Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Pamoja na kwamba sioni sababu ya ku-question nia yake ambayo ameitimiza kwa kuhamia chama kingine, naona haikuwa vyema kwake kusema alikuwa akilipwa kiasi gani na CUF. Masuala ya mshahara ni makubaliano yake na chama alichokuwepo. Na ni masualaya kibinafsi sana. Kinachotakiwa ni sababu za kuhama, na kuhamia CHADEMA, nia ya kuendeleza upinzani wa kidemokrasia na mikakati aliyonayo ya kisiasa baada ya kuondoka CUF.

Kuweza kupata wanachama wa CUF wenye nia ya kuhama nae ni hatua muhimu sana pia. Kwani anaingiza mtaji mpya kwenye chama chake kipya. Ila anatakiwa kuahidi kushirikiana na chama chake kipya na kujifunza imani zao, malengo yao na kupania kukiimarisha zaidi kwa kushirikiana na wenzake aliowakuta huko.

Siasa za upinzani Tanzania ni ngumu sana. Inabidi tumuelewe tu ndugu yetu huyo kwamba amebidi kuhama na zaidi ametumia haki yake kufanya hivyo. Tuheshimu maamuzi hayo, kwani kufanya hivyo ni kumtendea haki. Hakuna haja ya mtu kubaki sehemu moja ambayo una uhakika kuwa hutaweza kutoa mchango wowote kwa haki, na uhuru. Hasa baada ya kutokea yaliyotokea.

Kila binadamu hupenda challenges. Bila challenges maisha yanakuwa boring. Hivyo kuhama kwa Lwakatare inaweza kuwa ni challenge kwake, ni kwa manufaa yake kabla hayajawa manufaa kwa mwingine yeyote.

Jamaa mshamba haelewi hata issue nzima ya confidentiality na amicable parting, kashazoea kuachana na zogo zogo kama mke/mme mwenye wivu.

Yaani unaweza kumu asses mtu kwa mitihani midogo tu akakupa picha ya personality yake nzima, kama Pinda alivyoenda kutoa acceptance speech ya u PM bungeni huku kavaa suti na ki wife beater, unaona kazi tunayo kama Waziri Mkuu ndiye huyu, watu ooh mpe muda, wengine tukaona plae pale haya maboya, tena ya uchina.

Na huyu Lwakatare egotistic narcissist anayetafuta chati na ulaji wa chap chap si mwanasiasa anayeelewa siasa za Tanzania. Mwanasiasa aliyekomaa anayeelewa siasa za Tanzania ni aibu kujinadi kwa wazi hivyo, essentially kashajitangaza kwamba yeye ni wa chee sana na ana matatizo katika somo zima la PR.

Afadhali mara mia hata Zitto anajua principle ya pricelessness ya ideas na leadership mpaka kusema "I have no price tag" hata kama anayo price it is reassuring kumsikia mtu at least anajua kwamba anatakiwa asiwe na price.Huyu mshamba kashatutajia hela yake ndogo kuliko some belvedere shoes.
 
IMGP2144 i.jpg
Wananchi bila kujali ukali wa jua wakisikiliza hotuba ya Lwatare

IMGP2145 i.jpg
Lwakatare akihutubia.

IMGP2148 i.jpg
Lwakatare akipongezwa na Profesor Baregu baada ya hotuba

IMGP2149 i.jpg
David Kalikawe, mmoja wa waanzilishi wa Chadema Kagera na mmoja wa wadhamini 200 wa Chadema akihutubia.

IMGP2150 i.jpg
Christopher Ngaiza, akitoa salaam na nasaha kwa ana Bukoba.

IMGP2151 i.jpg
Profesor Baregu akisalimia mkutano.

IMGP2154 i.jpg
Katibu wa Chadema mkoa wa Kagera Bi Conchesta akinena jambo na Dr Slaa wakati akimtambulisha.

IMGP2155 i.jpg
Bi Conchesta, akionyesha fomu maalumu anayotakiwa kuijaza mwanachama mpya ndugu Lwakatare.

IMGP2156 i.jpg
Katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa akimkabidhi fomu maalum ya maombi ya wanachama Mh Lwakatare.

IMGP2157 i.jpg
Lwakatare akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa fomu
 
Ebo! Fujo zote hizi kumbe mtu hata fomu za maombi ya uanachama hajajaza! Mimi nilifikiria kuwa wakuu walikuwa wanaenda kumkabidhi kadi baada ya kukubaliwa maombi yake ya uanachama! Iko kazi.

P.S. Hivi hizo fomu MAALUM za maombi zikoje? Zina tofauti gani za zile za kawaida?

Amandla.......
 
Last edited:
IMGP2158 i.jpg
Lwakatare akipongezwa.

IMGP2159 i.jpg
Lwakatare akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa Chadema.

IMGP2160 i.jpg

IMGP2162 i.jpg
Lwakatare akikabidhiwa rasmi katiba ya Chama cha chadema

IMGP2163 i.jpg
Lwakatare akikabidhiwa rasmi katiba ya Chama cha chadema

IMGP2164 i.jpg

IMGP2165 i.jpg
Lwakatare akikabidhiwa bendera ya chama cha chadema na wazee na viongozi wa chama mkoa wa Kagera.

IMGP2166 i.jpg
Profesor Baregu akimkabidhi kalamu kama ishara ya kumukaribisha kazini moja kwa moja. Lwakatare alikuwa mwanafunzi wake Chuo kikuu Dar es salaam

IMGP2167 i.jpg
Timu ya viongozi Chadema na mwanachama mpya Lwakatare
 

Attachments

  • IMGP2161 i.jpg
    IMGP2161 i.jpg
    31.5 KB · Views: 30
Ebo! Fujo zote hizi kumb mtu hata fomu za maombi ya uanachama hajajaza! Mimi nilifikiria kuwa wakuu walikuwa wanaenda kumkabidhi kadi baada ya kukubaliwa maombi yake ya uanachama! Iko kazi.

P.S. Hivi hizo fomu MAALUM za maombi zikoje? Zina tofauti gani za zile za kawaida?

Amandla.......
Wasiliana na viongozi wa Chadema kama na wewe unahitaji kujiunga kuwa mwanachama. Watakupa maelekezo😀
 
Wasiliana na viongozi wa Chadema kama na wewe unahitaji kujiunga kuwa mwanachama. Watakupa maelekezo😀

Sina mpango. Wasiwasi wangu ni kuwa ni safari ndefu kati ya mkono na kinywa. Tonge lisiishie njiani! Mtamshangiliaje mtu ambae hata hajawa mwanachama?

Amandla......
 
Tuone ashinde huo ubunge hapo ,maana naona kuna ulimbukeni si mdogo.Na kwa wenyeji wa hapo ndio kipimo chao ,kama chama ni mtu na kama walikuwa ni MaCUF menyu basi ipo kazi pevu,ila kama matarajio yao waliyaweka kwa Lwakatare basi wanaweza kumchagua sioni ubaya wowote ule muhimu ni kuipunguzia kasi CCM.
 
IMGP2168 i.jpg
Aliyekuwa katibu wa mkoa CUF akitoa nasaha zake.

IMGP2171 i.jpg
Aliyekuwa katibu wa mkoa CUF akikabidhi kadi ya uanachama CUF kama ishara ya kujivua kutoka chama hicho.

IMGP2172 i.jpg
Dr Slaa akimuasa mwanachama mpya kabla ya kumkabidhi kadi ya uanachama wa Chadema.

IMGP2173 i.jpg
Dr Slaa akimkabidhi kadi ya uanachama wa Chadema aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha CUF Kagera.

IMGP2175 i.jpg
Katibu mkuu wa Chama cha Chadema akihutubia mkutano katika viwanja vya Uhuru platform mjini Bukoba.

IMGP2176 i.jpg
"Nani anakubali Mh. Lwakatare ahamie Chadema na atakuwa tayari kufuatana naye?" Waliokuwa tayari mikono ilikwenda juu!


Mpaka hapa nimefikia mwisho wa session ya picha.
Nitawaletea dondoo ya machache yaliyozungumzwa mbele ya wananchi
 
I love CHADEMA..... wanakwenda kisasa zaidi. Kuweza kuajiri watu 24/7 kushinda mtandaoni na kufanya spinning.. is not a joke!

Omutwale hongera amakweli unakula kwa jasho lako, maana kwa propaganda! utadhani ulipitia pale Kivukoni?
Watu wengine wa ajabu sana. Is this spinning?
Tumeajiliwa na Chadema kuleta spinning?
ili iweje?
Si jionee mwenyewe?
 
Hiyo fomu alijaza saa ngapi kabla hajakabidhiwa kadi ya uanachama? Au ndiyo maana iliitwa MAALUM maana iliisha jazwa na yeye alitakiwa kuisaini tu? Tuwe serious kidogo na hizi siasa zetu.

