asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,039
EMT Actually inaweza ikawa nzuri au mbaya kutegemeana na matumizi.
-VE
. .Inachangia uchovu wa akili.
Sadly mimi ni mmoja wa watu ambao huwa wanaishia kulala na kuacha tv on. Ukiamka asubuhi macho yanakuwa machovu pamoja na akili kwasababu ya kelele na mwanga.
. .Inasababisha mtu achelewe kulala.
Ukiwa nayo chumbani unashawishika kuangalia na kuangalia na kuangalia hata kama muda uliopanga kulala ulishafika, kwasababu tu ipo karibu.
. . Inaweza kupunguza mawasiliano kati ya wanandoa wawapo chumbani. Badala ya kupiga story na kuchombezana wakati mnautafuta usingizi mama yuko busy na tamthilia/baba yuko busy na news BBC hata kusumbuliwa.
+VE
. . Inapunguza sababu ya mtu kuishia kulala kwenye kochi/sofa na kuambulia maumivu ya shingo na mgongo.
. . Inaweza kuongeza ukaribu kati ya wanandoa.
Badala ya mmoja kubaki sebuleni akisubiria sijui kipindi gani huku mwenzie akienda kubembeleza usingizi peke yake mnaongozana na kama mko vizuri hicho kipindi kinaweza hata kisiangalike.
. . Ukaribu + +
Kama sio wabinafsi mnaweza kujikuta kila mmoja anajenga interest na kile anachopenda mwenzake (mf movie, tamthilia, michezo, habari n.k) kwenye tv kitu ambacho kitaongeza mambo ya ninyi kuzungumzia.
. . Distraction
Bila kusahau kelele kidogo ili kuficha wakati wanandoa wanajishughulisha.
Nadhani jambo la muhimu ni watu kujiangalia tu na kujua walivyo. Wengine inafaa zaidi wawe nazo chumbani, na wengine haifai.
Daah kule ni noma....miaka ya nyuma nilimpeleka mgeni wangu pale nikamsindikiza chumbani...sasa kwenye kypigapiga stori mbili tatu si nikawasha tvii!!!daah almanusura nivunje tv yao!!nilikutana na sarakasi za kufa mtu...imagine mgeni mwenyewe tulikuwa tunaheshmiana ile mbaya
.Kama mtu anaweka TV chumbani na haitumii kwa muda wa mwezi mzima, then haistahili kuwapo pale.
Unless hulali humo chumbani, it becomes redundant and it should be removed.
Tena inaweza hata kuleta vumbi chumbani maana itakuwa imefungwa tuu huko.
Break down the experience for us then.
.....kelele si kwa kupigana tu mkuu,
Hata 'mazungumzo' mwaweza jisahau mkajikuta mwapiga kelele...
tv chumbani hapana aisee
chumbani sehemu ya kupumzika na kupumzikiana, na kushusha stress au kuonyesha furaha
no tv
Namshukuru Mungu sijawahi kusumbuka na watoto.... wanajua watafanya kitu ambacho mimi nataka wafanye.....
chumbani kwao kuna TV na games za kila aina but wanajua games wanaruhusiwa kucheza weekends tu, kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili, siku za wiki no games.
TV wanaangalia kila siku, wakimaliza homework wanachagua kucheza nje au kuangalia cartoon, but muda wa mwisho ni pale wanapoenda kuoga, wanakula na kulala saa 1 na nusu wakichelewa sana saa 2. sijawahi sikia nung'uniko kuwa wanataka kucheza game wala kuangalia TV muda ambao sio wa kufanya hivyo. wanaheshimu na wamekubaliana na kila kitu.
Usiniambie team ikishindwa hata strip teasing haiwezi amsha vilivyonuna??????
Kuna haja ya kuwaelimisha watoto jinsi ya ku-share vitu. If the programme is so important then, siku hizi unaweza kurekodi hata vipindi wakati unaangalia vipindi vingine bila interruption.
