Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Lwekatare wa CUF kuhamia CHADEMA

Waungwana kwanza niwaulize na kuwakumbusha vipi CUF iko Imara kwani sio chama cha Mrema kile we go by the book .
Nitawarudisha nyuma kwenye historia.
CUF haitetereki kwa wanasiasa wenye tamaa ya kuhongwa ukiwa na njaa ya vyeo tuna ku dump na kukutizama msimamo wako.
Rudi Kwenye Historia ukileta mchezo utaekwa Pembeni hata ukawa na cheo gani.
Tulianza na Founder chairman, James Mapalala , alibebwa juu kwa juu na wananchi kuanzia Sikonge Tabora mpaka PEmba na alipoanza kurubuniwa na CCM aliwekwa Pembeni.
Nyaruba na kundi lao waliojaribu kuigawa CUF ionekane CUF ya Bara na Visiwani waliekwa Pembeni.
Naweza kuwatajia majina mengi ya waliotamba ndani ya CUF na walipotaka kuleta ufisadi waliekwa Pembeni.
Hiza Tambwe amemaliza kisiasa amebaki kutumiliwa na CCM
Shaib Akwilombe yuko wapi amebaki kutumiliwa na Chadema
Lwakatare alikua ndio Msemaji na powerful figure kwa Upande wa Bara ila alipo onesha udhaifu wake aliwekwa kwenye duara na alijistukia na ndio akatafuta njia ya Kukimbilia.
Wako Wengi ambao wataekwa Pembeni pindi wakileta usalitu wanasema wana ngangari hawarudi nyuma bali kusonga mbele.
CUF HAKUNA BIASHARA YA UFISADI CUF HAINUNUI WANASIASA.

Nitawakumbusha wana jamii si Munamkumbuka Masumbuko Lamwai na DR Amani Kaborou wa Kigoma si wamebaki Historia tu Mpinzani wa Kweli hagombei vyeo bali anagombea demokrasia ya kweli ukiwa na njaa ya vyeo au njaa ya Pesa ukitaka Ufisadi nenda CCM utapokewa kwa mikono miwili.
 
Wewe unena sahihi. Lwakatare tatizo lake ni njaa na kaenda Chadema kuganga njaa yake tu.

CUF haitayumba kwa kuondokewa na wanasiasa uchwara kama Lwakatare if anything ndio itakuwa imara zaidi sasa kimeingia kifaa kingine Joram huyo ni kata funua.

Ndegeres!!!!!!
 
Mkubali msikubali CUF ina matatizo!.. na hayakuanza jana.. Kiashirio kikubwa cha chama ni kura za wananchi... CUF inazidi kupoteza majimbo yake bara na sasa hivi wako mbioni kupoteza mengine kama sio pekee wanakotegemea toka bara.

CUF ya mwaka 2000 sii CUF ya leo hii na ajabu kubwa hata Lipumba wa mwaka 2000 sii huyu tena. Kifupi CUF imeishiwa hoja na watu wengi waliokuwa chama hicho miaka ya nyuma kujia 2000 wakipandisha bendera za chama majumbani mwao, wameziondoa kwa sababu chama hiki mwaka hadi mwaka kinapoiteza malengo yake..Kuondoka kwa Mapalala CUF ilijenga ngome yake zanzibar na kupoteza kabisa historia ya chama kwamba kilianzishwa bara.. Ni Watanzania wachache sana wanafahamu kwamba CUF ni chama cha Kitaifa, na kutokana na mabadiliko mengi ndio maana unasikia watu wakisema CUF ni chama cha Wapemba..Haya ni matokeo ya Uongozi uliopo na sii wale waliotoka.

Hivyo kufukuza watu wakati mnakijenga chama kuingiza tofauti baina ya watu, ardhi na hata maslahi inayosimamia.ni kubomoa chama wala sii kujenga hata kidogo.. Jamani nakataa katakata kuwa huwezi kuita ni maendeleo ya chama..CUF wanashindwa hata kusimama kulaani UFISADI unaoendelea leo, kila siku utawasikia wakisemma tusome Historia! jamani Ufisadi upo leo hii , mnataka sisi wananchi turudi nyuma kutazama kitu gani?..