Amandla......
 
Yaliyojili kwa ufupi:
*Mkutano ulifunguliwa kwa sala ya viongozi wa madhebu mawili. Akianza muislamu na kisha mkristo.

*Shughuli zote ziliendeshwa na M/C ambaye ni mwanamke nimeweza kulijua jina lake moja tu anaitwa Susan na anatoka makao makuu ya Chadema Dar.

*Kisha walikaribishwa viongozi wa vuama vingine vya siasa waliohudhlia na wakatoa salaam zao. Viongozi hawa walitoka vyama vya tlp,na nccr Bukoba.

*Kisha alipewa nafasi ya kuhutubia Katibu wa CUF wilaya ya Muleba ambaye alimsifia Lwakatare kwa uongozi kwa jinsi alivyokuwa akimfahamu kiuongozi.
Na alisema alikuwa safari Musoma ila ilibidi arudi haraka Bukoba baada ya kusikia hafla ya jana.
Alitoa nasaha zake jinsi upinzani ulivyo na safari ndefu ya kuhakikisha dhuruma inaondolewa maana mdhurumiwa na anayedhurumu wote wana hukumu.
Alieleza changamoto zinazotaka viongozi walio serious ili kukiondoa Sisi Maf... madarakani. Na alisema hii inahitaji ushirikiano katika upinzani. Alisikitikia ubabaishaji katika baadhi ya vyama.
Hata hivyo alitangaza pia kujivua uanachama wa CUF pale pale.
*Kisha alipewa nafsi ya kuhutubia katibu mkuu wa CUF wa mkoa wa Kagera ambaye alitoa hotuja iliyokuwa imejaa nasaha kwa wana kafu na watu walio katika kambi ya upinzani.
alieleza jinsi alivyotembelea maeneo mengi katika mkoa huu na hali za wananchi zilikuwa za hali ya chini kiasi cha kutisha.
Alishangaa kutowaona baadhi ya viongozi wa kafu mkutanoni jambo aliloliona kama usaliti maana wao ndio walimshauri pamoja na wananchi kwamba ajiondoe kafu.
 
Aliyozungumza Lwakatare kwa ufupi:
*Alianza kwa slogan ya Haki............ na akasema hii slogan anaipenda kiasi kwamba hawezi kuiacha maana ina maana kubwa katika maisha yake kwani yeye ni mtu anayependa haki.
*Alisema pamoja na kuamua kujitoa kafu hakuwa na mpango wa kutoka katika Chama. Lakini anasema yeye kama kiongozi alipowaeleza viongozi wa Kafu wilaya pamoja na wapiga kura wa Bukoba mjini yaliyojiri kiasi ambacho ilimlazimu kuvua nyadhifa alizokuwa nazo, (Ikumbukwe kuwa nyadhifa nyingine alizojivua zilikuwa ni za kuwakilisha mkoa wa Kagera katika Vikao vya juu vya chama).
Anasema wananchi waliokuwepo pamoja na viongozi wa Kafu wa wilaya kwa pamoja walimutaka atoke katika chama cha Kafu.
Alipowauliza je wanataka aende chama gani? Je wanahitaji aende sisi Maf.... au iweje huku akitaka wanaotaka aende Sisi Maf........ wanyoshe mikono, ni watu wawili tu katika mkutano walionyosha mikono.
Na aliwauliza wengine waliobaki sasa nyie mliobaki mnataka nitoke je mnataka niende chama gani? Sauti kubwa ikasikika kuwa Chadema.
Akaomba wanaotaka aende Chadema wanyoshe mikono na mkutano karibu wote ukanyosha mikono.
 
