Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,999
- 1,187
Just thinking... hivi mkuu mwiba yu wapi siku hizi?
Aende huko Chadema haya mambo ya ku beep yanampotezea muda
Just thinking... hivi mkuu mwiba yu wapi siku hizi?
Masa,Anaweza pia kuachana na siasa hakuzaliwa awe kwenye vyama, kama ni msomi afanye kazi za professional yake mchango kwa taifa utaonekana!
Ni lazima Wilfred aendelee kushiriki siasa.
FYI nyota yake kule Bukoba bado inang'ara. Akiacha kuji involve katika siasa atakuwa amewa let down wapenzi wake kule Bukoba.
Matokeo turn out ya wapiga kura katika jimbo la Bukoba mjini watapungua sana maana naamini, narudia naamini wengi watajikata kutopiga kura.
Na hii itakuwa ni kwa faida ya sisi M......
Kweli hata mi nimemiss sana michango yake hapa,, sijui amekumbwa na nini?
Sitaki niwe bias katika hili suala la Bw Wilfred na wenzake wa CUF. Ninadhani tukipata maelezo ya upande wa pili tutakuwa tumepata mwanga mzuri zaidi wa sakata lake la uongozi.
But to chip in while waiting to hear much from the other side, ninaona kuwa Mh Wilfred alisahau kuwa uongozi ni dhamana tu na wala si kitu cha kulalamika hasa pale unapoukosa kwa mujibu wa taratibu halali. Nikisoma mawazo yake alitegemea kuwa ataendelea kuwa kiongozi bila ya kujali ukomo na kupisha wengine kuleta fresh idea. Yeye mwenyewe anakiri kuwa hali ya kisiasa kwa CUF upande wa bara si nzuri na amekuwa katika Uongozi wa juu kwa kipindi cha kutosha. Nafikiri ni vema akaondoa kinyongo na badala yake aendelee kuwaomba wakuu wake wampatie kile ambacho ni halali yake.
Lakini hata hivyo ametoswa wakati mbaya sana kwani ana kesi ambayo akishindwa hatakuwa nafasi ya 'kulazimisha' CUF ilipe gharama za kesi, nadhani hili CUF ndiyo labda limewaogopesha.
Vilevile, katika maelezo ya Mh Wilfred sijaona mahali popote akiutaka uongozi wa CUF uanzishe uchunguzi rasmi wa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za chama dhidi yake. Kitendo cha kulifumbia macho suala hilo inaonesha weakness kubwa katika uwajibikaji wake aidha na yeye 'anafunika kombe mwanaharamu apite' na kuhakikisha kuwa anakaa chini ya miguu ya wakuu wake ili yaishe.
Kwa hapo juu naona nimeelewa tofauti. Hakukataa wala hapingi kupigwa chini ila utaratibu uliotumika. Naamini alistahiri kupewa walau taarifa mapema ili kuacha hilo swali la kwa nini wanamfanyia surprise. Hilo nadhani ni tatizo kubwa sana. Kwa sababu kama angekuwa ameelezwa toka mwanzo basi kusingekuwa na sababu ya yeye kushangaa! Kwa ngazi aliyokuwa nayo si vizuri kuacha kumweleza hata kama kitu hicho ni kibaya kwake. Na hili ndilo tatizo la viongozi wetu. Yaani hawana ubavu wa kumwambia mwenzao anapokosea. Na ndiyo maana huweza kuacha kufikiria kuwa hapo kulikuwa na mizengwe fulani (conspiracy).
Ni bahati mbaya sana kwamba TLP hawana ruzuku ya kutosha kum-bailout, lakini kama angejiunga huko angetengeneza timu nzuri sana na Lyatonga!
Kwa upande mwingine, ni haki ruzuku ya chama (Pesa ya walipakodi) kutumika kulipia kesi binafsi za wanachama? Kulipa pensheni za wanachama wastaafu kama Mloo alivyokuwa akilipwa 500,000/= kwa mwezi? Just curious!
Hivi huyu Mheshimiwa si tulitangaziwa (na Omutwale) kua atajiunga na jamvi letu hili jana mchana imekuaje? yumo humu?
Thubutu, Lyatonga yupi?Huyu mzee wa Kiraracha? Hapo umempoteza Lwakatare kwa ushauri huo.Ni bahati mbaya sana kwamba TLP hawana ruzuku ya kutosha kum-bailout, lakini kama angejiunga huko angetengeneza timu nzuri sana na Lyatonga!
Kwa upande mwingine, ni haki ruzuku ya chama (Pesa ya walipakodi) kutumika kulipia kesi binafsi za wanachama? Kulipa pensheni za wanachama wastaafu kama Mloo alivyokuwa akilipwa 500,000/= kwa mwezi? Just curious!