Lushoto: Irente view point hotel, Mazinde Juu,Magamba na Nyumba ya Mkapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lushoto: Irente view point hotel, Mazinde Juu,Magamba na Nyumba ya Mkapa

Discussion in 'Jamii Photos' started by Mndundu, Sep 18, 2009.

 1. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Irente View Point Hotel iliyopo Lushoto (mazingira ya Nje na Ndani ya Vyumba)
   

  Attached Files:

 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kali sana...unajua bei kwa usiku mmoja? Unaweza enda jificha huko na mke wa mtu week end mojawapo!
   
 3. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mazingira ya Lushoto vijijini, kivuko cha kusafirishia magogo na jiwe lenye alama ya unyayo wa mguu (nadhani wenyeji wanaita unyayo wa Mungu kama sijakosea)
   

  Attached Files:

 4. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mzee executive suites ni laki moja kwa siku nilipoenda mwaka jana
   
 5. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Magamba Secondary School ya enzi hizo na Mazinde Juu Secondary
   

  Attached Files:

 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naomba bei za kulala hapo nataka nije vekesheni Lushoto.
   
 7. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nyumba ya Rais mstaafu kwa mbaaaali na maporomoko ya maji (water fall) yaliyo njia ya kwenda kifungiro
   

  Attached Files:

 8. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hotel ya Muller`s ambayo inapakana na nyumbani kwa Rais Mstaafu Mkapa
   

  Attached Files:

 9. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu kwa Picha. Nilishawahi kufika Lushoto zamani saana. Nilipandishwa kwenye basi la East Africa Railway (mabasi meupe na mstari mweusi) na sister wangu tukiwa na mwanae. Tulisafiri na kijana mmoja kama Kondakta wa Bus aliyeonekana kufahamu tunakwenda wapi maana tulikuwa below 5 years. Tulipoingia tu mwanzo wa mji (kulikuwa na barabara ya lami na taa za barabarani) basi likasimama na tukashushwa na hapo kulikuwa na kijana aliyekuja kutupokea. Alituchukua hadi kwa babu mmoja akienda kwa jina la Mzee Mtangi. Nyumba nakumbuka ilikuwa eneo la milimani, nyasi safi kabisaa. Babu alikuwa na kigorofa chake miaka hiyo ya 70 na mke wa Kizungu juu. Tulikaa wiki mbili na tukarudishwa tena Korogwe kwa njia hiyohiyo.

  Natamani siku moja nirudi tena nilione hili eneo. Lushoto kwa kweli ni pazuri saana na ukichukulia hali ya hewa na mimea inayoota hapo, kweli mtu unapumzika saafi sana.
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  yeah - thank you - the photos are splendour
   
 12. k

  katoto Member

  #12
  Sep 18, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mdundu,
  Asante kwa kunuikumbusha shule ya Magamba, nilikuwa hapo hadi mwaka 1989.
  Na ile irente view inanikumbusha enzi hizo hii hotel haikuwepo, lakini tulikuwa tunashuka pale mlimani kwa miguu kwenda likizo (maalufu kama kupiga jumbo). Headmaster alikuwa mzee Dimoso!!!

  Naona na Skyline ya shume
  Wao, hakuna shaka Lushoto ni eneo zuri sana kwa utalii. Kama huna pesa nyingi kukaa Irente View nenda ukae loans hotel, nadhani bado ipo.

  Katoto.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
 14. m

  masaiti Senior Member

  #14
  Sep 18, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimefurahi sana kuziona picha hizo.
  Lushoto ni sehemu nzuri sana hasa kwa utalii, nilifika huko miezi michache iliyopita na
  sikuamini jinsi kunavyopendeza.
  Watanzania ambao bado hatujafika, tujaribu siku moja kutembelee na tukajionee wenyewe.
  Vivutio ni vingi. Tutembelee jamani
   
 15. p

  p53 JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nilifika Lushoto mara mbili.Kwanza nikiwa high school siku hizo dada yangu anafanya kazi pale.Nili enjoy sana manake sister anafanya bank halafu alikuwa well known yani ukijitambulisha kuwa ni kaka yake basi totoz wote wako!
  Then wakati nafanya chuo kikuu ilikuwa ni fieldwork wiki 2 pale NIMR.This time nikiwa na 'boom' langu la field nikapanga chumba cha peke yangu halafu nikaingia mtaani nikakamata toto moja saafi la kisambaa basi kila usiku nikawa namega kisela.Wiki mbili zilikuwa kama siku moja babako
  Lushoto wacha kabisa mshkaji unaweza kulowea!
   
 16. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Yeah, Lushoto pazuri sana nilikuwa huko mwaja jana na nilifika hapo Irente View Point Hotel kweli panapendeza. Mji ulivyokaa ni kama Geneva tofauti tu ni majengo. Ukiwa pale nyuma ya hiyo Hotel kuna jiwe ambalo ukikaa juu yake unaiona vizuri barabara ya Dar - Arusha na ni parefu sana, yaani kama uko angani vile na mtu akiteleza hapo ndoo basi tena wataokota vipandevipande huko chini.
   
 17. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hapo jirani na nyumba ya Mkapa pia kuna nyumba ya Ngwilizi. Tena inasemekana ndo aliyemtafutia hicho kiwanja.
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mafisadi wanajuana kwa ufisadi wao na kulindana.
   
 19. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni kweli ndo maana pale mwanzoni mwa hekaheka za uchaguzi mkuu wa 2005 watu waliokuwa wakisemekana kuwa ni machaguo ya Mkapa kugombea urais na Ngwilizi alikuwemo kutokana na uswahiba wao. Mtu mmoja alituambia tulipokuwa Lushoto kuwa hicho kiwanja alichojenga Mkapa aliporwa mwananchi mmoja na akaambiwa asithubutu kupiga kelele. Sasa sijui kama ilikuwa hivyo kweli au watu waliongeza chumvi.
   
 20. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kwa mnaopajua vizuri Irente, hivi kile kituo cha watoto yatima bado kipo?
   
Loading...