Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Lwakatare afutiwa mashtaka ya Ugaidi

Ni aibu ya mwaka kwa Zitto Kabwe.Anajutia kuvujisha barua maana hakujua kama ingeishia hivi sasa waliotaka ajiuzulu walikua na Hoja.Zitto jiuzulu kwa kitendo chako cha kutoa shutuma kwa ofisi ya katibu mkuu wa chama chako upishe uchunguzi huru
Hiyo inaitwa twanga kotekote hadi kwa masalia na maCCm,
kwa hili Zitto alikurupuka, inaweza kuwa kwa makusudi ama bahati mbaya, hii itakuwa aibu kwake na huyo gamba Msacky.
Mahakama imewaumbua watu kibao....

Mkuu Confederate Spy baada ya ZK kupiga kelele kamanda Lissu alitoa msimamo wa CHAMA kuwa LWAKATARE chama hakitamtosa...

Msome LISSU kwenye moja ya Post zake...
By Tundu Lissu
Hivi tunavyoandika humu ndani Wilfred Lwakatare yuko mahabusu ya Segerea kwa sababu amenyimwa dhamana kwa makosa ya kutunga ya ugaidi aliyoshtakiwa nayo. Na kwa wasiomfahamu, basi niseme kwamba hali yake ya kiafya sio nzuri kwa sababu anasumbuliwa sana na ugonjwa wa kisukari. Kwa mazingira aliyo nayo, dhana kwamba alitumwa na maCCM ili aihujumu CHADEMA is a bit far-fetched, to say the least. Kwanza kabisa, angekuwa ametumwa basi angetoa kauli ambazo ni more damaging kwa CHADEMA kuliko ilivyo sasa. Nimeisikiliza sana hiyo video clip na narudia kusema kwamba there's nothing in there inayothibitisha chochote kati ya makosa aliyotuhumiwa nayo. Nothing!!! Na hiyo ni kama tuna-assume kwamba video clip yenyewe inaweza kukubalika.mahakamani Kama ushahidi, kitu ambacho sheria ninayoifahamu mie inaniambia hapana. Pili, angekuwa ametumwa basi video hiyo ingemwonyesha yeye pamoja na 'mtumwa' mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura ili kukamilisha ushahidi wa njama. Kwa hali ilivyo, video clip hiyo haimwonyeshi mla njama mwenzake na kwa hiyo haiwezi ikawa ushahidi wa kuthibitisha njama zozote. Kosa la kula njama linahitaji wakosaji wawili au zaidi. Aidha, kosa la kufanya mkutano wa kigaidi linahitaji 'magaidi' watatu au zaidi, sio wawili Kama inavyodaiwa katika kesi ya Lwakatare. Kama hakuna mkutano wa kigaidi hakuwezi kuwa na njama ya kufanya makosa ya kigaidi na wala hakuwezi kuwa uhamasishaji wa ugaidi, ambayo ni makosa mengine anayotuhumiwa nayo Lwakatare. Tatu, Ludovick na Dennis Msaki walikuwa na mawasiliano makubwa kati yao kwa zaidi ya mwezi mzima kabla ya tarehe 28 Desemba, siku ya kufanyika kwa makosa yanayodaiwa. In brief, katika kipindi hicho, Ludovick aliongea muda mrefu na Msaki kuliko alivyoongea na mie wake mwenyewe!!! Na hayo ni mbali na mawasiliano kati yake na Mwigulu Nchemba na kale ka-payment ka shilingi 50000 kwa M-Pesa wiki mbili baada ya Mwigulu Nchemba kuutangazia ulimwengu kuwa ana video ya mipango ya mauaji ya viongozi wa CHADEMA!!! Kitu kikubwa inachokithibitisha video clip hii, ukiachia njama dhidi ya CHADEMA na viongozi, ni jinsi ambavyo wahusika ni amateurs kwenye mambo hay a!!! Kwa maneno ya Sugu, 'wanahitaji kurudi studio', maana hii picha imeharibika!!!! !!!!
 
Last edited by a moderator:
Ooh god,thank you very much!,the wolves have proved another big failure! Thanks.
 
Ni aibu kwa kiongozi mwandamizi wa chama kushtakiwa kwa kutaka kumpa mtu sumu
 
Tutakoma, sasa ni kutekwa, kutobolewa macho na kuvutwa na kutolewa kucha kwa kwenda mbele. Kufutwa kwa mashtaka ua Ugaidi kutamfanya Lwakatare na Chadema waone kuwa kumbe kuteka watu na kutoa kucha zao ni vitendo vinavyokubaliwa chini ya sheria...this is a mockery to the law!!!
Hacha kuisingizia CDM jilaumu mwenyewe kukubali kuongozwa na mtu wasiojua kila kitu!.

Wizara ya ulinzi (na tasisi zake) inafanya kazi gani mpaka hayo yanafanyika?.

Wizara ya mambo ya ndani inafanya nini?.
 
Hiyo inaitwa twanga kotekote hadi kwa masalia na maCCm,
kwa hili Zitto alikurupuka, inaweza kuwa kwa makusudi ama bahati mbaya, hii itakuwa aibu kwake na huyo gamba Msacky.
Mahakama imewaumbua watu kibao..TISS na wasiopenda haki, habari hii ni mbaya kwao!

lakini hivi zitto kweli aliiamini ile video mpaka aseme lwakatare ajiuzuru? No, labda kama alikuwa na plan B.
 
Last edited by a moderator:
Ni aibu kwa kiongozi mwandamizi wa chama kushtakiwa kwa kutaka kumpa mtu sumu
Ni aibu kubwa kwa kiongozi mwandamizi wa chama tawala kutengeneza ushahidi wa uongo dhidi ya viongozi wa upinzani na kushindwa mbele ya serikali yake aanayoiongoza.
CC: Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
mwigulu alivyokua anatoka povu alijua majaji wote wa ccm.!!



ameaminishwa kwamba majaji na polisi ni wa ccm. Nimtaarifu kwamba majaji wa ccm ni wale ambao hawana vyeti.eti mtu hana digrii ya sheria anateuliwa jaji.wanajulikana!!!magamba na mtandao feki bana!!!eti wanataka watawale milele.we acha tu.
 
tulishasema siku nyingi....harakakati za mabadiliko zinapofikia hatua ya juu kabisa ya kupevuka ni kama vile mama mjamzito anapofikia miezi tisa ya ujauzito wake. Katika khali ya kawaida, mama huyo akishafkia miezi hiyo, ni lazima atajifungua tu no matter what(mapinduzi ni lazima yatatokea no matter what). kumzuia asijifungua ni sawa na kuziba tundu la haja kubwa la mtu anayeharisha. ukiliziba tundu hilo kwa muda mrefu, say kwa kutumia chupa, halafu ghafla ukaja kulifungua baada ya muda, basi skizia hilo bomu la uha.o litakalokulipukia....ni kher ungemuacha tu mhusika ajisaidie haja yake kubwa taratibu kuliko kuiziba uje upate hasara ya kuoga na kufua, tena kwa jiki. haja kubwa ikishakuja ni lazima tu u.ye, no way, mama mjamzito akiishafikisha miezi tisa ni lazima tu ajifungue no way, yai likishakwiva ni lazima tu kuku atataga, no way.

khali ya kisiasa ya Tanzania ya leo ni kama mama mjamzito wa mimba ya miezi tisa(harakati za mabadiliko zimefikia hatua ya juu kabisa ya mpevuko), ni lazima tu mama ajifungue sasa (mapinduzi ni lazima yatokee sasa) no matter what....chemba, cris lukosi, nepi na wenzenu kasomeni french revolution ilikuweje, mapinduzi yale yalitokea katika kipindi na muda ambao yasingeweza kuzuilika tena, haja kubwa ilishabana mno, ilikuwa na lazima mtu ajisaidie tu.

