Faith
Member
- Jul 9, 2008
- 52
- 11
na Eugenia Kimolo
KESI ya madai inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency International, Hashim Lundenga, inatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Jagalile Mwaseba.
Kesi hiyo iliyofunguliwa Agosti 5, mwaka huu na mke wa Lundenga, Twigi Hashim Lundenga, mlalamikaji anataka kugawana mali walizochuma pamoja na mumewe huyo, baada ya kumtelekeza na familia.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Septemba 3 mwaka huu, Ritha Tarimo alimtaka mwanasheria wa mlalamikaji (Twigi), kuwa anatakiwa kuwasilisha pingamizi la majibu yaliyoletwa na wakili wa Lundenga, Audax Kahendaguza.
Licha ya kuwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Lundenga, pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga.
Pamoja na dini ya Kiislamu kumruhusu Lundenga kuwa na mke zaidi ya mmoja, kinacholalamikiwa mahakamani hapo, ni madai ya Lundenga kuitelekeza familia ya mke wake wa kwanza, baada ya kuoa mwanamke mwingine, aliyewahi kuwa mmoja wa warembo wa Mkoa wa Tanga mwaka 1997.
Inadaiwa kuwa, baada ya Lundenga kumwoa mwanamke huyo wa Tanga, alihamia katika nyumba mpya iliyoko Sinza, ambayo aliijenga akiwa na mke wa kwanza, huku akiitelekeza familia ya mke huyo na kusababisha atinge mahakamani.
source Tanzania Daima - Sauti ya Watu
Tanzania Daima - Kesi ya Lundenga kuitosa familia leo