Lwakatare Hajawahi Kusimamia Ndoa Yangu

Lwakatare Hajawahi Kusimamia Ndoa Yangu

Joseph Ludovick

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
382
Reaction score
506
View attachment 187933

Wakuu,

Kumekuwa na madai ya uongo na kupotosha hapa kwa muda mrefu hapa kuwa Lwakatare ndiye alisimamia ndoa yangu. madai haya yalitolewa kwa mara ya kwanza na Tundu Lissu hadharani na tangu hapo mashabiki wa chama chetu cha CHADEMA wameendelea kuamini kuwa ni kweli Lwakatare alikuwa msimamizi wa ndoa yangu.

Napenda leo kusema rasmi kuwa ndugu Lwakatare hajawahi kuwa msimamizi wa ndoa yangu kwa maana ya patron (best man) wala kwa maana ya kuwa mfadhili mkuu. aliyesimamia ndoa yangu ni kijana mwenzangu anaitwa Prosper Mberwa (pichani kulia kwangu, na mke wake Savera (pichani kushoto kwa mke wangu). hawa wengine waliosimama nasi ni ndugu zetu wanafamilia wa pande zote mbili.

Nalizimika kusema kuwa Lwakatare alichangia harusi yangu kama wengine na alichangia SH. ELFU 30. namshukuru kama wote walionichangia.Picha hii ni authentic,ilipigwa Morogoro Hotel, jioni ya siku ya ndoa yangu tarehe 28 july,2012.

sasa wanaosema Lwakatare ndiye aliyesimamia ndoa yangu wanapotosha umma kwa sababu gani? uongo huu wa nini? maana siyo vizuri watu wanaoaminika na jamii kudanganya. "you can fool some people all the time, and you can fool all the people for some time, but you can not fool all the people all the times". sasa baadhi anzeni kuona kuwa watu hawa mnaowaamini sana wakati mwingine hudanganya.
 
Dogo siku hizi unajipa promo sana, tupia picha nyingine ili kuweka mambo sawa.
 
Hii habari haijawa timely,naomba kuuliza mlikkuwa na uhusiano gani kifamilia na Lwakatare, vp uliwahi kuishi kwake? Je una ugomvi nae?

Sent from my BlackBerry using JamiiForums
 
kwani wewe ndio nani!!??
maana hata sijaelewa kitu.
 
Hii habari haijawa timely,naomba kuuliza mlikkuwa na uhusiano gani kifamilia, vp uliwahi kuishi kwake? Je una ugomvi nae?

Sent from my BlackBerry using JamiiForums

sijawahi kuishi kwake. nimewahi kufika kwake mara mbili tu na mara zote sikuwahi kukaa zaidi ya saa mbili. lakini waongo wa chadema wamekuwa wanadanganya humu kuwa nimewahi kuishi kwake. huyu ndugu ni rafiki yangu tu
 
Tukusaidieje na kama hajawahi kusimamia ndoa yako kuna lipi la ajabu sasa
Kusimamia kwake ndoa yako au kutosimamia kutainua vipi maisha ya mtanzania
Kama ni mambo yenu ya familia au ya chama chenu si muende huko kwenye vikao vya chama chenu myamalize
 
sijawahi kuishi kwake. nimewahi kufika kwake mara mbili tu na mara zote sikuwahi kukaa zaidi ya saa mbili. lakini waongo wa chadema wamekuwa wanaganganya humu kuwa nimewahi kuishi kwake. huyu mni rafiki yangu tu


kama ni rafiki yako kwa nini msiyamalize kirafiki mpaka unafikia kuja kumtangaza huku mpaka na kiasi alichotoa kwenye harusi yako
Hivi unaweza kusimama sehem ukasema huyu ni rafiki yangu wakati unamtangaza mpaka na kiasi alichotoa kwenye harusi yako
 
Kumbe unajua kwamba hao watu wanaaminiwa sana wewe ni kibaraka na utaendelea kutumika sana kwa umasikini wako wa kuomba omba misaada kwa viongozi ni kijana gani unahistoria ya hajabu sana hata haibu hauoni
 
Tukusaidieje na kama hajawahi kusimamia ndoa yako kuna lipi la ajabu sasa
Kusimamia kwake ndoa yako au kutosimamia kutainua vipi maisha ya mtanzania
Kama ni mambo yenu ya familia au ya chama chenu si muende huko kwenye vikao vya chama chenu myamalize

Mr. Rocky,
Leo ndo umeona hili tatizo? mbona uongo kuwa ndiye alisimamia ndoa ulipokuwa ukisemwa humu haukutoa angalizo hili?
 
Mr. Rocky,
Leo ndo umeona hili tatizo? mbona uongo kuwa ndiye alisimamia ndoa ulipokuwa ukisemwa humu haukutoa angalizo hili?


Hatukatai yamesemwa ila haya ni mambo madogo sana ambayo ni wewe ni mhusika kuyamaliza na kama kuna forum kwenye chama chenu ya kuongea haya mngeyamaliza huko huko
Sioni hili linasaidia nini hapa au linamsaidia vipi mtu ambaye hakujui na wala hamjui Lwakatare na issue ya ndoia yako ni mambo binafsi ambayo hayahitaji kuja kuyaanika kwenye forum mpaka na picha zako
 
Back
Top Bottom