nepi mnachoweza kufanya sasa si kumzuia mama mjamzito wa mimba ya miezi tisa asijifungue, bali mnachoweza kufanya ni kuangalia ni jinsi gani mtaweza kuji-adopt kwenye mazingira mapya ya siasa za kiushindani na hata ikiwezekana kuweka mazingira ya kushirikishana madaraka na wale waitwao vyama vya upinzani ili kila mwenye uwezo achangie katika maendeleo na ustawi wa mama yetu Tanzani (chambeche J. Mbatia) kwa kadri ya vipawa na uwezo wake bila kujali sana tofauti za kiitikadi na kimtizamo. kutumia nguvu nyingi haitawasaidia kwa sababu historia ipo wazi kuwa, kila unapokandamiza haki na uhuru wa watu ndivyo watu hao wanavyozidi ku-grow militant na kupinga kwa nguvu zote hATA IKIBIDI DAMU kumwagika. fuatilieni historia na harakati za ukombozi duniani kote. kwa haraka tu, je, kaburu aliua kina mandela wangapi? je kina mandela walijikunyata? palestina wamechinjina wangapi? je jamaa wamejikunyata?..hakika hakuna atakayejikunyata ni mpaka hapa HAKI, UHURU na USAWA vitakapokuwa accessible to all equally without fear or fevour...

haya, msijesema hamkuambiwa.........mene mene tekel perez:lol:
 
ni aibu kubwa zaidi kwa kiongozi kwa nafasi ya naibu katibu mkuu kutunga ugaidi ili umsaidie kisiasa.SHAME ON MWIGULU and YOU !
Ni aibu kwa kiongozi mwandamizi wa chama kushtakiwa kwa kutaka kumpa mtu sumu
 
Mungu akisimama hakuna mwingine awezaye! Hiyo iliyobaki ni rojorojo tuuuuuu..... CCM na polisi wao chali
 
Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa CHADEMA waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Mwanafamilia mmoja wa Lwakatare huku akibubujikwa machozi akasema mkono wa Mungu umeonekana dhidi ya shetani mtoa roho za watu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari,Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.
Mbombo ngafu!!
Hongreni lakini and may the better side win.
 
leo nipo radh kupata ban endapo tu nitaona gamba anaongea utumbo kweny h thread
 
By Tundu Lissu
Kitu kikubwa inachokithibitisha video clip hii, ukiachia njama dhidi ya CHADEMA na viongozi, ni jinsi ambavyo wahusika ni amateurs kwenye mambo hay a!!! Kwa maneno ya Sugu, 'wanahitaji kurudi studio', maana hii picha imeharibika!!!! !!!!
 
Haya sasa magamba wameshakula za uso mahakamaa kuu. Hakuna cha ugaidi wala ndugu yake na ugaidi, sasa Mwigulu aende akatoe ushahidi mbingu ya shetani kwakuwa anao kama alivyokuwa anapiga propaganda.

Tulishawaambia tangu mwanzo kwamba hii kesi imetengenezwa tu na hakuna substance ya kuifanya iwe kesi ya ugaidi, zaidi ya kuwa makosa ya kanuni ya adhabu lakini hawakutaka kuelewa, haya sasa mahakama kuu imewaumbua.

Sarakasi za DPP zimeishia wapi? Ni aibu kwa DPP na Mtu aliyemteua kwa kuteua mbumbumbu wa sheria, hapo inaonesha wazi DPP hana weledi zaidi ya kutumiwa na CCM, kulikuwa na mantiki gani kuifuta na kuifungua upya kesi ile ile na kisha kufutwa tena na mahakama kuu! Alistahili kujiuzulu, ila kwa kuwa alikuwa anafanya kazi ya kumpendeza bwana wake basi hata bwana wake (CCM na JK)hawana budi kumfutia kosa lake na kuendelea kumwache akalie hiyo ofisi
 
Ni aibu kwa kiongozi mwandamizi wa chama kushtakiwa kwa kutaka kumpa mtu sumu

Tehe tehe tehe tehe mpaka kesho asubuhi....Acha matumizi mabaya ya kichwa wewe....Hata Yesu alishtakiwa acha Rwakatare.....Hakuna aibu hapo aibu ni kwa waliomstaki kwa mashtaka ya uongo na ambayo hayapo!

 
Back
Top Bottom