*Anasema alipata kadi ya kafu mwaka 91 katika tawi la Kibeta wakati huo akiwa mtumishi wa serikali, na hata famila yake ililidhia. Na aliona vigumu kuwakubalia watu hadi awasiliane na famila yake.
*Anasema alipata maswali mengi na kikwazo kikubwa kilikuwa kwa baba yake mzazi ambaye alihofia hatima ya usalama wa mwanae kisiasa na hata katika maisha ya kisiasa.
Baada ya kupata ushauri toka kwa wazee fulani alikubaliana na utashi wa wananchi wa Bukoba mjini kwamba anaweza kuhama.
*Alisisitiza aliamua kuchukua hatua zote hizo maana yeye si mwanasiasa sawa na wale wanasiasa ambao uamua tu kwenda Maelezo na kuita waandishi wa habari kutangaza kuamia chama kingine bila kutafakari. Wala yeye hakushauriwa na viongozi wa Chadema kuhamia huko, na si kweli kwamba amepewa rushwa kama wengine wanavyovumisha, maana yeye si mla rushwa. Bali alitaka kuheshimu matakwa ya wapiga kura wake.
Alisisitiza kuwa yeye hakuumbwa kunyamazia kitu kibaya kinapotokea na huwa tayari kujitoa kukieleza wazi maana hiyo ndivyo alivyo katika maisha yake.
*Anasema alikuwa anapata mshahara wa sh. laki 3 alipokuwa kafu kama kaimu katibu mkuu, na anasema uamuzi wa kumuondoa katika wadhifa kwa ghafla ulimfanya afikiri kuanza ujasiliamali na alianza kuuza Matikiti maji na Chips kuku. Na amebainisha kwamba kwa mwezi kwa kuuza matikiti maji alipata faida ya sh. laki 2 na chips laki 3.
*Alisema kwa sasa tunahitaji kujenga misingi ya vyama na si ushabiki wa vyama na kuwaasa wanachi wa Bukoba kulielewa hilo.
*Aliomba iwekwe detector ya kubaini wale watu wanaokwenda katika vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, dini au ukabila. Maana hayo uua vyama badala ya kuvijenga.
 
*Anasema alipata kadi ya kafu mwaka 91 katika tawi la Kibeta wakati huo akiwa mtumishi wa serikali, na hata famila yake ililidhia. Na aliona vigumu kuwakubalia watu hadi awasiliane na famila yake.
*Anasema alipata maswali mengi na kikwazo kikubwa kilikuwa kwa baba yake mzazi ambaye alihofia hatima ya usalama wa mwanae kisiasa na hata katika maisha ya kisiasa.
Baada ya kupata ushauri toka kwa wazee fulani alikubaliana na utashi wa wananchi wa Bukoba mjini kwamba anaweza kuhama.
*Alisisitiza aliamua kuchukua hatua zote hizo maana yeye si mwanasiasa sawa na wale wanasiasa ambao uamua tu kwenda Maelezo na kuita waandishi wa habari kutangaza kuamia chama kingine bila kutafakari. Wala yeye hakushauriwa na viongozi wa Chadema kuhamia huko, na si kweli kwamba amepewa rushwa kama wengine wanavyovumisha, maana yeye si mla rushwa. Bali alitaka kuheshimu matakwa ya wapiga kura wake.
Alisisitiza kuwa yeye hakuumbwa kunyamazia kitu kibaya kinapotokea na huwa tayari kujitoa kukieleza wazi maana hiyo ndivyo alivyo katika maisha yake.
*Anasema alikuwa anapata mshahara wa sh. laki 3 alipokuwa kafu kama kaimu katibu mkuu, na anasema uamuzi wa kumuondoa katika wadhifa kwa ghafla ulimfanya afikiri kuanza ujasiliamali na alianza kuuza Matikiti maji na Chips kuku. Na amebainisha kwamba kwa mwezi kwa kuuza matikiti maji alipata faida ya sh. laki 2 na chips laki 3.
*Alisema kwa sasa tunahitaji kujenga misingi ya vyama na si ushabiki wa vyama na kuwaasa wanachi wa Bukoba kulielewa hilo.
*Aliomba iwekwe detector ya kubaini wale watu wanaokwenda katika vyama vya siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, dini au ukabila. Maana hayo uua vyama badala ya kuvijenga.

KWENYE barua zake alizoweka hapa JF alionekana anatafuta mtu wa kumpa pesa za wakili na kumsaidia gari nk.Chadema lazima watakuwa wamekubali kuchukua gharama zake.alikuwa kama anajitembeza yaani kibaya chajitembeza na kizuri cha jiuza.kwani barua zile za chama chake kuziweka kwenye mtandao ni kinyume na maadili ya uongozi.wenzake CUF hawajatoa siri zake
 
