ukinyooosha mikono ukitaka Mh. Lwakatare ahamie CHADEMA.

Wawili=abaki CUF
Waliobaki wote=aende chadema

Mbona mgumu wa kuelewa mkuu? Kweli inaumiza kwa ndugu zangu wana kafu lakini ndio ukweli tena ukweli mtupu. Fuatilia. Hiyo ndio Bukoba. Tafuta source zako mwenyewe toka Bukoba kuhakiki habari hii, usianze kupinga tu.

MF
 
Umenena vyema!! Mkutano ulikuwa wa chama cha CUF, na wanachama wote wa CUF isipokuwa wawili tu walimtaka ahamie Chadema, hapo kuna walakini wa kuripoti au habari amekuwa exagerated kwa malengo maalumu, hata kama kuna chembe ya ukweli ndani yake.

Soma vizuri habari hiyo tena. Ondoa hapa uzushi wa kitu ambacho sikukiandika.

*Hakuna nilikoandika kuwa mkutano ulihudhuriwa na wana kafu peke yao.
*Wala sikusema wale wawili walionyoosha mkono against kafu walikuwa wana kafu.

Kama wewe una data za hakika weka thread yako usilete upotoshaji hapa. Hizi habari nimezipata kutoka kwenye zaidi ya source tatu kule Bukoba.
 
Wawili=abaki CUF
Waliobaki wote=aende chadema

Mbona mgumu wa kuelewa mkuu? Kweli inaumiza kwa ndugu zangu wana kafu lakini ndio ukweli tena ukweli mtupu. Fuatilia. Hiyo ndio Bukoba. Tafuta source zako mwenyewe toka Bukoba kuhakiki habari hii, usianze kupinga tu.

MF
Mkuu mm sipingi.
Huo umati ulioelezea hapo ni mkubwa mno kiasi kuwa hawa wawili tu ndio uliwaona ww (au umehadithiwa Mkuu?) pia si vibaya ushatusaidia, halafu zaidi heading inasema "wananchi wa Bukoba wataka...." wakati mkutano ni wa CUF waliohudhuruia hapo ni wanachama wa CUF(au niseme ni wa Lwakatare),halafu mkuu unaapa? unasema "...ukweli mtupu..."
 
Kwenye umati mkubwa unaweza kuhesabu mikono na kuona miwili tu?

Wanacheza hawa, either kulikuwa na watu wa kuhesabika, au hawakuweza kuthibitisha kwamba ni mikono ya watu wawili tu.

The whole presentation seems like there is a big PR move behind this, wote hawana imani yangu, si CUF wala huyu Lwaka nani sijui, wasanii watupu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom