Mkuu Mndundu,
Nimekumbuka kitu kingine muhimu sana nilichokiona miaka hiyo ya 70 huko Lushoto.
Ilikuwa ikifika jioni, ilikuwa ni raha kuona magari ya mashindano yakipita kwa speed kali sana na yakiwa machafu si kawaida. Nilikuwa nashangaa hasa nikiyaona mchana, kwa nini yana taa nyingi namna hiyo. Baadaye nilipokuja yaona jioni yakipita ndipo nikajua. Unakuta taa zote zimewashwa na anakokwenda dereva inakuwa kuna mwanga mkubwa na wa kutosha.
Kama sikosei ilikuwa ni East African Safari Rally. Ni bahati mbaya sana haya mashindano yalikufa maana ilikuwa ni tangazo la nchi muhimu sana. Baadaye Wakenya walibaki peke yao na kama sikosei na wao sasa wameondolewa. Too sad.
Thanks for the pics, the Mkapa house is rather modest from what I expected.
Kuna mijengo ova Bavaria vile.Huku ndiko mijerumani ilikaa nini?
Hamna noma mkuu nilikuwa huko kwa likizo ya kama siku tatu hivi kwa kweli ni kuzuri sana na kuna matunda mengi.
Kwa mnaopajua vizuri Irente, hivi kile kituo cha watoto yatima bado kipo?
Mkuu hukufanya kuulizia huko plot zinakuwa bei gani.....walau Low density plot......?
ni kweli ndo maana pale mwanzoni mwa hekaheka za uchaguzi mkuu wa 2005 watu waliokuwa wakisemekana kuwa ni machaguo ya mkapa kugombea urais na ngwilizi alikuwemo kutokana na uswahiba wao. Mtu mmoja alituambia tulipokuwa lushoto kuwa hicho kiwanja alichojenga mkapa aliporwa mwananchi mmoja na akaambiwa asithubutu kupiga kelele. Sasa sijui kama ilikuwa hivyo kweli au watu waliongeza chumvi.
Magamba Secondary School ya enzi hizo na Mazinde Juu Secondary
thanks prodigal son... je kabla ya engineer hakulizwa mtu hapo??sio kweli ni vema kama jambo hulijui ukanyamaza na sio kuongea kwa kuhisi, ni kweli mkapa na ngwilizi ni maswahiba saana na yeye ndio alichangia mpaka mkapa akajenga huko,,historia ya hicho kiwanja kuna mkandarasi nadhani alikuwa mzungu alipewa dili la kujenga barabara hiyo ilikuwa ni site yake jamaa alijenga hapo nyumba nzuri tu za wahandisi wake na yeye mwenyewe alikuwa anaishi hapo, alipomaliza ujenzi zile nyumba zilikuwa zikabidhiwe wilaya, gwiliza kama unakumbuka ndo alikuwa boss wa tamisemi ndo akampa mzee,
kiwanja hakunyanganywa mtu kama unavyojaribu kueleza hapa
Kwa mnaopajua vizuri Irente, hivi kile kituo cha watoto yatima bado kipo?