Lini mmesikia Maalim Sief au Lipumba wakilaani Ufisadi? lini umesikia viongozi wa CUF wakizungumzia Ubinafsishaji mbaya wa vyanzo vya uchumi wetu, matumizi mabaya ya mashirika ya Umma, misafara isiyokwisha, rada, Richmond, madini na kadhalika kama sii maswala ya Muungano na haki za Wazanzibar kuwa hoja kubwa ya kusimama kwa chama hicho!.. Kweli hii ndio CUF tunayoijua miaka ya 2000?..

Acheni jamani Lwakatare ana mambo yake lakini msitake kabisa kuudanganya Umma kwamba CUF ni chama kimesimama imara zaidi wakati mnajua fika kuna matatizo makubwa hasa ktk Uongozi wa juu. Lipumba na Maalim Seif ni mzigo kwa chama hicho mkubali msikubali wanachojali wao ni posho na marupurupu ya Uongozi.. badala ya viongozi kugombania haki za wananchi mnagombania ruzuku na matumizi yenu ambao mnashindwa hata kuyaweka hadharani kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu..

Kama kweli Lwakatare alitumia vibaya fedha na mwenye tamaa ya fedha, hakuna njia bora zaidi ya kufikisha swala hili kwa wanachama na kuwaonyesha mahesabu ya mkaguzi yanavyoonyesha, badala yake tunakaa hapa tukibishana kutokana na taarifa ambazo hazina uhakika.. Lipumba amekana, viongozi wa CUF wamekana kuwepo na matumizi mabaya... sasa hawa wanaficha nini haswa kusema ukweli kwa wanachama na kuwapa report nzima ya matumizi..
 
Mkandara si kweli kuwa Lipumba na Seif hawajawahi kulaani ufisadi.

Hebu peruzi hapo chini kidogo,

Lipumba: Ufisadi ni matokeo ya utawala...

2008-08-29 09:31:45
Na Dunstan Bahai
Matukio ya rushwa, ufisadi na nyufa mbalimbali zilizojitokeza kwenye Muungano, ni matokeo ya kuwa na viongozi wasio waadilifu, hekima na busara.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, kwenye kongamano lililoandaliwa na chama hicho jijini Dar es Salaam likiwa na lengo la kujadili ukosefu wa uongozi na hatma ya Tanzania.

Alisema uongozi usio adilifu na usio na dira wala kujiamini, hujenga matabaka kama ya mitandao.

Alisema matabaka hayo ndiyo yanayojikuta yakiishikilia nchi katika nyadhifa mbalimbali na hata mmoja wao akifanya madudu ni vigumu kumuengua, kwani kwa kufanya hivyo ni kukiuka makubaliano yaliyomo kwenye mtandao huo.

Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, wanamtandao hao ndiyo chanzo cha matokeo mabaya ya utawala wowote duniani kwani maamuzi yao hawawashirikishi wananchi.

``Katika nchi inayokabiliwa na dimbwi la umaskini, na inataka kujenga demokrasia ya kweli, uadilifu ndiyo unapaswa kuwa msingi wa siasa, msingi wa maongozi ya siasa.

``Kuzungumzia uongozi na uadilifu katika siasa si jambo jepesi. Hisia na mitazamo ya watu wa kawaida kuhusiana na siasa, imekuwa ya kuihusisha fani hiyo na tamaa, ubinafsi, uroho, unafiki, ulaghai, upotovu, uovu, fitina, hiyana na hata hujuma. Tena si watu wa kawaida tu bali hata baadhi ya wasomi wetu wanaonekana kuiona hivyo,`` alisema Profesa Lipumba.