*Lakini anasema aliipenda sana kafu na si kweli kwamba kafu likuwa na misingi ya dini kama ilivyokuwa inaenezwa, na aliifahamu hivyo tangu 1991 alipojiunga nayo ikiwa CCW na hata ilipoungana na KAMAHULU kuzaa kafu.
*Amebeza wale wanaosema yeye ni malaya wa kisiasa akijitetea kuwa Chadema ni chama chake cha pili kwani hajawahi kuwa mwanachama wa chama kingine mbali na kafu.
*Akiasa wana kafu alisema, unaposema unakipenda chama uwe na malengo, na isiwe unasema mchana mimi ni kafu usiku unsema mimi ni Sisi Maf...... Usiwe ndumila kuwili. Ukiona kafu haitimili malengo ya kisiasa kuliko kuvaa ngozi nyingine ni bora uondoke na kwenda kwingine huku akifuatisha msemo wa kihaya ulio na tafsiri ya usife kama kupe ambaye yeye hufa huku ameng'ang'ania juu ya ngozi. Na kuongeza mfano mwingine kwamba kama unasafiri kwenda Dar na njiani Biharamulo gari ikaharibika deaf, huku mkiahidiwa kupata spare toka Dar, ikija gari nyingine nzima na nauli bado unayo panda la sivyo utahadhirika maana hutajua spare italetwa lini nawe utoke porini.
*Anasema alikubariana pia na matakwa ya kwenda chadema kwa sababu aliona the guys are working seriously huku akisema viongozi wa chadema amefanya nao kazi alipokuwa mbunge na wakati huo huo kwa ajili ya uwezo wake katika kuongoza, alichaguliwa kuwa waziri mkuu kivuli na hawa viongozi wa chadema wakiwa mawaziri chini yake. anajua ufanyaji kazi wao na uadilifu wao. Anasema Chadema ni sawa na Real Madrid wao wanawekeza kwa watu ambao ni potential kwa kuchukua stars katika politics kukiendesha chama.
 
KWENYE barua zake alizoweka hapa JF alionekana anatafuta mtu wa kumpa pesa za wakili na kumsaidia gari nk.Chadema lazima watakuwa wamekubali kuchukua gharama zake.alikuwa kama anajitembeza yaani kibaya chajitembeza na kizuri cha jiuza.kwani barua zile za chama chake kuziweka kwenye mtandao ni kinyume na maadili ya uongozi.wenzake CUF hawajatoa siri zake
Wait a minute plz Kandambili, usianze kulialia 😀
 
Duh..huyo jamaa aliyepiga sun glasses ndo 'security detail' ya Chadema?
 
*Amekili kuwa yeye ni muumini wa ushirikiano katika vyama vya upinzani, na amewahi kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa vyama vinne vya upinzani ulioundwa ili kutafuata namna vyama vinavyoweza kushirikiana katika masuala ya uchaguzi na siri anayo kwa nini haikuwezekana.
*Amesema si lazima tu yeye peke yake ndiye awe mgombe katika jimbo hili la Bukoba mjini maana hajui kama chake kitamteua wakati ukifika. Lakini anasema yuko tayari kushirikiana na mgombea yeyote na kumpigia kampeni kama atakuwa anakubalika hata kama atakuwa ametoka katika chama chake cha zamani Kafu.
*Na kwa sababu hiyo ameamua kujikita hapa Bukoba na kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa upinzani unashinda na kuchukua council na hatimaye ubunge kwa mbunge yeyote wa upinzani anayekubali. Ameapa kufanya kila jitihada kuona anatimiza aima yake hiyo.
*Amesema sasa anahitaji wanachama walio hai katika chama na si kundi la ushabiki tu. Hao wawe na kadi kadi zakupigia kura wafahamike waliko, waorodheshwe katika daftari la chama, wajulikame simu zao au hata email zao.
 
*Amekili kuipenda sana kafu hadi kumiliki kadi namba 149 ya mwaka 1991lakini anasema anaipenda nchi yake sana kuliko vyama vya siasa.
*Amesema ameamua kuwa muandishi na kuna kitabu anachoandika ingawa kakili anahitaji msaada ili akichapishe, ambapo alipata ahadi ya sh laki 3 toka kwa Dr Slaa, laki 2 toka kwa Baregu, 250,000 toka Balozi Ngaiza nk nk nk.
*Amesema mipango yake anayofikiria kuianzisha sasa ni kujenga chuo cha Technologia hapa Bukoba, ili kuhakikisha vijana wengi wanapata mafunzo ya namna ya kujiajili mara wamalizapo shule.
*Katangaza kuwakutakuwa na party ya kumpongeza itakayokuwa katika hotel ya Spice Bukoba.
 
Back
Top Bottom