Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Wengi wetu tuliamini haya kufanyika though tulikuwa na mashaka kutokana na Serikali ya CCM kuoeteza Credits kabisa katika misingi ya Sheria. Pamoja na kwamba kosa hilo lina Dhamana bado tunaendelea kujiuliza kamteka nani, kwa nini, lini, kapanga nani? Tujuze pia kuhusu Ndugu yetu Ludovick Joseph (Traitor) yeye imekuwaje.

Pongezi nyingi sana kwa jopo la mawakili hawa wa CHADEMA,,,,kweli CHADEMA sasa ni taasisi iliyokamaa na inaweza kuaminiwa na Wananchi 2015. LONG LIVE CHADEMA, LONG LIVE LWAKATARE.

Ta Muganyizi sasa naona Swahiba wako Kagasheki atakufa kwa Pressure,,huku kabanwa na Meya Amani huku Rwakatale, kule Msigwa na meno ya Tembo na Loliondo,,,,mmmmh namhurumia
 
Labda Mwigulu nikuombe utuambie tu utuambie uko tayari kunyea ndoo segerea au? Kwa sababu hapa una mashitaka ya kujibu ktk hili, lazima uuleze umama wa watanzania na umma wa Duniani na umma wa Mbinguni kwamba haya mambo nani alikutuma kuyatengeneza? Hapa utatuletea wengi na bila kukosea haya mambo yanayotokea hivi sasa ktk udini nadhani wewe ndiyo Kinara wa haya mambo, yote yatafunguka
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

Tutakoma, sasa ni kutekwa, kutobolewa macho na kuvutwa na kutolewa kucha kwa kwenda mbele. Kufutwa kwa mashtaka ua Ugaidi kutamfanya Lwakatare na Chadema waone kuwa kumbe kuteka watu na kutoa kucha zao ni vitendo vinavyokubaliwa chini ya sheria...this is a mockery to the law!!!
 
Leo kila mwanacdm anaisifia mahakama eti imetenda haki ila kama maamuzi yangekuwa kinyume na matakwa yenu basi yangemwagika matusi ya ajabu humu.

Tungelalamika kama mahakama ingeshindwa kutenda haki ingefuata matakwa yetu tungeidharau.
 
Hata hao wa Arusha sio Magaidi kama uvyoamini or mnavyoaminishwa...ni serikali yenyewe imejipiga bomu huko ili kuwaadaa wananchi na matatizo yao. Msicheze na serikali inayoongozwa na msanii.

Mkuu, kama hiyo ni kweli........basi Mwenyezi Mungu Atalipa!
 
chris lukosi, bungeni, ritz, marcopolo mko wapi, njooni huku muone, mwiteni na mwigulu
 
'We cannot defeat injustice by becoming more inferior before oppressors but by becoming more superior against oppressors and injustice'. Congratulations commander Lwakatare! Viva Prof Safari, Learned brothers Lisu, Naronyo,Mabere and Kibatara! You have really made it. Up! Up! CDM and all wellwishers of this Nation. I'm warming up to get into the game. Peooooples!
 
hiyo nimeipenda. Mhimili huu wa Judicial unaiweka nchi katika balance. Katika mihili yote ya Dola naona muhili imara at least ni huu na hasa katika mahakama za juu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
 
Mwigulu Lameck Mchemba na CCM yake watakuwa wamepata aibu ya karne, hawafai kuwa viongozi wa watu! Peeeeeeeplezzzz..........., Poweeeeeeeeeeeeeer!
 
mahakama kuu ya tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chadema wilfed lwakatare.

Taarifa kutoka mahakama kuu zinasema mahakama kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa chadema walioko mahakamani na familia ya lwakatare.baadhi ya wafuasi wa chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii lwakatare anawakilishwa na jopo la mawakili nguli watano ambao ni mabere marando,tundu lissu,professor abdallah safari,peter kibatala na naronyo kicheere.


ni ushindi kwa cdm, na ni pigO kwa ccm ( wazee waku fabricate evidence ) aibu kwa mwigulu, nchimbi, lukuvi na magamba mengine katika chama chao cha mapapa( mafisadi ).
 
Back
Top Bottom