Alisema kutokana na hali hiyo, imechukua muda Watanzania kuamini kama mabadiliko yanawezekana hapa nchini ingawa alisema sasa wameamka na kuunga mkono jitihada za kuwepo kwa mabadiliko hayo.Profesa Lipumba, aliainisha mabadiliko 11 ambayo alidai Watanzania wanayahitaji.

Mabadiliko hayo ni yale yatakayowapa uongozi wa namna bora ya kutumia neema ya rasilimali zilizopo, yatakayomhakikishia kila Mtanzania anamiliki alau milo mitatu iliyotimia kwa siku na kuongeza kipato chake kupitia kazi halali na jasho lake na kuhakikisha gharama za maisha hazipandi kiholela
Tuikomboe Tanzania kutoka ufisadi wa CCM – Prof. Lipumbahttp://hakinaumma.wordpress.com/2008/10/18/tuikombe-tanzania-kutoka-ufisadi-waa-ccm/http://hakinaumma.wordpress.com/2008/10/18/tuikombe-tanzania-kutoka-ufisadi-waa-ccm/
18 10 2008
Hotuba ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, Oktoba 9, 2008 na kutanguliwa na maandamano ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete awataje mafisadi na awapeleke mahakamani.
Waheshimiwa Wananchi,
Awali ya yote nawashukuru kwa kujitokeza kwa wingi, pamoja na hali ngumu ya maisha ya wananchi wa Tanzania kwa geuzwa kuwa ndege ambapo kila kukicha hutoka kutafuta riziki zao, kwani hakuna mwenye uhakika na riziki ya kesho ataipata wapi, lakini hata hivyo mmejitokeza kwa wingi, nami sina budi kuwashukuru.
Maandamano kama haya siku za nyuma yalikuwa yanaekewa vizingiti na kuzuiwa na jeshi la Polisi, mnamo Januari 27, 2001 ambapo tulitaka kufanya maandamano ya amani matokeo yake watu waliuliwa Zanzibar na kwa Dar es Salaam watu walipigwa na vijana wawili waliuliwa, hivyo naamini kuwa mambo kama hayo hayatatokea tena hapa nchini.
Napenda kuliasa Jeshi la Polisi liwe linafuata taratibu na sheria, pia nachukua fursa hii kumshukuru Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, halikadhalika na askari wote waandamizi kwa ushirikiano walioutoa kufanikisha maandamano haya.
Waheshimiwa wananchi, katika miongoni mwa waandamanaji wa siku yetu ya leo yupo Mzee wetu mmoja amebeba bango lenye ujumbe kuwa ‘CCM SI TANU’, nami nakubaliana na ujumbe wa mzee huyu kwani katika ahadi kumi za chama cha TANU, mojawapo ya ahadi hizo ilisema kwamba “Rushwa ni adui wa haki, sitopokea rushwa wala kutoa rushwa”.
Leo hii Chama kilichotokana na TANU yaani CCM, badala ya kupambana na rushwa kimeamua kuikumbatia, kimekuwa chama cha Mafisadi, na kibaya zaidi Waheshimiwa wananchi, si kwamba ufisadi na rushwa ni adui wa haki tu lakini pia ni adui wa maendeleo.

http://hakinaumma.wordpress.com/2008/10/18/tuikombe-tanzania-kutoka-ufisadi-waa-ccm/

