Kuna watu humu ukiandika
mazuri ya CHADEMA na ukaandika mabaya ya CCM, wanakuona ni wa kawaida
kwa kuwa unaandika wanayoyapenda wao. Lakini siku utakapoandika mabaya
ya CDM na kuyasifia mazuri ya CCM, hata kama yana ukweli, watu watakujia
juu. Wanadhani ukiwa CHADEMA basi unatakiwa uwe mnafiki na kusifia kila
kitu hata kile chenye kutishia mstakabali wa chama.
Ninajua wengi hivi sasa wanapenda mageuzi na wanayatafuta kwa hali na
mali, kiasi cha kwamba wapo tayari kuona chadema inaingia madarakani
despite mapungufu yake. Lakini mageuzi ya namna hii yatatuumiza. kama
hatutaclear baadhi ya weakness zetu, basi tunaweza kuingia madarakani
halafu tukafanya vibaya kuliko hata hao CCM. Jifunzeni kutoka kwa
Fredrick Chiluba kule Zambia.
Ni lazima tujenge utamaduni wa kukosoana. Na ni lazima tutambue kwamba
CHADEMA kinaongozwa na binadamu wenye tabia kama za wale wa CCM.
Kunahitajika kuonyana na kukaripiana ili kurudishana kwenye mstari na
kuweza kujitofautisha na CCM. Kama tutaamini kila wafanyacho chadema ni
kizuri, na hata wakikosea tunatafuta namna ya kuyapaka mafuta makosa
yao, basi tutakimaliza hiki chama yumkini hata ikulu kinaweza kisiingie.
Tukosoane ili tujengane.
cc.
Kdm255