View attachment 187933
Wakuu,
Kumekuwa na madai ya uongo na kupotosha hapa kwa muda mrefu hapa kuwa Lwakatare ndiye alisimamia ndoa yangu. madai haya yalitolewa kwa mara ya kwanza na Tundu Lissu hadharani na tangu hapo mashabiki wa chama chetu cha CHADEMA wameendelea kuamini kuwa ni kweli Lwakatare alikuwa msimamizi wa ndoa yangu.
Napenda leo kusema rasmi kuwa ndugu Lwakatare hajawahi kuwa msimamizi wa ndoa yangu kwa maana ya patron (best man) wala kwa maana ya kuwa mfadhili mkuu. aliyesimamia ndoa yangu ni kijana mwenzangu anaitwa Prosper Mberwa (pichani kulia kwangu, na mke wake Savera (pichani kushoto kwa mke wangu). hawa wengine waliosimama nasi ni ndugu zetu wanafamilia wa pande zote mbili.
Nalizimika kusema kuwa Lwakatare alichangia harusi yangu kama wengine na alichangia SH. ELFU 30. namshukuru kama wote walionichangia.Picha hii ni authentic,ilipigwa Morogoro Hotel, jioni ya siku ya ndoa yangu tarehe 28 july,2012.
sasa wanaosema Lwakatare ndiye aliyesimamia ndoa yangu wanapotosha umma kwa sababu gani? uongo huu wa nini? maana siyo vizuri watu wanaoaminika na jamii kudanganya. "you can fool some people all the time, and you can fool all the people for some time, but you can not fool all the people all the times". sasa baadhi anzeni kuona kuwa watu hawa mnaowaamini sana wakati mwingine hudanganya.