Lipumba azidi kulia na ufisadi

na Asha Bani, Kilwa
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, ameitaka Serikali kuchukua hatua dhidi ya wale wote waliohusika kuliingiza taifa katika mikataba yenye utata.
Amesema serikali inapaswa kuwachukulia hatua watendaji waliohusika katika utiaji sahihi mikataba ya IPTL, Mradi wa kufufua umeme wa dharura ( Richmond ), Meremeta na wale waliohusika katika ununuzi wa rada iliyoligharimu taifa mabilioni ya fedha.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jana katika Kata ya Kipatimo Wilaya ya Kilwa, alisema Serikali inatakiwa kuwachukulia hatua viongozi wote waliohusika na ulafi wa fedha, rushwa na kujilimbikizia mali.
Profesa Lipumba alisema kuwa ulafi wa viongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu na Nne ndiyo kiini cha Watanzania wengi kuwa maskini.
Alisema kama taifa lisingekuwa na mafisadi ambao sasa wameanza kupelekwa mahakamani, taifa lisingekuwa katika hali mbaya kama ilivyokuwa kwa sasa ambapo baadhi ya wanachi wanaishi kwa mlo mmoja kwa siku.
Profesa Lipumba aliishauri serikali kuchukua hatua zinazoeleweka badala ya kufanya viini macho kwa kuwapeleka mahakamani na kisha kuwachia waliohusika kulifikisha taifa katika hali lililo nayo sasa kwa madai kuwa hakuna ushahidi.
“Ni nani asiyejua kuwa kuna mafisadi hadi leo wanapeta na pengine wakawa wameshatoroka nchini kutokana na serikali kutokuwa makini, kinachotakiwa ni kuwakamata waliohusika na kama kuna mpango wa kuwapeleka mahakamani lakini taratibu hazijakamilika, inatakiwa kuzuia hati zao za kusafiria,” alisema Profesa Lipumba.
Akitoa mfano alisema, kuzubaa na kutokuwa makini kwa serikali kumesababisha wakala wa ununuzi wa rada, Salesh Visirani, kutoroka nchini baada ya kuchukua rushwa ya dola za kimarekani bilioni 12 ambapo hadi leo serikali imekaa kimya bila ya kufuatilia sakata hilo .

juu
 
Mmmmhhh alipokuwa kafu alikuwa kiongozi maahili na amekwenda chadema kawa ovyo.
Wadanganyika bwana! ngoja basi tuone mwisho wa yote.
Hivi mnasemaje kuhusu Amani? Mnasemaje kuhusu wale wote waliokwenda sisim wakina wasira? na leo ni wabunge? Hawa je nao walifulia?
 
Lwakatare kashindwa kusema na njaa yake. Kazi ya wito na mshahara wa 300,000 havikumtosha anatafuta short cut ataangukia pua na huko vile vile

Masatu..ukisoma vizuri hivyo viambatanishi utagundua mambo ma 4
1. Anahusishwa na ufisadi (ubadhirifu) ndani ya CUF tuhuma ambazo hajazijibu.

2. Anapendekeza sana kama waasisi (akiwemo yeye) wa enziwe

3. Anasema kama anaishi kwa kubangaiza kuuza Chipisi kule DSM

4. Ana kesi mahakamani ambayo kama akionekana anahatia anaweza kufilisiwa..alimnukuu Kagasheki akiwaambia watu wake kama Lwakatare atauza kila kitu....

Sasa unadhani kwa njaa kama watu kama CHADEMA wangemuacha?.

Duh! amakweli wamesema watu kama muombee adui yako njaa. Lwakatare huyu aliyekuwa mtiifu kwa CUF leo amegeuka hivi!
 
Njaa mbaya sana. Duh!

Si uende huko Chadema kimya kimya?. Najua mwisho wako ni CCM tu, huko unapitia tu.
 
Lwakatare ni mfano halis wa viongozi wengi wa siasa nchini Tanzania wenye uchu wa madaraka na ubinafisi. Hao ni hatari marakumi kuliko hata ugonjwa wa ukoma. Ni dhahiri kwamba kama muheshimiwa Lwakatare atabahatika kuwa waziri siku zijazo basi atakuwa ni miongoni mwa wale mafisadi wakubwa wanaofilisi nchi yetu. Lengo la Lwakatare kujipenyeza katika siasa ni kuja kuwa mwizi wa mali za umma na si kuwatumikia wa lala hoi wa Bongo. Enyi wa bongo wapenda haki, maendeleo na usawa tujihadhari naye mtu huyu na wa mfano wake popote pale walipo, ndani ya vyama vya siasa, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali.
 