In fact, badala ya watoto na wazazi kujikita in the house muda mwingi wakigombania TV, they should get out there. It might be much better healthy.
But at the end of the day, ni option ya mtu of course, though the fact kuwa watu wengi wanapendelea multi-room TV installation sidhani kama ina-convince niweke TV chumbani.
Najua baadhi ya familia ambazo hazima hata TV moja nyumbani pamoja na kuwa wana uwezo mkubwa tuu wa kuwa nazo.
Wala sidhani kama ni uamuzi radical bali ni watu tuu kuamua wanachokitaka zaidi maishani mwao. Tena that can be supplemented na shughuli nyingine kama kusoma vitabu zaidi, kupika, kuwa na muda mrefu wa mazungumzo, kufanya training za aina mbalimbali na kulala.
Faida za kutokuwa na TV kabisa ni pamoja na ku-save pesa, kutoangalia matangazo ya biashara (love this one), kutumia ule muda ambao ungeangalia TV kwa kuwa more more creative, n.k.
Hata hivyo, inahitaji commitment sana, udhubutu, kuwamua kwa pamoja na siyo maamuzi ya mtu mmoja tuu, kuweka angalizo na kuweka time frame kama ile ya kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe. You cant just stop watch TV just like that kama umeshaizoea.
Ila kwa sie wapenda soka, kwa kweli kuacha kuangalia TV kabisa inabidi pia kuacha kabisa kufuatilia soka which is extremely difficult thing to do for me personally.
kwa sisi tuliokuwa na wake wenye mishahara mikubwa kuliko sisi ni bora miaka 100 kuwa na Tv chumbani maana ukimgusa mkeo akikukaripia basi unachukua series yoyote ya kikatili na kuiangalia ili ujifanye umesahau kumbe unaumia.
Nalog off
Me ambaye niko single TV inanifariji sana
TV zinachangia sana kuweka distance kwa watu wanaoishi pamoja. Nakumbuka wakati nakua, tulikuwa hatuna TV ana were extremly close. Tunakaa tunapiga story hadi saa nne. Tena kama ni wakati wa likizo hadi hata saa 6. Sasa nikijiuliza huwa hata sielewi tulikuwa tunaongelea nini.
Hata sasa huwa naona umeme ukiwa umekatika, hasa nyakati za usiku. Najikuta nasimulia watoto hata mambo ambayo hayana maana niliyokuwa nafanya nikiwa mdogo, havina maana, lakini vinawafanya watoto wakujue zaidi.
Siku hizi hatuna hata muda wa kusimulia watoto hadithi, matokeo yake watoto wanafundishwa hadithi na TV, lakini hadithi hizo zi za asili yetu ni imported. Ndio maana unakuta mtoto msukuma lakini hajui hata hadithi moja ya kisukuma wala utamaduni, anachojua ni Ben 10 na Santa Claus.
Ha ha ha. Na hio ndio kazi yake - Kukutia hamasa kwa kile kilichokupeleka pale:wink2:Kule NAMNAANI mbona runinga ndio mhamasishaji mkuu?
ukishaoa tu tv tupa kule,
chumbani ni sehemu ya faragha na mkeo
tena mkiwa uchi
ngozi kwa ngozi
mcheze, mcheke, mpeane mahaba mtaniane mfurahiana
ndo sehemu ya kupanga mipango, mipango ya chini ya shuka achana nayo, ukitoka hapo una nguvu kubwa ya kwenda kutekeleza
ndo sehemu ya kufarijiana na kujaza ulimwengu kwa nafasi,
nyie wawili ni tv tosha, hamuitaji tv nyingine kwanza zitawapigia makelele kama sio kuwamulika na kuwaumiza macho
mke mwenza unamwaga point aisee......
siku hizi kitoto cha miaka 3 kinalilia katuni
hakuna bond kisa tv, sasa ikiwa chumbani si ndo balaa?
Mhh speechless