Lumumba kwafukuta; Ya Dodoma yaanza kutoa cheche

Lumumba kwafukuta; Ya Dodoma yaanza kutoa cheche

watakuwa wamekuvuruga wewe hapo mtaa wa ufipa. hivi ukiwa msukule huna hata akili za kwendea chooni?

Tangu makada warudi toka Dodoma (mimi nilitangulia kurudi Dar es Salaam), hali si shwari ndani ya Ofisi Ndogo za CCM hapa Lumumba. Makada wanapingana kimakundi yaliyopata na kukosa ushindi kule Dodoma. Wapo makada wenye tabasamu la hamu na wale wenye sura zilzosheheni hasira. Hali si ile. Imebadilika.

Kazi zinakwenda polepole na hata hakuna wa kumuuliza mwingine kwa staha na raha. Maneno na matendo ya makada yamebadilika. Utaniutani uliokuwa ukituunganisha,umepungua na kuonekana unasumbua. Sasa ni urafiki wa kinafiki tu. Kwa werevu,tunayaona makovu ya Dodoma. Yanafanya kazi sasa. Kununiananuniana ofisini kumekwamisha hata Redio Uhuru kutenda kazi zake ipasavyo. TCRA wanaivizia kuifunga kwa kutolipa kodi. Kodi imekwamishwa.

Viongozi mpo? Hali si shwari chamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Kichaka kimeanza kufuka moshi bado kidogo kiwake mtatafutana mliingia kwa njia moja sasa mtatoka kwa njia saba, mmeshindwa kutenda haki juu ya taifa mmekuwa walafi na kujiona kama nchi ni mali ya familia mateso wanayopata watanzania imekuwa kama mziki mtamu masikioni mwenu. Acha Mungu aitengeneze Tanzania yenye matumaini turudi kwenye haki na neema aliyotupa hakika kwake hakuna lililogumu Asante Mungu kwa 2015!
 
Mtahangaika sana ila CCM imeshamaliza kazi subiri Mbowe na SACCOS yake awaletee mgombea maana hamjitambui mnaenda kama gurudumu la gari CCM ni democrasia daima hakuna kuzunguka kama gudurumu la gari lisilojua kuwa linatakiwa kwenda wapi? Mnashabikia wizi wa kwenye SACCOS ya Kichaga bado mnafurahia kisha wajifanya mwajua kila kitu!!!
 
Nimewaona na vijana wa vyuo vikuu boom limewaishia wakajitoa ufahamu kuwahi fasta mafao yao! Duu SACCOS imekabwa koo na Mayuda Eskariote!
 
Tangu makada warudi toka Dodoma (mimi nilitangulia kurudi Dar es Salaam), hali si shwari ndani ya Ofisi Ndogo za CCM hapa Lumumba. Makada wanapingana kimakundi yaliyopata na kukosa ushindi kule Dodoma. Wapo makada wenye tabasamu la hamu na wale wenye sura zilzosheheni hasira. Hali si ile. Imebadilika.

Kazi zinakwenda polepole na hata hakuna wa kumuuliza mwingine kwa staha na raha. Maneno na matendo ya makada yamebadilika. Utaniutani uliokuwa ukituunganisha,umepungua na kuonekana unasumbua. Sasa ni urafiki wa kinafiki tu. Kwa werevu,tunayaona makovu ya Dodoma. Yanafanya kazi sasa. Kununiananuniana ofisini kumekwamisha hata Redio Uhuru kutenda kazi zake ipasavyo. TCRA wanaivizia kuifunga kwa kutolipa kodi. Kodi imekwamishwa.

Viongozi mpo? Hali si shwari chamani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kwani wewe umekuwa ccm tangu lini nadhani imefika wakati tukutaje kwa majina yako mpaka ulipo ili ujue kuwa tunakujua wewe ni bavicha tena kwenu tunapajua mpaka unapofanyia kazi hata jina lako halisi unalotuia humu jf tunarijua.
 
Unabii wa Askofu Zachary Kskobe lazima utimie. Sisi hatuna wasiwasi wala mashaka yoyote kuhusiana na barua yake ya wazi ambayo alimwandikia Rais Kikwete akielezea mafarakano yatakayotokea ndani ya ccm. Barua hiyo ipo mitandaoni. Ukiitafuta kwa kuandika BARUA YA KAKOBE, WARAKA WA KAKOBE, KAKOBE AMWANDIKIA BARUA RAIS KIKWETE, n.k. Ukiitafuta na kuisoma vizuri, utaelewa kinachotokea sasa. Barua hiyo ni ya tarehe 10/ 03 / 2014. Aliiandika na kuiweka wazi kama Mungu alivyomuagiza. Tafadhari, nakuomba uipitie barua hiyo ili ujue yale yanayokwenda kukipata chama tawala. Mungu aliahidi kuwachafulia usemi wao. Inaeleza kuwa katika vikao vyao watatofautiana, n.k. Hakika Nabii hakosi heshima isipokuwa katika Nchi take mwenyewe. TUKO PAMOJA BABA YETU ASKOFU ZACHARY KAKOBE. WEBSITE: Home - Bishop Zachary Kakobe International Ministries
 
Kwani wewe umekuwa ccm tangu lini nadhani imefika wakati tukutaje kwa majina yako mpaka ulipo ili ujue kuwa tunakujua wewe ni bavicha tena kwenu tunapajua mpaka unapofanyia kazi hata jina lako halisi unalotuia humu jf tunarijua.

Usipanic bwa'mdogo. Kaka zako walianza kuruka ruka kama kuku aliyekatwa kichwa...jinsi yako. Wameufyata. Utaelewa tu.
 
Mzee Tupatupa, mbali na ujumbe murua katika post zako, nakupongeza sana kwa umahiri wako wa kuandika na kwa matumizi ya lugha kwa ufasaha mkubwa. Cheers!!!
 
nikuvute-vuta

Hahaha Bahati Furaha,pole mie na VUTA-Nkuvute watu wawili tofauti,na wala kwa uhakika siwezi vaa viatu vyake,kiumri,kiuelewa maana yeye ni MWANASIASA na MWANASHERIA,mie ni MUHASIBU...............Pole sana
 
CCM wanamsubiri mzinzi wenu wamburuze tena kama 2010, ajiandae tu kususia sherehe za kumwapisha Pombe.

Mbona hata huyo ni MZINZI pia!Kumbuka aliamua kuitoa NYUMBA ya SERIKALI KUMPA KIMADA....................Ufanyalo usiku mchana litaonekana......................
 
Kwani wewe umekuwa ccm tangu lini nadhani imefika wakati tukutaje kwa majina yako mpaka ulipo ili ujue kuwa tunakujua wewe ni bavicha tena kwenu tunapajua mpaka unapofanyia kazi hata jina lako halisi unalotuia humu jf tunarijua.

acha mikwara Nepi Na Yule
 
Back
Top Bottom