Mbona akina Tambwe,Kaborou,Msabaha hamuwaiti njaa kali au kwa sababu kaenda upinzani mwacheni hayo ni maisha yake hayawahusu kabisa
 
Mbona akina Tambwe,Kaborou,Msabaha hamuwaiti njaa kali au kwa sababu kaenda upinzani mwacheni hayo ni maisha yake hayawahusu kabisa

Kama Lwakatare wanasema ni njaa, basi hata wale ambao bado wanaikumbatia CCM pamoja na ufisadi wote huu, ni njaa zao ndo zinawatuma wafanye hivo, kwani kwa hakika hayo mapenzi na ufisadi wote huu yana walakini, walau basi wangeamua kuondoa huo uozo ikabaki kama CCM ya zamani, siyo hii ya wakumbatia ufisadi.

Mpambanaji Lwakatare, wala usigeuke nyuma, endeleza libeneke, kuna siku tu, yatatimia.
 
Nyie endeleeni na kulia lia na UFISADI wa Billion 133 tu.........

Kuna mengi ya maana mnatakiwa mchangie, tuangalieni way forward bandugu tuache kulia lia na mambo yaliyopita.
 
Nyie endeleeni na kulia lia na UFISADI wa Billion 133 tu.........

Kuna mengi ya maana mnatakiwa mchangie, tuangalieni way forward bandugu tuache kulia lia na mambo yaliyopita.

Hivi unafahamu kuna sifuri kama kwenye namba hizo? halafu unamalizia na tuu!
 
Lwakatare ni mfano halis wa viongozi wengi wa siasa nchini Tanzania wenye uchu wa madaraka na ubinafisi. Hao ni hatari marakumi kuliko hata ugonjwa wa ukoma. Ni dhahiri kwamba kama muheshimiwa Lwakatare atabahatika kuwa waziri siku zijazo basi atakuwa ni miongoni mwa wale mafisadi wakubwa wanaofilisi nchi yetu. Lengo la Lwakatare kujipenyeza katika siasa ni kuja kuwa mwizi wa mali za umma na si kuwatumikia wa lala hoi wa Bongo. Enyi wa bongo wapenda haki, maendeleo na usawa tujihadhari naye mtu huyu na wa mfano wake popote pale walipo, ndani ya vyama vya siasa, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali.

Unaweza kuwa na vielelezo na madai y ako hayo; alikuambia; ulisimuliwa; au ni hisia zako au porojo au la basi naona unajaza bandwidth tu au kwa kuwa ni ya bure- waweza kuwa fisadi wa bandwith na hivyo wewe ndiye bahati mbaya hujapata nafasi tu; ungekuwa zaidi ya fisadi PAPA; put substance in
 
Hopefully hawajachukuwa watu kutoka majimbo mengine na kusingizia kama ni wana CUF wa BKB, Maana whata they did kule Busanda ilikuwa ni aibu tupu.

Jamaa wamekwenda kuchukua vijana kutoka all the way TARIME na kuwapeleka Busanda.
Hili sikulijua asante sana Kingwele.
 
Lwakatare endelea kujiimarisha kwenye chama makini kama Chadema.
 
Hili sikulijua asante sana Kingwele.

Hli maarufu sana na wenyewe hawapingi. You know what happened jamaa walikwenda kuwachukua vijana kule Tarime masikini..wakawa wanawalipa pesa ili waende kuzomea kwenye mikutano ya CCM.

Polisi ikawa inaendesha kamata kamata..huwezi kaumini asilimia kubwa ya vijana walioshikwa wakizomea walikuwa wanatoka Tarime.

Ah ndo siisa za kwetu hiki kanda2.
 
CCm ndio wenyewe kwa kusafirisha watu toka sehemu za mbali na jirani chaguzi zinakofanyika bora chadema walichukua Tarime sasa CCM waliwatoa toka Dar es Salaam,wakifanya tabia za kijambazi kabisa
Polisi sasa hivi wanjulikana kwamba lao moja mkuu kuchafua chadema kwa mbinu zozote zile na wala sio jpya kila mtu anafahamu
 
Back
Top Bottom