Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,673
- 22,264
Katikati ya mwaka huu yaani 2023 mwezi wa sita nilikwenda hospitali ya Aga Khan iliyopo Sea View Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu, kama taratibu zilivyo niliwasilisha kadi yangu ya bima ya afya ilipokelewa na nikapewa jibu kuwa siwezi kutibiwa kwenye hospitali hiyo!
Haikuwa shida kwangu, nikaenda hospitali ya Shree Hindu Mandal iliyopo Upanga na nikapata tiba kwa kutumia kadi hiyohiyo.
Mwezi huu wa kumi nilienda kwenye tawi la hospitali ya Aga Khan lililopo uswahilini na nikisema uswahilini ni uswahilini kweli kwani madakitari, manesi na wafanyakazi wengine ni waswahili wenyewe wanakiri wahindi wa uzao wa Aga Khan hawakanyagi huku uswazi!
Baada ya kupata tiba kwenye hilo tawi letu la hospitali ya Aga Khan nikamuuliza dakitari kuhusu hospitali mama ya Sea View, naye hakusita kuniambia kuwa kule ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa serikali, nikajua kuwa ukiwapendelea hawa basi jambo lako litakwenda vizuri bila kuhojiwa.
Miaka iliyopita tulikuwa tukitibiwa bila tatizo kwenye hospitali hiyo ya Aga Khan Sea View licha ya tatizo la hawa wazalendo watanzania wenzetu kutokujua kiswahili vizuri, lakini walipoona tunawabana wakatufungulia matawi uswazi na madakitari wetu wakiswazi tumaliziane huku huku.